John tendwa nakubaliana na utafiti wako | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

John tendwa nakubaliana na utafiti wako

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Lu-ma-ga, Oct 5, 2010.

 1. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #1
  Oct 5, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,838
  Likes Received: 469
  Trophy Points: 180
  Nadiriki kuita ni utafiti kwa kuwa majibu yake yanaanza kuonyesha viashiria vya ukweli.

  Bwana tendwa alisema mapema kabla ya kambeni kuanza kuwa " Upinzani unatarajia kuzoa viti vya ubunge wa kuchaguliwa zaidi ya 100.Inavyoonyesha bwana Tendwa alilifanyia kazi kabla hajatamka.Japo alipata upinzani toka kwa Makamba wa SISIEMU.

  Kwa upande wao CHADEMA wameweka wagombea 187 nchi nzima , tathmini zao za mara kwa mara zinaashiria kupata viti karibu 150.

  Nakubaliana kuwa Tendwa alichobashiri (Hypothesis) kinaonyesha ni kweli hasa kutokana na majibu ya CHADEMA kuwa ndani ya ubashiri wa Tendwa(100+).

  Nimegundua kumbe tendwa ni makini katika mambo ya msingi lakini anajifanya ni KICHAA WA CCM

  Tafakari
   
 2. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #2
  Oct 5, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,767
  Likes Received: 216
  Trophy Points: 160
  Na comments zake kuhusu tamko la Askofu Kakobe nalo unaligoneleaje?
   
 3. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #3
  Oct 5, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,838
  Likes Received: 469
  Trophy Points: 180
  Hapo kafanya upuuzi lengo lake ilikuwa kuhalalisha uozo wa sheihk Yahaya. Ndiyo maana aliongelea kupitia Kakobe.Hapo hana credit ni mbofumbofuuuuuu
   
 4. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #4
  Oct 5, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Tendwa mnafiki maana aliweka sharti kuwa kama watatumia fursa zilizopo.
  Alafu ndio wale wale, hakutoa hata vigezo vya utafiti wake. Yeye ali generalize kwa kuangalia tu jinsi watu walivyoichoka sisi m, na kwa hiyo kama kada mzuri wa chama alikuwa anawapa red indicator ili wasipoteze majimbo yao, lakini si kwamba alisema akiwa na nia nzuri.

  Sasa tunaona ujinga wake kwa kupinga watu kupewa elimu ya uraia. Na jambo hili ndilo shida katika nchi hii. Yeye ameshindwa jukumu lake la kutoa elimu ya uraia sasa wanamsaidia wale walio na mafungamano na raia anakasirika na kufikiri kutunga sheria eti kuzuia viongozi wa dini wasiwambie kondoo wao elimu ya uraia. Huu utakuwa ni unafiki sana maana hakuna kiongozi wa kiserikali ambaye hatumii jukwaa la dini kuwafikia wananchi.

  Tumekuwa tukiona marais wakialikwa katika sherehe za kidini kama wageni waalikwa na kupewa jukwaa la kueleza mambo yao ya kisiasa na hakuna anayewakemea. Hapo ni sawa maana wanawafikia wananchi. Sasa wenye wananchi hao wamefikia zamu yao ya kuwasaidia kuwaelewa vizuri viongozi bora na haki zao za kiraia imekuwa nongwa kwa Tendwa.

  Mwaka huu Tendwa utapata wenda wazimu.
   
Loading...