Joke: Ingekuwaje bible ingeandikwa ktk mazingira ya leo?

Next Level

JF-Expert Member
Nov 17, 2008
3,153
176
I got this as forwarded sms from ma friend!

Kutokana na ukweli kwamba vijana wengi hawapendi kusoma bible, umefika wakati bible ingetakiwa iandikwe upya kwa kiswahili cha kisasa zaidi (watumiacho vijana) ili iliwavutie vijana wengi zaidi waisome na wapate wokovu. Mfano bible ingekuwa na verse kama hizi;

Yesu akawaibukia masela wake na akawapa laivu, Oya washikaji mi ndo naenda kwa dingi, ila ndo hivo msikandamizane, msipige fix, msimind mademu wa washikaji zenu, wapeni shavu madingi na mamaza zenu...au sio machizi? akamaliza huyooooo!...akasepa! Toa maoni yako
 
Last edited:
Mbona unawapendelea vijana? Bible iliandikwa kwa ajili ya rika zote,na ole wake atayeongeza au kupunguza neno.Chunga sana.
 
Wameshapunguza sana, wameshaongeza mengi, na wanendelea kufanya hivyo. unajua kuna versions ngapi tofauti za bible?
 
Neno la Mungu limepimwa,na kuhakikiwa na Mungu mwenyewe,ole wake yule atakayebadilisha,au kuongeza hata nukta,hasira ya Bwana Mungu itawaka juu yake
 
Nakubali ziko versions nying za Bible zilizokwisha andikwa nyingine ni kwa matakwa binafsi.Lakini ole inabaki pale pale atakayeongeza/kupunguza Ufunuo wa Yohana 22:19.Mimi simo.
 
Kwani ndugu yangu unajua bible version ya kwanza iliandikwa kwa lugha gani? mbona nyie mmebadilisha kwenda kwenye kiingereza, kiswahili, kiarabu, kifaransa etc? halafu mbona tena ukiangalia misamiati iliyotumika inatofautiana kutoka version moja hadi nyingine? so unataka kuniambia wote watumiao new versions za bible watawakiwa na hasira ya bwana?

Na wewe je, unatumia version ipi, ya lugha gani (kama ni msomaji bible)?
 
Neno la Mungu limepimwa,na kuhakikiwa na Mungu mwenyewe,ole wake yule atakayebadilisha,au kuongeza hata nukta,hasira ya Bwana Mungu itawaka juu yake

Acha uwongo. yaani mungu alikuwa anasubiri watu waandikiane barua (waraka wa huyu kwenda kwa yule, kama ilivyo katika bibila) halafu yeye ahakiki na kuidhinisha kuwa hayo ni maneno yake. hocus pocus.
 
Nakubali ziko versions nying za Bible zilizokwisha andikwa nyingine ni kwa matakwa binafsi.Lakini ole inabaki pale pale atakayeongeza/kupunguza Ufunuo wa Yohana 22:19.Mimi simo.

ole huo ni kwa ajili ya kutishwa watu kama wewe wanaofuata nyayo za wasiyemjua.
 
Ukitaka kuona ole ni kwa ajili ya matisho ama vinginevyo ni sawa,ila ukweli unabaki kuwa ukweli Neno la Mungu limepimwa na Mungu mwenyewe.Swala la lugha ni lugha na si kubadili na Mungu mwenyewe ndio mwasisi wa lugha zote.
 
Ndugu yangu Rainbow napenda nikuhakikishie kuwa namwamini na namfwata Mungu ninayemjua na wala sibahatishi hata kidogo,nikutangazie tu kwamba mimi ni mkirsto tena Mkristo halisi na si wa mapokeo,
 
.
Inamaana ulikuwa pamoja na Yesu?
 
Sikuwa wala sijawahi kuwa pamoja na Yesu,ila pia kumjua na kumfwata Mungu hakutegemei kuwa na yesu,hata Yuda aliekuwa na yesu yalimshinda,swala la msingi ni uhusiano wako na Mungu,na ni swala la Imani
 
Acha uwongo. yaani mungu alikuwa anasubiri watu waandikiane barua (waraka wa huyu kwenda kwa yule, kama ilivyo katika bibila) halafu yeye ahakiki na kuidhinisha kuwa hayo ni maneno yake. hocus pocus.

Afadhali na akheri za barua za wanazuoni akina Paulo, kuliko utumbo unaokutikana ktk kitabu cha Mwamedi.
 
Kuwa na version ya lugha yeyote inakubalika kwa ajili ya usitawi wa jamii husika

It is a good idea, nakubaliana na wale wanaosema kuwa bible isibadilishwe, lakini inaonekana haijakatazwa kutafsiriwa katika lugha nyingine kama ilivyo katika kiswahili, kirundi, kiyoruba, kisukuma, kihaya, nk. Ni wakati mufaka pia kuiweka katika lugha nyingine nyepesi kwa watu wa kijiweni, neno litawafikia na kuwasaidia.
 
I got this as forwarded sms from ma friend!

Kutokana na ukweli kwamba vijana wengi hawapendi kusoma bible, umefika wakati bible ingetakiwa iandikwe upya kwa kiswahili cha kisasa zaidi (watumiacho vijana) ili iliwavutie vijana wengi zaidi waisome na wapate wokovu. Mfano bible ingekuwa na verse kama hizi;

Yesu akawaibukia masela wake na akawapa laivu, Oya washikaji mi ndo naenda kwa dingi, ila ndo hivo msikandamizane, msipige fix, msimind mademu wa washikaji zenu, wapeni shavu madingi na mamaza zenu...au sio machizi? akamaliza huyooooo!...akasepa! Toa maoni yako

Tusubiri Yesu aje tena kama alivyohaidi (lini/siku wala saa havijulikani). Ha..ha...habari ndio hiyo.
 
Back
Top Bottom