John Tendwa na double standard: CCM kujivua Gamba "YES" lakini M4C ya CHADEMA ''NO" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

John Tendwa na double standard: CCM kujivua Gamba "YES" lakini M4C ya CHADEMA ''NO"

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by makoye2009, Sep 12, 2012.

 1. makoye2009

  makoye2009 JF-Expert Member

  #1
  Sep 12, 2012
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,646
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  Nimesikitishwa sana kama siyo kushangazwa na kauli ya Msajili wa vyama vya siasa Tanzania Bwana John Tendwa baada ya kutishia kukifutia usajili chama cha CHADEMA! TIshio hilo limekuja baada ya CDM kulaumiwa kuwa kimekuwa kinahusika na mauaji ya watu kwenye mikutano na maandamano yake yanayokwenda kwa kauli mbiu yake maarufu kama M4C(Movement for Change) ambayo yameendelea kuwavuta Watanzania wengi na kukijengea CDM umaarufu unaotishia uhai wa Chama Twawala CCM!

  Kauli ya John Tendwa inaonekana kuwa ni double standard. Hii yamkini siyo bahati mbaya ila inaonekana Tendwa anajua anachokifanya kwa maelekezo juu (ya Serikali na CCM).Kwamba CDM kitafutwa kama kitaendelea na KAULI MBIU yake ya M4C maana inasababisha vurugu na mauaji kwenye mikutano yake! Ni dhahiri kwamba kauli mbiu siyo katiba ya chama baali ni mkakati tu unaoanzishwa na chama husika kwa makusudio fulani. Kila Mtanzania anajua kwamba wakti CHADEMA wana M4C,chama Twawala CCM bado kinaendelea na kauli mbiu yake ya KUJIVUA GAMBA ingawa kauli mbiu hiyo imeshindwa kuleta matumaini au matarajio yaliyotegemewa na vigogo wa CCM!

  Viongozi wa CCM walizunguka nchi nzima kuinadi kauli mbiu hiyo kwa maandamano na mikutano ya ndani na nje lakini haikufua dafu mbele ya M4C. Matokeo hayo aidha yamewakatisha tamaa au kuwaudhi baadhi vigogo wa CCM na hivyo kuelekeza hasira na udhaifu wao kwa CDM. Kwa kulitumia Jeshi la Polisi,UWT na Msajili wa Vyama John Tendwa wameamua kuzuia M4C ya CDM kwa mtindo wa kuua watu na hatimaye ku-justfy kuwa M4C haifai kuendelea maana inachochea vurugu na mauaji.

  Watanzania wanauliza,''Why double standards?" Kwamba msajili huyo huyo anaruhusu kauli mbiu ya CCM ya Kujivua gamba ienezwe nchi nzima kwa maandamano na mikutano lakini kauli mbiu ya CHADEMA ya M4C inazuiliwa kwa kutishiwa chama kufutwa??!!! Hii ni ajabu na kweli!Juzi tu CUF nao wametangaza kauli mbiu yao inayosema" Mchakamchaka mpaka 2015" Je, hii nayo ataizuia Tendwa anatakiwa kujua kuwa yeye ni Msajili wa vyama vyote kwa hiyo asiwe biased kwa CCM tu simply because aliyemteua ni Rais ambaye ni Mwenyekiti wa CCM taifa. Huu ni ujinga ambao unatakiwa kukomeshwa mara moja.

  Nawasilisha.
   
 2. G

  Gongerfasil Member

  #2
  Sep 12, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 96
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 25
  Very good analysis lakini hawa watu aina ya akina tendwa nape mwigulu they just do it intentional hata waambiwe vp lakini they are ready to kill kutunza ukoloni wao
   
 3. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #3
  Sep 12, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,090
  Likes Received: 10,448
  Trophy Points: 280
  T2015CDM

  Hakuna huruma..
   
 4. zenmoster

  zenmoster JF-Expert Member

  #4
  Sep 12, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 953
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  hivi hiii post anapewa na nani?? hivi awezi achika?? maana jamaaa anajikuta anajua kila kitu...katiba mpya izungumzie post yake pia...asijikute anamamlaka ya kufanya maamuzi mwenyewe tu...he must b fair and nt otherwise.
   
 5. Takalani Sesame

  Takalani Sesame JF-Expert Member

  #5
  Sep 12, 2012
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 588
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Tendwa nae amegeuka na kuliangalia tumbo lake binafsi na kuacha kufanya kazi yake kwa mujibu wa sheria. Akili yote katia mfukoni!
   
 6. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #6
  Sep 12, 2012
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 8,999
  Likes Received: 582
  Trophy Points: 280
  mbona naskia huyo mzee sio ridhki??? sishangazwi na mambo anayofanya.
   
 7. Uhalisia Jr

  Uhalisia Jr Senior Member

  #7
  Sep 12, 2012
  Joined: Sep 10, 2012
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mahesabu yashamchanganya kuhusu katiba itamuachaje? au ndo NISTAAFU kwa raha.
   
 8. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #8
  Sep 12, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Mbona kujivua gamba na M4C mambo mawili tofauti inakuwaje una compare?
   
 9. m

  mjuaji Senior Member

  #9
  Sep 12, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 166
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  anaweza kuifuta chadema kama chama.ila hawezi kuifuta CHADEMa iliyoko moyoni mwetu.
   
 10. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #10
  Sep 12, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,840
  Likes Received: 470
  Trophy Points: 180
  Wazee serikali kwa sasa ni wa kuogopa hawajali tena miiko ya kazi wanataka kustaafu vizuri.pambafuuuuuuuuu haya mazee
   
 11. Mzalendo2015

  Mzalendo2015 JF-Expert Member

  #11
  Sep 12, 2012
  Joined: Aug 14, 2012
  Messages: 1,951
  Likes Received: 2,312
  Trophy Points: 280
  makoye2009,

  Good analysis. Mkuu umesema ukweli na ukweli mtupu. Tendwa anaonekana kutumiwa na CCM na Serikali yake kuihujumu CHADEMA. Hili liko wazi kabisa kwa mtu yeyote anayefuatilia upepo wa siasa za Tanzania kwa sasa.

  Kule Nyololo Polisi walimwua David Mwangosi kwa kisingizio cha kuzuia mikutano na maandamano ya vyama vya siasa. Lakini wakati huo huo CCM walikuwa wakiendelea na Mikutano ya chaguzi za Jumuia zake na Uchaguzi mdogo kule Bububu-Zanzibar. CCM waliendelea na shughuli zao za kisiasa bila ya bugudha yoyote ya Jesshi la polisi nchi nzima. Hapa ndipo unaweza kuona ujinga wa CCM na serikali yake. Kwamba maandamano ya CCM na mikutano yake ya ndani na hadhara ruksa lakini CDM marufuku. Yaleyale ya double standards!!!

  Kweli CCM wamezidiwa na CDM kwa kila mbinu sasa wameamua kucheza rafu na kupiga mipira nje ilmradi mchezo umalizike! Ndicho wanachofanya CCM kwa sasa! Naona mpaka kufikia 2015 tutashuhudia vioja na vifo vingi kama Kikweta hatachukua hatua za maksudi za kukinusuru chama chake. Tatizo la huyu jamaa kaamua kuwaachia chama kina Nape na Mchumba Mwigulu wanaotumiwa na mafisadi na makundi ndani ya CCM kuhujumiana na kumhujuma Kikwete. Mbona kazi ipo!
   
Loading...