Jokofu (Friji) gani linatumia umeme kidogo na inawahi kupoza?

Wizobaby

Member
Dec 3, 2011
41
8
Mwanzo nilikuwa natumia super general. je, bado zipo sokoni
Kwa Dar? zinapatikana maeneo gani? Je, kuna fridge nzuri zaid ya super general

images (2).jpeg
 
Kama walivyoweza sema wengine kama unataka efficiency nenda mpaka kwenye A+++ ndio itakufaa
 
Kuna aina mbili za Fridge mkuu,

Kwanza kuna zile ambazo ni lazima zitoe au ziweke mabarafu kwenye kuta zake kwa ndani ili zipoze vizuri. Aina hii ya fridge inatumia umeme mwingi sana na inapotokea umeme umekatika huwa zinamwaga maji yatokanayo na kuyeyuka kwa barafu.

Pili kuna za kisasa ambazo ni Nonfrost ambazo haiziweki mabarafu kwa ndani bali zinagandisha au kupoza kilichohifadhiwa tu ndani yake mfano kama juice au maji na pia zinatumia umeme mdogo sana kwakuwa zimetengenezwa kwa mfumo wa energy saver.

Mwisho unapokuwa na Fridge ili kuitunza na kuendelea kuitumia vizuri ni muhimu sana kuwa unatumia ile nob ya kuongeza au kupunguza ubaridi wa ndani kulingana na hali ya hewa, Kuna kipindi cha joto kali na Kuna kipindi cha baridi pia. Mfano kama mtu anaetumia kwa dar anaeza akaseti kwenye no 5 na kuendelea na mtu anaetumia kwa mikoa Kama Singida Arusha au Mza anaeza akaseti kuanzi no 2, 3 na 4 na akapata kitu murua kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Try LG mkuu, utaleta mrejesho mwenyewe.

Ila toa hiyo "TETESI" basiii 😂😂
 
Kumbe, sasa likiwa dukani utalijuaje?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom