Jokate Mwegelo ametoa rai kwa Wananchi kuunga mkono juhudi za Serikali kwa kushiriki katika miradi ya maendeleo

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
666
835
WANANCHI WATAKIWA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA SERIKALI

Mkuu wa wilaya ya Temeke mheshimiwa Jokate Mwegelo ametoa rai kwa Wananchi kuunga mkono juhudi za Serikali kwa kushiriki katika miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwenye maeneo yao.

Mhe. Jokate ametoa rai hiyo leo Disemba 02,2021 alipotembelea kata ya Chamanzi kwa kwa lengo la kuamsha ari ya Wananchi wa kata hiyo kushiriki katika shughuli za maendeleo.

Katika ziara hiyo pia Mhe. Jokate amesisitiza juu ya suala la usafi, ambapo amesema kwamba wilaya ya Temeke itazindua siku ya usafi.

"Tarehe 4 tunafungua kampeni ya mkoa 'Safisha Pendezesha Dar es salam' sasa sisi tunasema 'Safisha Pendezesha Temeke', ilikuwa tuzindue usafi Nyerere road lakini tutazindua Kilwa road eneo la Mbagala Kiwilaya, na tunatarajia watu wote tukutane hapo kwa wingi tusafishe maduka yetu''.Alisisitiza Mhe. Jokate.

Aidha amewataka Wananchi kulipa tozo mbalimbali zilizowekwa ili wakandarasi waweze kulipwa.

Wakati huo huo Mhe. Jokate amefanya ukaguzi katika shule ya sekondari Chamanzi ambapo ujenzi wa vyumba vya madarasa 10 unaendelea.

Uhamasishaji Wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo zinazotekelezwa na Serikali, ni mojawapo ya shughuli za maadhimisho ya miaka 60 ya uhuru wa Tanganyika.Ziara ya leo ni muendelezo wa utekelezaji wa shughuli hizo.

@jokatemwegelo

#kaziiendelee🇹🇿

IMG-20211202-WA0373.jpg

IMG-20211202-WA0372.jpg

IMG-20211202-WA0370.jpg

IMG-20211202-WA0371.jpg

IMG-20211202-WA0374.jpg

IMG-20211202-WA0369.jpg
 
WANANCHI WATAKIWA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA SERIKALI

Mkuu wa wilaya ya Temeke mheshimiwa Jokate Mwegelo ametoa rai kwa Wananchi kuunga mkono juhudi za Serikali kwa kushiriki katika miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwenye maeneo yao...
😍
 
Back
Top Bottom