Jokofu langu linaniumiza kichwa, kili likiongezwa gesi baada ya siku 3-4 halifanyi kazi tena

BradFord93

JF-Expert Member
Oct 11, 2017
910
2,164
Nina jokofu aina ya bird line....mwanzo lilikuwa linapiga kazi fresh..

Nikaita fundi wa kwanza akasema tatizo ni power control na gesi imepungua, tukarekebsha ikafanya kazi fresh

Siku 3 tu likazingua linawaka ila haligandishi nikaita fundi akasema yabidi system nzima isafishwe na iwekwe gesi mpya, nikasema poa. Tukasafisha system nzima na likawekwa gesi. Likapiga kazi siku 4 ghafla limkaa kimya. Linawaka lakini haligandisha

Leo ndo nimekaa chini na kufikiria litakuwa linavujisha gesi. Hao mafundi walichofanya ni mbwembwe ila kikubwa ni kuwa waliongeza gesi tuu.

Nahitaji fundi jokofu wa uhakika acheki kama kuna ufa na kama linavujisha pia azibe..

Namba zangu ni 0769011871
Fundi awe maeneo ya Airport mpaka Gongo la mboto
 
Niamini Mimi...hilo friji tupa

Hiyo hela ya kuwapa mafundi ongezea nunua friji mpya!..Ni hayo tu


Sent using Jamii Forums mobile app
Jina la kampuni ya hilo friji litakuwa kimeo...

Kuna friji nililinunua kwenye mnada kwenye ubalozi flani la boss ninalo kama miaka 10 sijawahi kulijaza gasi, halijawahi kuguswa na fundi.. masaa 7 nagandisha barafu ngoma inatoka jiwe
 
Me binafsi kitu cha electronic huwa kikiaribika tu natafta na mteja. Sitakagi ujinga.

troublemaker 2019. all right received.
 
Niamini Mimi...hilo friji tupa

Hiyo hela ya kuwapa mafundi ongezea nunua friji mpya!..Ni hayo tu


Sent using Jamii Forums mobile app
Na akanunue jipya kweli lenye warranty (sio yale used yanaouzwa vichochoroni).
**halafu friji tu linakuumiza kichwa siku unamiliki gari ya maana (sio IST sijui Passo) halafu ikazingua ukaambiwa kutengeneza ni 3m si ndo utakufa kabisa.
 
Back
Top Bottom