John Stephen Akhwari; Mtanzania maarufu ulimwenguni kuliko hapa Bongo

chifu77

JF-Expert Member
Aug 2, 2014
902
595
Heshima kwenu wakuu.

John Steven Akhwari ni mwanariadha mstaafu. Alizaliwa mwaka 1938 kule Mbulu- Mkoani Manyara. Aliiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Olimpic mwaka 1968 nchini Mexico, katika mashindano ya riadha ya kilomita 42. Washiriki walikuwa 75, lakini waliomaliza shindano ni 57 pekee, huku John Steven Akhwari akimaliza wa mwisho kabisa.

Kwa nini alimaliza wa mwisho? Baada ya mbio kuanza, walipofika kilomita ya 19, mshiriki mojawapo alimparamia, kumsukuma na kuanguka vibaya mno. Aliumia begani, na goti la mguu wa kulia lilitenguka. Gari la huduma ya kwanza lilimfikia na kumpa matibabu, akaweza kusimama tena na kuendelea na riadha.

Umaarufu wake duniani. Watu waliomhudumia walimlazimisha kuaihirisha shindano na apande kwenye gari lakini alikataa katakata. Aliendelea na riadha huku akichechemea. Alifanikiwa kumaliza kilomita zote 42, jioni ya saa 1 kwa saa za Mexico. Watu wachache waliokuwa wamebakia uwanjani walimshangilia sana.

Mwishoni kabisa, waandishi wa habari walimuuliza, Kwa nini aliendela kukimbia ili hali ameumia kiasi hicho? Aliwaambia Nchi yangu Tanzania haikunituma maili 5000 kuja Mexico kuanza hili shindano bali walinituma kumaliza shindano.

Katika mashindano ya Olimpic na mpaka hivi leo Bwana John Stephen Akhwari anatambulika kama 'The Greatest Last- Place Finish Ever'. Japo hakushinda tuzo yoyote lakini ameonyesha uvumilivu, ujasiri na wenzetu wamekuwa wakimtumia kufundishia watoto na vijana wao kwamba they must struggle to finish the race, not just to start it.

Kwa bahati mbaya sana, watanzania walio wengi hawamjui. Huyu ni mfano wa kuigwa, ilistahili kauli yake hiyo ingekuwa nukuu muhimu kwa vijana wetu.

John Stephen Akhwari - Inspirational Story - Athslife

John Stephen Akhwari - Wikipedia
 
Attachments

  • Story of John Steven Akhwari of Tanzania.mp4
    11.7 MB · Views: 65
  • Story of John Steven Akhwari of Tanzania2.mp4
    2.8 MB · Views: 57
  • BBC Olympian John Stephen Akhwari.3gp
    4 MB · Views: 44
mie mara ya kwanza kumsikia nilikuwa natazama kipindi fulani tbc kinarushwa na vijana wa arusha, then nkamsikia dr mmoja ghana anasimulia kuhusu story yake ya kumaliza mashindano. Hongera kwake kwa kutoa somo
 
Ahsante sana kwa taarifa, nakiri ni kweli simjui kama wapo na wengine endelea kutujuza mkuu
Nalog off
 
mie mara ya kwanza kumsikia nilikuwa natazama kipindi fulani tbc kinarushwa na vijana wa arusha, then nkamsikia dr mmoja ghana anasimulia kuhusu story yake ya kumaliza mashindano. Hongera kwake kwa kutoa somo
Mimi mara ya kwanza nilimsikia mhubiri mmoja wa marekani akitumia hii story kufundisha watu kanisani kwake. Nikalazimika kuanza kusearch youtube, na kwingineko. Mhubiri aliwaambia waumini wake kuwa Imani ni sawa na story ya Huyu bwana.
 
Katika mashindano ya Olimpic na mpaka hivi leo Bwana John Stephen Akhwari anatambulika kama 'The Greatest Last- Place Finish Ever'. Japo hakushinda tuzo yoyote lakini ameonyesha uvumilivu, ujasiri na wenzetu wamekuwa wakimtumia kufundishia watoto na vijana wao kwamba they must struggle to finish the race, not just to start it.
Hakikia, Inatia moyo sana.
 
Heshima kwenu wakuu.

John Steven Akhwari ni mwanariadha mstaafu. Alizaliwa mwaka 1938 kule Mbulu- Mkoani Manyara. Aliiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Olimpic mwaka 1968 nchini Mexico, katika mashindano ya riadha ya kilomita 42. Washiriki walikuwa 75, lakini waliomaliza shindano ni 57 pekee, huku John Steven Akhwari akimaliza wa mwisho kabisa.

Kwa nini alimaliza wa mwisho? Baada ya mbio kuanza, walipofika kilomita ya 19, mshiriki mojawapo alimparamia, kumsukuma na kuanguka vibaya mno. Aliumia begani, na goti la mguu wa kulia lilitenguka. Gari la huduma ya kwanza lilimfikia na kumpa matibabu, akaweza kusimama tena na kuendelea na riadha.

Umaarufu wake duniani. Watu waliomhudumia walimlazimisha kuaihirisha shindano na apande kwenye gari lakini alikataa katakata. Aliendelea na riadha huku akichechemea. Alifanikiwa kumaliza kilomita zote 42, jioni ya saa 1 kwa saa za Mexico. Watu wachache waliokuwa wamebakia uwanjani walimshangilia sana.

Mwishoni kabisa, waandishi wa habari walimuuliza, Kwa nini aliendela kukimbia ili hali ameumia kiasi hicho? Aliwaambia Nchi yangu Tanzania haikunituma maili 5000 kuja Mexico kuanza hili shindano bali walinituma kumaliza shindano.

Katika mashindano ya Olimpic na mpaka hivi leo Bwana John Stephen Akhwari anatambulika kama 'The Greatest Last- Place Finish Ever'. Japo hakushinda tuzo yoyote lakini ameonyesha uvumilivu, ujasiri na wenzetu wamekuwa wakimtumia kufundishia watoto na vijana wao kwamba they must struggle to finish the race, not just to start it.

Kwa bahati mbaya sana, watanzania walio wengi hawamjui. Huyu ni mfano wa kuigwa, ilistahili kauli yake hiyo ingekuwa nukuu muhimu kwa vijana wetu.

John Stephen Akhwari - Inspirational Story - Athslife

John Stephen Akhwari - Wikipedia
He real was great
 
Back
Top Bottom