Jokate Mwegelo zaidi ya unavyomfahamu

Michael Amon

JF-Expert Member
Dec 22, 2008
8,775
3,610
jk.jpg


WENGI ukiwauliza kuwa wanamfahamu vipi Kojate Mwegelo, jibu lao litakuwa ni Mshindi wa pili wa Miss Tanzania mwaka 2006.

Wengine watakuambia ni Miss Temeke mwaka 2006 na pia Balozi wa bia ya Redds wa mwaka huo huo. Kuna kundi la watu watakujibu kuwa ni mrembo aliyefanikiwa sana katika medani ya urembo.

Majibu yote hayo ni sahihi, hata hivyo kuna mengi ambayo wengi hawayafahamu kuhusu mrembo huyu.
Jokate ana vipaji lukuki, vipaji ambavyo anasema ndivyo vinavyomuweka mjini.

Tofauti na urembo, Jokate ana uwezo mkubwa katika uigizaji wa filamu, kipaji chake katika kuigiza kimeonekana katika filamu ya ‘Fake Pastors' ambayo alicheza kama mtoto wa mzee wa kanisa lakini hakuwa na maadili mazuri.

Mbali na kuwa na uwezo mkubwa katika kucheza filamu, Jokate pia ni Mwendesha shughuli mbali mbali, maarufu MC, kazi ambayo kwa mujibu wa mrembo huyu, inamsaidia kuongeza kipato chake.

Kwa kuonyesha kuwa ana vipaji vingi, mrembo huyo alishinda mchujo wa kuwania nafasi ya kuwa mtangazaji wa kituo maarufu cha televisheni cha Channel O cha Afrika Kusini mwaka jana.

Jokate anasema haikuwa kazi rahisi kwake kufanikisha mahojiano mbalimbali katika matamasha nchini humo ambapo alikuwa akihoji watu mbalimbali maarufu wakati wa ‘Red Carpet.'

"Niliweza kuwahoji zaidi ya wasanii 200 na mahojiano yote yalikuwa moja kwa moja , nilianza kwa kuogopa, lakini nilipiga moyo konde na kuendesha mahojiano hayo kwa ustadi mkubwa, najivunia kuwa Mtanzania wa kwanza kutangaza katika kituo hicho." anasema Jokate.

"Watanzania wengi wanajua kwa nini Afrika Kusini ipo juu kimuziki na hata katika fani nyingine mbali ya michezo, ni nchi ambayo ina watu maarufu wengi (celebrities), wote hawa kabla ya kuingia katika ukumbi, ilikuwa lazima wapitie kwangu na kuhojiwa, ilikuwa kazi kubwa ambayo imeweza kuniongezea uzoefu mkubwa katika fani ya utangazaji." anasema.

Anafafanua kuwa kwa sasa bado ni mtangaziji wa kituo hicho, ingawa hurekodi vipindi vingi kabla ya kurejea nyumbani kuendelea na shughuli zake nyingine.

Anasema kuwa utaratibu wa Channel O umemwezesha kuingia katika fani nyingine ya ubunifu wa mavazi ambapo kwa sasa ameibuka na staili mpya ijulikanayo kwa jina la Kidoti.

Maonesho ya mavazi
Jokate ameshiriki maonesho ya mavazi mawili makubwa mojawapo likiwa la Mitindo la Red Ribbon lililokuwa maalum kuchangisha fedha kwa ajili ya watoto waliothirika na ugonjwa wa Ukimwi chini ya Taasisi ya Tanzania Mitindo House (TMH) iliyochini ya mwenyekiti, Khadija Mwanamboka.

Katika maonyesho hayo, Jokate pia alikuwa mmoja wa wabunifu wa mavazi ya asili ya Kitanzania yaliyotumia malighafi za Khanga na Vitenge.

"Tunaweza kutumia malighafu za hapa hapa nyumbani kuvaa nguo nzuri, kinachotakiwa ni ubinifu tu, nina kipaji hicho na tayari wadau wameanza kunipongeza kwa kazi nzuri niliyofanya," anasema na kuongeza:

"Nimeona mwanga katika maonesho ya mitindo japo fani hii bado haijawa na muamko mkubwa, lakini nimeweza kufanya mambo makubwa kama haya."

Jokate anawashauri vijana kujishughulisha ili kupambana na hali ngumu ya maisha na kuachana na mambo ambayo yanawapotezea muda.
 
toka ahusishwe na skendo ya kumpora bwana malaya mwenzake wema sepetu- 'diamond' nimemshusha sana.namchukulia kama kahaba mwenye viwango kwa kila afanyalo,thenkyuu!
 
hongera sana jokate. ziba masikio usisikie la kusikia wakikusema ovyo wanakuongezea umaarufu, nani ambae ni msafi kati yenu na asimame amtupie jiwe yule ambae ni mchafu?? watu inabidi wajidhaminishe hata ufisadi ni dhambi kubwa sana na sio kwamba na mtetea ila hata kwa hapo alipofikia tumpongeze na masiyatizame ya zamani eti kafanya nini au vip, tugange yajayo, i wish jokate ningepata nafasi ya ku hug i real nakupenda sana ila sio kwa ngono, kwa maisha yako unayoyaweka sio kubwabwaja ovyo kama wengine wakina,,,,,,,, kimya kimya maisha yanasonga, wengine wakinunua chupi tu mlimani city tayari anataka kutolewa kwenye gazeti.
 
Pia ni mwanakwaya mzuri sana wa kanisani.. Ukitaka kuhakikisha fika pale St. Peters Oysterbay.

Aisee tedo itabidi nifike hayo maeneo nipate kujionea mwenyewe badala ya kuishi kusikia kwa watu.
 
Last edited by a moderator:
toka ahusishwe na skendo ya kumpora bwana malaya mwenzake wema sepetu- 'diamond' nimemshusha sana.namchukulia kama kahaba mwenye viwango kwa kila afanyalo,thenkyuu!

Kahaba tena...??? Duh!!! Mie ngoja ninyamaze.
 
Ana nyota ya kupendwa saana ila alipoingia masakata kugombania yule Diamond aahhh anatia hasira wengi wamemtoa dhamani
 
hongera jokate, you are a shining star, napendezwa sana na mafanikio yako! Mungu azidi kukubariki.
 
Kwa kujiinua kimaendeleo, namsifu though ni kicheche wa kimyakimya akichanganya na kuwa muabuduji mzuri na mwanakwaya kanisani, hapa ni kujaribu kulazimisha kuchanganya mafuta kwenye maji ili yasionekane, yataonekana tu, kidogokidogo watu wameshajua tabia zake zisizo nzuri, ila jamani Diamond naye, namkubali, anaimba vizuri but akicheza, ustaa, utamuua
Ana nyota ya kupendwa saana ila alipoingia masakata kugombania yule Diamond aahhh anatia hasira wengi wamemtoa dhamani
 
Back
Top Bottom