Elections 2010 Joka hili

Jibaba Bonge

JF-Expert Member
May 6, 2008
1,246
401
Umetimia wakati, joka kuliondosha
Tupaze zetu sauti, jitu hili kulifisha
Yake haki ni mauti, ulimwengu kuujulisha,
Oktoba imefika, joka hili liuliwe

Kazize kuchakachua , uchumi umetitia
Dhahabu limechukua, mafisadi kuwapatia
Mashimo kutuachia, eti uchumi umekua!
Oktoba imefika, joka hili liuliwe

Mali yote ya umma, lenyewe limekalia
Eti mali yake mama, wakati ya familia!,
Umma sasa kusimama ,mali ni kwa familia
Oktoba imefika, joka hili liuliwe

Kuliua tuwe makini, lisije kutukimbia
Kwanza taimu kichwani, halafu ndiyo mkia
Kura zetu kwa makini, na hilo ndiyo jambia
Oktoba imefika, joka hili liuliwe
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom