John Shibuda na mgogoro wa Kauli ya kuisifia CCM; Kauli za wana CHADEMA

na aende zake asirudi sana, nachukia sana binadamu anayependa kunyenyekewa , hakuna haja ya kubembeleza hapa, chapa lapa..kuna watu kibvao wenye uwezo wa kuwa viongozi bora tena mara mia zaidi yake ..
 
BAVICHA msipoteze hii nafasi adimu. Mtangazeni Shibuda enemy of M4C.

Anasema yeye ni mjumbe wa APRM? Kwa hiyo anataka watu waamini APRM ndio wamemtuma aende kwenye NEC ya CCM na kusema chama chenye uwezo wa kuongoza Tanzania ni CCM? Mbona naona kama anataka kuichafua APRM?

Malizeni hii shughuli.enemy of M4C.
 
CDM na BAVICHA vilikuwepo kabla ya huyo mpuuzi Shibuda.... Hakuna kumuomba rdhi kwan yeye atapita lakini CDM na BAVICHA vitabaki!!
 
Bavicha waliyataka wenyewe ..wangenyamaza wangefukuzwa kazi? ..mimi nawalaumu bavicha na nitaendelea kuwalaumu ..mngenyamaza watu hata wasingejua ila haya malumbano wala yasingepata coverage

Saint Ivuga,

Sema ukweli tu bila unafiki kwamba wa kulaumiwa hapa ni Shibuda wala siyo BAVICHA! Haiwezekani Mbunge wa CHADEMA akakae kwenye mkutano wa CCM-NEC na aombe kugombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA lakini M/Kiti Taifa CCM ambaye ni Kiwete ndo awe Manager wake wa kampeni . Twende mbele turudi nyuma. Je, kama angelikuwa ni Mbunge wa CCM ameenda kwenye mkutano wa NEC au CC ya CHADEMA halafu akaomba kugombe Urais kwa tiketi ya CCM lakini Mwenyekiti wa CDM mhe. Mbowe ndiyo awe Campaign Manager wake, hivi ungetegemea CCM na UVCCM wangemshangilia huyo Mbunge na kumpongeza kweli???

Jibu ni HAKUNA KITU KAMA HICHO. Kwa hiyo tusidanganyane. Shibuda amenyea kambi he must go at any cost. CCM wenyewe walimpiga chini mwaka 2010 kwenye mchakato wa kura za maoni kwa ujinga wake huu huu wa kuropoka. Kila mtu anakumbuka huyu kihiyo Shibuda aliwahi kutangaza kugombea Urais kwa tiketi ya CCM lakini jina lake likatupwa!!!Hana sifa hata ya kuwa Balozi wa nyumba kumi. He is just a hooligan. Pambaf zake!
 
Mbunge wa maswa mashariki (Chadema) Mh. Magale Shibuda amewapa siku 3 bavicha
wamutake radhi yeye na wapiga
kura wake kuhusu kutoa kauli
kwenye NEC ya ccm kugombea
urais anasema wana fikra hasi na
kusahau kuwa yeye ni mjumbe
wa APRM mpango wa
kujitathimini africa kwa hiyo
alikuwa anatoa mada kwenye NEC.

Bavicha wanajua cha kufanya kwa mtu kama chibuda!
 
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO- CHADEMA-
MKOA WA SINGIDA​

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

TAMKO LA BARAZA LA VIJANA CHADEMA MKOA WA SINGIDA.

Taarifa kwa Vyombo vya habari na Umma wa watanzania.
Waheshimiwa waandishi wa habari, na watanzania wote kwa ujuma.
Tumewaiteni hapa leo mchana, kuunga mkono kauli ya Mwenyekiti wetu wa Baraza la vijana wa CHADEMA- Taifa.
Watanzania wamehangaika miaka mingi, wanajua shida walizopata, wanajua jinsi Chama cha Mapinduzi ambavyo hakikuwasaidia, wananchi wamebaki katika maisha magumu siku zote, shida mbalimbali, zikiwemo manyanyaso yanayotokana na serikali ya chama cha mapinduzi. Tunasisitiza kuwa ni kweli mabadiliko yanahitajika kwa sasa, watanzania wanahitaji mabadiliko na mabadiliko ni lazima.
Kama alivyosema Baba wa Taifa, Tumeonewa kiasi cha kutosha; tumenyonywa kiasi cha kutosha; tumenyanyaswa (tumetumikishwa) kiasi cha kutosha; na tumepuuzwa kiasi cha kutosha. Ni unyonge wetu uliotufanya tuonewe, tunyonywe, tunyanyaswe na tupuuzwe. Sasa tunataka mapinduzi ili tusionewe, tusinyanyaswe na tusipuuzwe tena. Huo ndio unapaswa kuwa msimamo wa watanzania wanaotaka mabadiliko ya sasa ambayo kweli tutake tusitake tunayahitaji kwa nguvu zote.
Hivyo Baraza la vijana Mkoa wa Singida, kama ilivyo kwa Baraza la vijana kitaifa ni kuwa hatuko tayari kuvumilia Kiongozi yeyote wa CHADEMA, au Mbunge yeyote wa CHADEMA anayesaliti harakati za mapambano kuelekea mabadiliko na Uhuru wa kweli unaohitajika kwa watanzania, na kwa manufaa ya watanzania. Nasisitiza kuwa Vijana wa CHADEMA, Tuseme ukweli ili Taifa la Tanzania linufaike liendelee kudumu. Wabunge wanaoona kuwa CHADEMA, ambacho ndicho chama pekee cha Upinzani nchini hakifai, na ambao wapo CHADEMA waende kule wanapona kunafaa tena haraka, kuliko kudhalilishana kwa misingi isiyo kidhi haja za kisiasa, kielimu wala hazina mantiki zinapotafakariwa na watu wenye akili timamu. BAVICHA tunasisitiza kuwa wabunge wa CHADEMA ambao wanashiriki vikao au kuomba makada wa CCM kuwasaidia kufanya mabadiliko, hasa viongozi wa CCM walioifisadi nchi yetu, wabunge hao ni wasaliti, na iwe mchana, gizani, au usiku. Chini, pembeni, juu au kando kando HATUWAUNGI MKONO, na hawafai kwa safari yetu ya mabadiliko. Shibuda ametudhalilisha kama Chama, kwenda kutangaza nia ya kugombea Urais kwenye Kikao cha CCM, na kumwomba Kikwete ambaye Chama chetu kwa niaba ya watanzania kinamtuhumu kwa ufisadi kuwa Meneja wa Kamepni, Hivyo tunasisitiza kuwa tunaunga mkono tamko la BAVICHA TAIFA.Ikiwezekana achukuliwe hatua za kinidhamu ndani ya CHAMA

Josephat Isango
MWENYEKITI-BAVICHA MKOA
SINGIDA.
 
Bavicha walikurupuka sasa things are coming back...shibuda achezewi yule ulizia yahaya yuko wapi asa hivi baada ya kumtabiria mzee wa mkoa mpya kifo
 
hii ni mara ya pili naona jinsi shibuda huyu anavyowapa shida hivi ni kwanini hamumuwajibishi mkiwa kama mfano wa chama kinachopenda kushinikiza chama tawala kuwawajibisha viongozi wake nimeanza kupata picha flani 2015.
 
Huyu shibuda sijui chadema wanasubiri nini. wamfukuzie mbali.
 
Jina lako limenifanya nisiandike nilichokuwa nataka kuandika. Uliripoti vizuri kesi ya Mh Tundu A Lisu
 
Back
Top Bottom