Joker Film: Kudharauliwa na kuambiwa maneno mabaya kunavyoweza kumfanya mtu awe muuaji

Da'Vinci

JF-Expert Member
Dec 1, 2016
35,677
106,786
imageshwdhjg.jpg


Tarehe 4 october 2019 Marekani muvi inayoitwa Joker ndio siku ilipotolewa officialy, kabla ya kuachiliwa mwezi september 18 jeshi la marekani ilisambaza ujumbe wa e-mail kuwapa tahadhari wamiliki wa kumbi mbalimbali zitakazo husika kuonyesha muvi hio kuchukua tahadhari wakati wa kuionyesha..Vinyago,nguo au kuvaa kitu chochote kinachohusu muvi hiyo ya joker ilikatazwa. Tena wakati wa kuionyesha kulikua na ulinzi madhubuti ili kudhibiti tukio lolote litakalo jitokeza. FBI , US Homeland Security waliingia kazini kuhakikisha hakuna mauaji au uvunjifu wa amani utakaotokea wakati muvi hii inaoneshwa.

Lakini kwanini haya yote yanatokea? Turudi nyuma kidogo..
July 20 mwaka 2012 kwenye ukumbi wa Century 16 Theater Aurora corolado kulikua kunaonyeshwa muvi ya Batman: The Dark knight rises (Tukumbuke muvi hii ilikua mwendelezo wa muvi ya Batman: The Dark Knight ilitoka mwaka 2008 ambayo Heath Ledger alicheza kama Joker). Basi bwana, usiku wa manane watu wako wanafurahia kuiangalia muvi jamaa mmoja akakiwasha ndani, ilikua hivi.

Jamaa mmoja anaitwa James Eagan Holmes alinunua tiketi hapo ukumbini akaenda zake kukaa siti za mbele kabisa, baada ya dakika 20 Holmes alitoka nje kwa kutumia mlango wa kutokea uliokua pembeni ya screen, mlango huo ulikua unatokea moja kwa moja kwenye parking ya magar mlango aliuacha wazi kidogo akaenda hadi kwenye gari lake na kubadri nguo...Baada ya dakika 10 alirudi kupitia ule mlango wa kutokea kavaa nguo za kujikinga huku usoni kavaa mask ya kujikinga huku akiwa na bunduki.

Alikua kavaa vitu vingi vya kujikinga mwilini mwake hafu alikua kavaa earphones anasikiliza muziki ili asisikie watu watavyokua na taharuki, kulikua na watu 400 ukumbini. kimuoneka alionekana kavalia kama watu wengine walivyo vaa kama Joker..jamaa akaanza kumwaga vitu risasi, akatupa mabomu ya gesi kwa ufupi jamaa aliua watu 12 na Kujeruhi wengine kama 58.

Mwisho wa siku jamaa alidakwa akakubali kua ni kweli kaua yeye ila akasema alikua na matatizo ya akili na uchunguzi ulionyesha kua jamaa hakua normal ila hawakumuacha. August 26 2015 jamaa alihukumiwa kifungo cha maisha mara 12, yaani kila mtu mmoja aliyemuua alibeba thamani ya kifungo kimoja cha maisha (x12). Mwisho kabisa akaongezewa miaka 3318 kama fidia kwa wale wote alio wasababishia madhara. Kiufupi hata akifa huyu bado anadaiwa miaka na miaka, hata akienda peponi itabidi afikie jela.

Huyu Joker ni nani hasa?
Jaquin Phoenix ndio kacheza kama joker, joker alikua ni mtu amabae alikua na matatizoo ya akili kutokana na makuzi aliyokulia ya kunyanayapaliwa na jamii, pia huyu joker alikua anatatizo linalofahamika kama pathological laughter, yaani mtu akiwa na tatizo hili anakua kwenye tatizo la kuhudhunisha yeye halii anachekaa tu au kwenye tatizo la kufurahisha yeye analia mpaka basi. Ikitokea umemuudhi basi atacheka weeee bila kujizuia. Kutokana na kudharauliwa kwenye jamii alikuja akawa mtu mbaya hasa anashawishi hatawatu kufanya matukio nao wanamuelewa. Ndiyo maana FBI walikua siriazi sana kwenye kuimarisha ulinzi wakati muvi hii inatolewa maana inahamasisha watu wanaodharauliwa kwenye jamii kufanya mambo ya hatari ili kulipa kisasi kwa ya wanayotendewa kwenye jamii na familia.

Twajifunza nini?
Waleeni watoto wenu vizuri mkiwapa maneno ya ushindi na kutia moyo hata kama unaona mwanao hana uwezo mkubwa, we unamwita mwanao we mjinga njoo hapa,we mpumbavu, we zezeta njoo n.k. Jamani mimi nikiwa namwanangu mtu akimwita hivo tutauana haya maneno nayajua uchungu wake na madhara yake nayaona mpaka leo. mtoto anakua hana imani na maisha, anajiona hafai kwenye jamii mwisho inampelekea kua na msongo hata ufikiri wake unayumba mwisho anaanza kutenda maovu ili kulipa machungu ya maneno anayoambiwa.

Treat your son like king not like a asshole. Mentality disturbance za watoto zinaharibiwa nanyi wazazi. 5yrs ago nilisoma soma Psycology upande wa tabia za binaadamu na makuzi yake toka akiwa na wiki 2 baada ya mimba kutungwa hadi umri wa miaka 70 nafahamu vyema sana, Kwenye Behavioural model tabia za binaadamu zimegawiwa katika makundi matatu makuu:​
  • Agressive: Huyu mtu aliye kwenye kundi hili yeye jambo dogo analikuza linakua kuubwa (amplifying), kila kitu yeye anamind...mara nyingi hua wanajitanguliza wao kwenye vitu hawajali wenzao nk nk.​
  • Passive: Hawa ni wale watu wa kuchukulia poa hawana shida na watu wao ukiwaudhi wanatabasamu tu. Mark zuckenburg, Wentworth Miller (michaelscolfied) hili kundi ndio husongwa na Msongo zaidi​
  • Assertive: Hawa wao wako tayari kufanya chochote kwa ajili ya wenzao hata kupoteza maisha..wanachukulia wengine ni wathamani kuliko wao. mf Jesus, Nyerere,All freedom fighters.​

Sasa fikiria mtu wa kundi la kwanza umemtendea mambo mabaya huyu lazima awe mbaya mbeleni tu si mnajua alichofanya hitler ajili ya kudharauliwa,akina Mao tsetung, serial killers wote, lakini kwa watu wa kundi la pili hua tofauti wao hua wanayatumia yale madharau wanayofanyiwa kufanya vitu kuwathibishia watu kua wao sio wajinga.

Mfano Mark wa Facebook alikua wanamchukulia poa sana kipindi yuko chuo ila ukizingatia kwa walikua maskini ila leo hii walio mdharau wako wapi? Thomas Edison hadi mama yake aliandikiwa barua na uongozi wa shule kua hana akili, mwisho kabisa kawa ndio mgunduzi na mfanyabiashara mkubwa sana kwenye maswala ya electrnonic na electricity. Akina Eminem leo hii wako level ipi? Wentworth Miller hadi sasa kutokana na kuwa abused hata hajielewi tena jinsia yake inataka nini (leo gay kesho mwanaume) mifano ni mingi mno.

Jamani wazazi wa leo na wazazi watarajiwa hatima ya mafanikio ya mwanao kiuchumi au kiakili yapo mkononi mwako, mwambie mema sio kumwambia mwanao maneno yanayo mfanya ajione inferior, hana thamani matokeo yake hua ni mabaya sana. Hata Jesus watu walimbeza ila mwisho wa siku kabaki kua ndio binaadamu ambae historia yake haitafutika kwa aliyoyatenda. Usimdharau mtu wala kumkandamiza hatujui hatima zetu. Serial killers wengi chnzo hua ni ugonjwa akili ambao unasababishwa na malezi mabaya.

Kuna kitabu kinaitwa What to say when you talk to yourself by Shad Helmstetter, kisomeni kinaweza kuwapa muongozo wa mambo ya kuongea wakati mnawasiliana na watoto wenu.

Yangu ni hayo tu!!
Vinci
el maestro
heath.jpg
 
Kila siku tunawaambia msiwapige watoto viboko mashuleni vinawaharibu kila kitu!

Hata Magufuli naamini alikuwa abused sana utotoni!

Lazima alipitia utoto wenye machungu sana!
Tena kwa wazazi wa kiafrika ndio hua hawajali wala nn wao wanajali mtoto ale akue tu.. mengine hapana.
Magufuli yupo kwenye kundi la watu wanaojifanya wema mbele za watu lakini kwa ndani kuna ubaya. Kama alivyokua Mao Tsetung..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom