Ndekirhepva
JF-Expert Member
- May 18, 2012
- 371
- 44
MBUNGE wa Maswa Mashariki (Chadema), John Shibuda jana alirudia kauli yake ya kumuomba Rais Jakaya Kikwete awe meneja wake wa kampeni wakati atakapojitosa kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.Shibuda alifanya hivyo mbele ya wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Spika wa Bunge, Anne Makinda na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samwel Sitta.
Kauli hiyo imekuja wakati Shibuda akiwa ameiligawa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha) baada ya mwenyekiti wake, John Heche kupingana hadharani na makamu wake, Juliana Shonza kuhusu msimamo wa baraza hilo dhidi ya hatua ya mbunge huyo kutangaza nia ya kuwania urais, akiwa ndani ya kikao cha Nec ya CCM.
Siku mbili baadaye Shibuda aliibuka tena na kumshukia Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa, kuwa ndiye anayewatumia vijana hao kumhujumu, kauli ambayo ilipingwa vikali na Dk Slaa.
Lakini, jana akiwa katika semina ya wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki iliyowahusisha pia wenyeviti wa kamati zote za kudumu za Bunge wakiwemo wa Kamati ya Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama, Shibuda alirudia kauli yake na kuwafanya washiriki wa semina hiyo kuangua kicheko.
Mimi naitwa John Shibuda ni Mbunge wa Maswa Mashariki na Mjumbe wa Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, pia ninayetaka Rais Kikwete awe kampeni meneja wangu katika kampeni za mwaka 2015, alisema wakati akijitambulisha.
Kauli hiyo ilizua zogo kwa baadhi ya washiriki wa semina hiyo ambao walianza kumpigia makofi huku Spika Makinda na Sitta wakiangua kicheko.
hili li ndumi la kuwili sijui limetutokea wapi jamani, yani bichwa kuuuuuuubwa akili nusu kijiko, au tumfungulie page kwenye fesi buku kama ile ya diva?????