Nimekuwa nikisikia kuwa kuna joka lenye vichwa saba linapatikana duniani.Kuna bwana mmoja aliniambia joka hili huuwa linapita chini ya miamba ya milima kwa mwaka mara moja hata hapa Tanzania chini ya milima mikubwa.Wanasema watu wanaohitaji utajiri huwa wanatega visu kwenye njia linayopita ili kupata kipande cha gamba lake ambacho kinahusishwa na kupata utajiri. Naomba mwenye utaalamu au uelewa kuhusu hili joka atujuze tuweze kujua kuhusu hili joka