WILAYA YA TEMEKE YATENGEWA ZAIDI YA TSH BILIONI 4 KUTEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO,SHUKRANI KWA RAIS SAMIA - DC TMK MHE.JOKATE MWEGELO
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe.Jokate Mwegelo kwa niaba ya Uongozi wa Wilaya ya Temeke ametoa shukrani za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kuwapatia fedha Tsh Bilioni 4.491,851,456.06 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.
Mhe Jokate ameeleza namna ambavyo fedha hizo zimetengwa katika matumizi mbalimbali ya kuleta Maendeleo ambapo Takribani Tsh B 3.14 zitatumika katika ujenzi wa vyumba vya madarasa mapya 157 kwa shule za sekondari,Tsh M 250 kutumika katika ujenzi wa kituo cha afya Tuangoma,Tsh M 300 kutumika katika ujenzi wa Jengo la Huduma za dharura (EMD),Tsh M 700 kutumika katika ujenzi wa bweni la shule ya sekondari Kibasila pamoja na Tsh M 101,851,456.06 kutumika katika kampeni ya chanjo ya UVIKO-19 ikiwa ni ngao madhubuti dhidi ya uginjwa wa corona.
Aidha Mhe.Jokate ametoa shukrani kwa Rais Samia kwa kuwapatia magari 2 mapya kwa ajili ya kubebea wagonjwa (Ambulance) na usimamizi wa huduma za afya.
"Natoa shukrani kwa Mhe.Rais Samia kwakweli ni ukweli usiopingika Mwanamama huyu alishika nchi kipindi kigumu lakini ameonesha ukakamavu wa akina mama na ameweza kutuvusha salama na amefanya maamuzi mengi mengine magumu lakini ni kwaajili ya Taifa letu la Tanzania" Alisema Mhe.Jokate.
Mhe.Jokate ameyasema hayo leo Oktoba 13,2021 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Iddi Nyundo wakati akitambulisha rasmi ujio wa kampeni ya TEMEKE GULIO yenye lengo la kuwainua wafanyabiashara wadogo (wamachinga).
#KaziIendelee