John Shibuda na Dhana yake ya Ukabila (Makala, Mwananchi Jumapili) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

John Shibuda na Dhana yake ya Ukabila (Makala, Mwananchi Jumapili)

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by maggid, May 27, 2012.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  May 27, 2012
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Ndugu zangu,

  Kuna wakati nilitua uwanja wa ndege wa Nairobi na kupanda teksi. Nilishangaa sana pale dereva wa teksi alipojitambulisha kwangu kwa kutamka; " I am Peter, and a Kikuyu"

  Kwamba anaitwa Peter na kabila lake ni Mkikuyu. Kwa mimi Mtanzania hilo lilikuwa jambo la ajabu sana. Sijapata kujitambulisha kwa jina na kabila langu katika maisha yangu yote. Si kawaida yetu Watanzania.

  Katika nchi za wenzetu kuna tatizo la ukabila. Watanzania tuna bahati kubwa; hatuna ukabila. Labda ukabila wetu upo kwenye lugha ya Kiswahili. Udugu wetu Watanzania umejenga sana kwenye lugha ya Kiswahili. Anayezungumza lugha ya Kiswahili ni mwenzako huyo, huulizi tena kabila lake.

  Ndio, Watanzania hatuna ukabila wala udini. Wenye kutaka kupandikiza mbegu za chuki za ukabila na udini miongoni mwetu ni wachache sana, na hususan wanasiasa kwa malengo ya kisiasa. Tuwe makini sana.

  Ona majuzi hapa, Mtanzania mwenzetu John Shibuda ameibua hoja ya ukabila. Nakubaliana na Shibuda kwenye hoja ya kutaka haki yake ya kutangaza nia ya kuwania Urais wa nchi hii iheshimiwe.

  Shibuda ana haki hiyo. Na haitakuwa mara ya kwanza kwake kututangazia Watanzania nia yake hiyo.

  Lakini, inasikitisha, kuwa hoja ya pili ya Shibuda imechangia kuua hoja yake ya kwanza; ni hoja ya ukabila.

  Shibuda anaonekana kututaka Watanzania tujadili ukabila na hususan chama chake cha Chadema na ukabila ulio ndani ya chama hicho.

  Shibuda ni mmoja wa viongozi ninaowaheshimu sana kwa mchango wao kwa taifa letu. Naamini, kuwa Shibuda anaheshimika na wengi wengine hapa nchini. Lakini, kwa kutuletea Watanzania hoja ya Chadema na ukabila, nahofia Shibuda amepotea.

  Maana, hoja yake haina msingi. Imejengeka katika hisia kuliko uhalisia. Yumkini, Shibuda amekuja na hoja hii sasa, ama , kwa bahati mbaya, au kukusudia. Hilo la mwisho halina kusudi la kujenga, bali kubomoa. Inasikitisha.

  Maana, hoja ya ukabila haina umaarufu katika nchi yetu kwa sasa. Watanzania wa sasa hatuendekezi ukabila. Kauli ya

  Shibuda kuwa anabaguliwa katika chama chake cha Chadema kwa vile ni Msukuma haikupaswa kutamkwa kwa mtu kama Shibuda na haikupaswa kutamkwa na yeye na bado akaendelea kubaki katika chama anachoamini kina ubaguzi wa kikabila na huku mwenyewe akiwa mwathirika wa ubaguzi huo.

  Na kwa vile hana ushahidi wowote wa kuthibitisha anachosema, Shibuda anachochea moto ambao Watanzania hatuutaki. Ukabila ni moto wa hatari, kama ilivyo kwa moto wa udini.

  Kama Shibuda analalamika kuwa anabaguliwa kwa vile ni Msukuma, ingekuwaje basi, John Shibuda angeitwa Ramadhan Shibuda? Je, angeongeza dai la pili; kuwa anabaguliwa Chadema kwa vile ni Muislamu. Si Mkatoliki?

  Kama Shibuda anadhani kauli zake za ukabila zinakisaidia chama chake cha zamani cha CCM, basi, napo anakosea; maana, kwa CCM kuhusishwa sasa na kauli za Shibuda za ukabila, kunakiharibia zaidi kuliko kukijenga kwa Watanzania walio wengi. Lililo bora kwa CCM sasa ni kujitenga na kauli za Shibuda juu ya ukabila.

  Maana, Watanzania wa leo si wa jana. Ni wepesi sasa wa kubaini hila na ghilba za wanasiasa. Wengi wanaonekana kusikitishwa na hoja ya Shibuda juu ya kubaguliwa kwa vile ni Msukuma. Wanasikitika kwa vile wanadhani hoja imejengeka katika hila na ghilba kwa wananchi.

  Shibuda afahamu ukweli huu; Watanzania walio wengi kwa sasa wanataka mabadiliko. Wanaiona sasa mishale ya saa ya mabadiliko ikisonga mbele. Wanamwona hata Rais wao, Jakaya Kikwete akisaidia kusukuma mabadiliko hayo.Ni mabadiliko ya kimfumo.

  Hivi, ni Watanzania wangapi walifahamu kuhusu uwepo wa CAG miaka mitatu iliyopita? Hakika, upinzani bungeni, ndani ya chama tawala, na uwepo wa ofisi ya CAG iliyopewa nguvu umeanza kurudisha matumaini ya Watanzania. Uwepo wa uwajibikaji wa viongozi.

  Naam, Watanzania hawataki tena kurudi katika mfumo wa chama kimoja kilichoshika hatamu. Majaribio yote ya kuua upinzani, kufuta fikra huru, yatazidi kulaaniwa na walio wengi katika nchi hii.

  Hivyo, Shibuda hawezi tena leo kurudisha nyuma mshale wa saa ya mabadiliko; hata kwa ajenda ya ukabila. Nahitimisha.

  Maggid Mjengwa,
  Iringa
  0788 111 765
  Mjengwa Blog::Habari,Picha,Matangazo
   
 2. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #2
  May 27, 2012
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,003
  Likes Received: 325
  Trophy Points: 180
  Napata taabu sana kuelewa Shibuda anatumiwa na nini, mąna sidhani kwa akili yua kawaida hata ĆCM wanaweza kumyumia mtu kama huyu.
   
 3. only83

  only83 JF-Expert Member

  #3
  May 27, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Uzee ni dawa, ila kwa Shibuda uzee ni ugonjwa.
   
 4. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #4
  May 27, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Nenda ofisi za chadema ndio utamuelewa shibuda anasema nini. 90% (plus or minus 10%) wachagga! Jee, hiyo ni "coincidence"?

  Ukitoka huko katazame wabunge wa upendeleo, ukisha waona tueleze asilimia ngapi ni wa wapi.

  Ukimaliza hapo, katazame na vyama vingine uone uwiano unalingana? Ukimaliza, usilete jibu hapa iwe siri yako!
   
 5. Higash

  Higash JF-Expert Member

  #5
  May 27, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 844
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 45
  umepiga mswaki leo?
   
 6. B

  Benaire JF-Expert Member

  #6
  May 27, 2012
  Joined: Dec 13, 2011
  Messages: 1,947
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Mlianza na CUF,wenye upeo mdogo wakawasadiki....Sasa mmehamia CHADEMA,wenye upeo mkubwa tumewastukia.
  Home work.
  Fanya utafiti kwa kuangalia wanachama wa TANU hapo mwanzoni kabisa...kwa kuangalia dini na ukanda wa wanachama wake kisha huo ukabila wako.
  Mwisho
  Kinachotuunganisha ni utanzania wetu na kiswahili chetu tu,ndio maana tunaishi popote Tanzania bila kubaguana.
   
 7. Comi

  Comi JF-Expert Member

  #7
  May 27, 2012
  Joined: Oct 2, 2011
  Messages: 3,347
  Likes Received: 478
  Trophy Points: 180
  fikiria mara mbili,je mikoa mingine ina mwamko wa mabadiliko?wachaga ni wangapi?je slaa,wenje,nyerere,mdee,mbilinyi,mchungaji,nasari,kabwe,lwakatare ni wachaga? Nyie endeleeni kugema minazi na kucheza bao mtegemee mabadiliko ya haraka.

  Mpende msipende,mtake msitake tutawakomboa na nyie mamwinyi kwani tunawapenda muishi katika nchi yetu tuipendayo ya tanzania, zidumu nguvu,fikra,utashi na uzalendo wa tanzania
   
 8. Maarko

  Maarko JF-Expert Member

  #8
  May 27, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,030
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Acha kupotosha Umma,toa takwimu tukuelewe acha kuongelea hisia zako,hakuna ukweli katika yote unayosema,jenga hoja kwa vielelzo.
   
 9. Comi

  Comi JF-Expert Member

  #9
  May 27, 2012
  Joined: Oct 2, 2011
  Messages: 3,347
  Likes Received: 478
  Trophy Points: 180
  mfa maji haachi kutapatapa, shibuda simtofautishi na yule mkuu wa wilaya ayetoa barua ya kujiuzulu baada ya kujua hatima ya uongozi inaisha sasa anatafuta ni jinsi gani ya kujisafisha, watu ambao ni wabinafsi utawajua kwa maneno,matendo n.k
  je hadi leo shibuda amewasaidia kwa kiasi gani wananchi wa jimbo lake? Huwezi kumsaidia mtoto wa jirani chakula ilhali mwanao anakufa njaa. Unataka kuwa rais je jimbo lako umeliletea maendeleo gani?
   
 10. Mtoto Wa Mbale

  Mtoto Wa Mbale JF-Expert Member

  #10
  May 27, 2012
  Joined: May 15, 2011
  Messages: 458
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Sina hakika kama huu ndo uelewa wako halisi au kuna anayekusaidia kufikiri. Sina haja ya kukueleza kwa kirefu sana, lakini naomba tuwapongeze wachaga kwa kuzaliana kwa wingi katika mikoa ya Rukwa, Mbeya, Iringa, Shinyanga, Mwanza, Arusha, Kagera, Mara, Ruvuma, Singida, Dodoma, Morogoro, nk. Kwani wote walio katika mikoa hiyo na wanaopenda mabadiliko ni wachaga.
   
 11. M

  Maskini Mkulima Member

  #11
  May 27, 2012
  Joined: Dec 27, 2011
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Natazama huu mchanganuo halafu utuonyeshe asilimia 90 ya wachaga iko wapi:

  ORODHA YA VIONGOZI MAKAO MAKUU YA CHADEMA:
  VIONGOZI WAKUU WA KITAIFA:
  [TABLE="class: MsoTableGrid"]
  [TR]
  [TD] S/N[/TD]
  [TD] JINA LA KIONGOZI[/TD]
  [TD="width: 222"] WADHIFA[/TD]
  [TD="width: 84"] KABILA[/TD]
  [TD="width: 127"] ANAKOTOKA[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 37"] 1.[/TD]
  [TD="width: 168"] Freeman Aikael Mbowe[/TD]
  [TD="width: 222"] Mwenyekiti Taifa[/TD]
  [TD="width: 84"] Mchaga[/TD]
  [TD="width: 127"] Hai - Kilimanjaro[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 37"] 2.[/TD]
  [TD="width: 168"] Said Arfi[/TD]
  [TD="width: 222"] Makamu Mwenyekiti (T) Bara[/TD]
  [TD="width: 84"] Mfipa[/TD]
  [TD="width: 127"] Mpanda - Rukwa[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 37"] 3.[/TD]
  [TD="width: 168"] Issa Said Mohamed[/TD]
  [TD="width: 222"] Makamu Mwenyekiti (T) Visiwani[/TD]
  [TD="width: 84"] Mpemba[/TD]
  [TD="width: 127"] Pemba - Zanzibar[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 37"] 4.[/TD]
  [TD="width: 168"] Willibrod Peter Slaa[/TD]
  [TD="width: 222"] Katibu mkuu Taifa[/TD]
  [TD="width: 84"] Muirak[/TD]
  [TD="width: 127"] Karatu - Arusha[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 37"] 5.[/TD]
  [TD="width: 168"] Zitto Zuberi Kabwe[/TD]
  [TD="width: 222"] Naibu Katibu Mkuu (T) Bara[/TD]
  [TD="width: 84"] Muha[/TD]
  [TD="width: 127"] Kigoma Ujiji - Kigoma[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 37"] 6.[/TD]
  [TD="width: 168"] Hamad Mussa Yusuph[/TD]
  [TD="width: 222"] Naibu Katibu MKuu (T) Visiwani[/TD]
  [TD="width: 84"] Mpemba[/TD]
  [TD="width: 127"] Pemba - Zanzibar[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 37"] 7.[/TD]
  [TD="width: 168"] John Heche[/TD]
  [TD="width: 222"] Mwenyekiti BAVICHA Taifa[/TD]
  [TD="width: 84"] Mkurya[/TD]
  [TD="width: 127"] Tarime – Mara[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 37"] 8.[/TD]
  [TD="width: 168"] Sharifa Suleiman[/TD]
  [TD="width: 222"] Makamu Mkt BAVICHA – Visiwani[/TD]
  [TD="width: 84"] Mzanzibari[/TD]
  [TD="width: 127"] Unguja – Zanzibar[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 37"] 9.[/TD]
  [TD="width: 168"] Juliana Shonza[/TD]
  [TD="width: 222"] Makamu Mkt BAVICHA – Bara[/TD]
  [TD="width: 84"][/TD]
  [TD="width: 127"] Mbeya[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 37"] 10.[/TD]
  [TD="width: 168"] Suzan Lyimo[/TD]
  [TD="width: 222"] Kaimu Mwenyekiti BAWACHA (T)[/TD]
  [TD="width: 84"] Mchaga[/TD]
  [TD="width: 127"] Moshi – Kilimanjar[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 37"] 11.[/TD]
  [TD="width: 168"] Nyangaki Shilungushela[/TD]
  [TD="width: 222"] Mwenyekiti WAZEE Taifa[/TD]
  [TD="width: 84"] Msukuma[/TD]
  [TD="width: 127"] Shinyanga[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  WAKURUGENZI WA KURUGENZI ZA CHAMA MAKAO MAKUU YA CHAMA WANAOMSAIDIA KATIBU MKUU:
  [TABLE="class: MsoTableGrid"]
  [TR]
  [TD] S/N[/TD]
  [TD] JINA LA MKURUGENZI[/TD]
  [TD="width: 228"] KURUGENZI ANAYOONGOZA[/TD]
  [TD="width: 88"] KABILA[/TD]
  [TD="width: 135"] ANAKOTOKA[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 37"] 12[/TD]
  [TD="width: 150"] Anthony Komu[/TD]
  [TD="width: 228"] Fedha na Utawala[/TD]
  [TD="width: 88"] Mchaga[/TD]
  [TD="width: 135"] Moshi vijijini - Kilimanjaro[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 37"] 13[/TD]
  [TD="width: 150"] Benson Kigaila[/TD]
  [TD="width: 228"] Organisation na Mafunzo[/TD]
  [TD="width: 88"] Mgogo[/TD]
  [TD="width: 135"] Kibakwe - Dodoma[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 37"] 14[/TD]
  [TD="width: 150"] Msafiri Mtemelwa[/TD]
  [TD="width: 228"] Kampeni na Uchaguzi[/TD]
  [TD="width: 88"] Mzaramo[/TD]
  [TD="width: 135"] Mkuranga - Pwani[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 37"] 15[/TD]
  [TD="width: 150"] John Mrema[/TD]
  [TD="width: 228"] Bunge na Halmashauri[/TD]
  [TD="width: 88"] mchaga[/TD]
  [TD="width: 135"] Vunjo - Kilimanjaro[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 37"] 16[/TD]
  [TD="width: 150"] Ezekiah Wenje[/TD]
  [TD="width: 228"] Mambo ya Nje[/TD]
  [TD="width: 88"] Mjaluo[/TD]
  [TD="width: 135"] Tarime - Mara[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 37"] 17[/TD]
  [TD="width: 150"] John Mnyika[/TD]
  [TD="width: 228"] Habari na Uenezi[/TD]
  [TD="width: 88"] Msukuma[/TD]
  [TD="width: 135"] Misungwi - Mwanza[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 37"] 18[/TD]
  [TD="width: 150"] Tundu Lissu[/TD]
  [TD="width: 228"] Sheria na Haki za Binadamu[/TD]
  [TD="width: 88"] Mnyanturu[/TD]
  [TD="width: 135"] Ikungi - Singida[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 37"] 19[/TD]
  [TD="width: 150"] Wilfred Lwakatare[/TD]
  [TD="width: 228"] Ulinzi na Usalama[/TD]
  [TD="width: 88"] Mhaya[/TD]
  [TD="width: 135"] Bukoba - Kagera[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 37"] 20[/TD]
  [TD="width: 150"] Deogratias Munisi[/TD]
  [TD="width: 228"] Katibu Mkuu BAVICHA[/TD]
  [TD="width: 88"] Mchaga[/TD]
  [TD="width: 135"] Moshi – Kilimanjaro[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 37"] 21[/TD]
  [TD="width: 150"] Naomi Kaihula[/TD]
  [TD="width: 228"] Katibu Mkuu BAWACHA[/TD]
  [TD="width: 88"] Mnyakyusa[/TD]
  [TD="width: 135"] Mbeya[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 37"] 22[/TD]
  [TD="width: 150"] Erasto Shija[/TD]
  [TD="width: 228"] Katibu Mkuu WAZEE[/TD]
  [TD="width: 88"] Msukuma[/TD]
  [TD="width: 135"] Shinyanga[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  MAOFISA KATIKA KURUGENZI ZA CHAMA MAKAO MAKUU WANAOWASAIDIA WAKURUGENZI
  [TABLE="class: MsoTableGrid"]
  [TR]
  [TD] S/N[/TD]
  [TD] JNA LA OFISA[/TD]
  [TD="width: 228"] KURUGENZI/WADHIFA WAKE[/TD]
  [TD="width: 88"] KABILA[/TD]
  [TD="width: 135"] MKOA ANAOTOKA[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 37"][/TD]
  [TD="width: 150"][/TD]
  [TD="width: 228"] FEDHA NA UTAWALA[/TD]
  [TD="width: 88"][/TD]
  [TD="width: 135"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 37"] 22[/TD]
  [TD="width: 150"] Mwalwisi[/TD]
  [TD="width: 228"] Mhasibu Mkuu wa chama[/TD]
  [TD="width: 88"] Mnyakyusa[/TD]
  [TD="width: 135"] Mbeya[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 37"] 23[/TD]
  [TD="width: 150"] Jiorojig[/TD]
  [TD="width: 228"] Ofisa utawala wa chama[/TD]
  [TD="width: 88"] Mmbulu[/TD]
  [TD="width: 135"] Mbulu - Manyara[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 37"] 24[/TD]
  [TD="width: 150"] Zuhura Nkya[/TD]
  [TD="width: 228"] Cashier[/TD]
  [TD="width: 88"] Mchaga[/TD]
  [TD="width: 135"] Moshi - Kilimanjaro[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 37"] 25[/TD]
  [TD="width: 150"] Hawa Mwaifunga[/TD]
  [TD="width: 228"] Cashier[/TD]
  [TD="width: 88"] Mnyakyusa[/TD]
  [TD="width: 135"] Mbeya[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 37"] 26[/TD]
  [TD="width: 150"] Edgar Njwaba[/TD]
  [TD="width: 228"] Afisa Matengenezo[/TD]
  [TD="width: 88"] Mnyakyusa[/TD]
  [TD="width: 135"] Kyela - Mbeya[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 37"][/TD]
  [TD="width: 150"][/TD]
  [TD="width: 228"][/TD]
  [TD="width: 88"][/TD]
  [TD="width: 135"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 37"][/TD]
  [TD="width: 150"][/TD]
  [TD="width: 228"] ORGANIZATION NA MAFUNZO[/TD]
  [TD="width: 88"][/TD]
  [TD="width: 135"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 37"] 27[/TD]
  [TD="width: 150"] Hajateuliwa mwingine[/TD]
  [TD="width: 228"] Baada ya kifo cha Regia Mtema[/TD]
  [TD="width: 88"] Aliyekuwa[/TD]
  [TD="width: 135"] Anatoka Morogoro[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 37"][/TD]
  [TD="width: 150"][/TD]
  [TD="width: 228"][/TD]
  [TD="width: 88"][/TD]
  [TD="width: 135"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 37"][/TD]
  [TD="width: 150"][/TD]
  [TD="width: 228"] HABARI NA UENEZI[/TD]
  [TD="width: 88"][/TD]
  [TD="width: 135"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 37"] 28[/TD]
  [TD="width: 150"] Erasto Tumbo[/TD]
  [TD="width: 228"] Ofisa Mwandamizi – Uenezi[/TD]
  [TD="width: 88"] Msukuma[/TD]
  [TD="width: 135"] Kisesa - Shinyanga[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 37"] 29[/TD]
  [TD="width: 150"] Tumaini Makene[/TD]
  [TD="width: 228"] Ofisa wa Habari[/TD]
  [TD="width: 88"] Mkerewe[/TD]
  [TD="width: 135"] Ukerewe - Mwanza[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 37"] 30[/TD]
  [TD="width: 150"] Benson Mramba[/TD]
  [TD="width: 228"] Mkuu wa CHADEMA TV[/TD]
  [TD="width: 88"] Mchaga[/TD]
  [TD="width: 135"] Moshi - Kilimanjaro[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 37"] 31[/TD]
  [TD="width: 150"] Neema Kishebuka[/TD]
  [TD="width: 228"] Mwandishi – CHADEMA TV[/TD]
  [TD="width: 88"][/TD]
  [TD="width: 135"] Morogoro[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 37"] 32[/TD]
  [TD="width: 150"] John Tendwa[/TD]
  [TD="width: 228"] Storekeeper[/TD]
  [TD="width: 88"] Mpare[/TD]
  [TD="width: 135"] Same - Kilimanjaro[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 37"][/TD]
  [TD="width: 150"][/TD]
  [TD="width: 228"][/TD]
  [TD="width: 88"][/TD]
  [TD="width: 135"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 37"][/TD]
  [TD="width: 150"][/TD]
  [TD="width: 228"] SHERIA NA HAKI ZA BINADAMU[/TD]
  [TD="width: 88"][/TD]
  [TD="width: 135"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 37"] 33[/TD]
  [TD="width: 150"] Esther Daffi[/TD]
  [TD="width: 228"] Ofisa wa Sheria[/TD]
  [TD="width: 88"] Mnyanturu[/TD]
  [TD="width: 135"] Singida[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 37"] 34[/TD]
  [TD="width: 150"] J. Mndeme[/TD]
  [TD="width: 228"] Ofisa wa Sheria[/TD]
  [TD="width: 88"] Mpare[/TD]
  [TD="width: 135"] Same - Kilimanjaro[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 37"][/TD]
  [TD="width: 150"][/TD]
  [TD="width: 228"][/TD]
  [TD="width: 88"][/TD]
  [TD="width: 135"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 37"][/TD]
  [TD="width: 150"][/TD]
  [TD="width: 228"] BUNGE NA HALMASHAURI[/TD]
  [TD="width: 88"][/TD]
  [TD="width: 135"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 37"] 35[/TD]
  [TD="width: 150"] Mwita Waitara[/TD]
  [TD="width: 228"] Ofisa wa Sera na Utafiti[/TD]
  [TD="width: 88"] Mkurya[/TD]
  [TD="width: 135"] Tarime - Mara[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 37"][/TD]
  [TD="width: 150"][/TD]
  [TD="width: 228"][/TD]
  [TD="width: 88"][/TD]
  [TD="width: 135"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 37"][/TD]
  [TD="width: 150"][/TD]
  [TD="width: 228"] KAMPENI NA UCHAGUZI[/TD]
  [TD="width: 88"][/TD]
  [TD="width: 135"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 37"] 36[/TD]
  [TD="width: 150"] Suzan Kiwanga[/TD]
  [TD="width: 228"] Ofisa wa kampeni na uchaguzi[/TD]
  [TD="width: 88"][/TD]
  [TD="width: 135"] Kilombero - Morogoro[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 37"][/TD]
  [TD="width: 150"][/TD]
  [TD="width: 228"][/TD]
  [TD="width: 88"][/TD]
  [TD="width: 135"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 37"][/TD]
  [TD="width: 150"][/TD]
  [TD="width: 228"] ULINZI NA USALAMA[/TD]
  [TD="width: 88"][/TD]
  [TD="width: 135"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 37"] 37[/TD]
  [TD="width: 150"] Hemed Sabula[/TD]
  [TD="width: 228"] Ofisa wa Ulinzi na Usalama[/TD]
  [TD="width: 88"] Msukuma[/TD]
  [TD="width: 135"] Mwanza[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 37"][/TD]
  [TD="width: 150"][/TD]
  [TD="width: 228"][/TD]
  [TD="width: 88"][/TD]
  [TD="width: 135"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 37"][/TD]
  [TD="width: 150"][/TD]
  [TD="width: 228"] MAMBO YA NJE[/TD]
  [TD="width: 88"][/TD]
  [TD="width: 135"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 37"] 38[/TD]
  [TD="width: 150"] Leticia Nyerere[/TD]
  [TD="width: 228"] Ofisa wa Mambo ya Nje[/TD]
  [TD="width: 88"] Msukuma[/TD]
  [TD="width: 135"] Kwimba - Mwanza[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 37"][/TD]
  [TD="width: 150"][/TD]
  [TD="width: 228"][/TD]
  [TD="width: 88"][/TD]
  [TD="width: 135"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 37"][/TD]
  [TD="width: 150"][/TD]
  [TD="width: 228"] MABARAZA YA CHAMA[/TD]
  [TD="width: 88"][/TD]
  [TD="width: 135"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 37"] 39[/TD]
  [TD="width: 150"] Subira Waziri[/TD]
  [TD="width: 228"] Naibu Katibu mkuu BAWACHA[/TD]
  [TD="width: 88"] Mhaya[/TD]
  [TD="width: 135"] Bukoba – Kagera[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 37"][/TD]
  [TD="width: 150"] Esther Daffi[/TD]
  [TD="width: 228"] Naibu Katibu mkuu BAVICHA[/TD]
  [TD="width: 88"] Mnyanturu[/TD]
  [TD="width: 135"] Singida[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]


  JUMLA WATU WOTE – 39
  JUMLA YA WACHAGA – 7
  ASILIMIA YA WACHAGA – 7/39 X 100% = 17.95%
   
 12. Chakunyuma

  Chakunyuma JF-Expert Member

  #12
  May 27, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 811
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ujumbe umefika na umewasilishwa vizuri sana hongera nina dogo tu la kurekebisha,
  Tujitahidi kutumia kiswahili vizuri, ona hii
  "chama cha chadema" ukirefusha unapata
  "chama cha chama cha demokrasia na maendeleo"
  sasa hii ni tautology. Tubadilike!
   
 13. A

  Activist p Member

  #13
  May 27, 2012
  Joined: May 20, 2012
  Messages: 48
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hakuna ukweli wowote katika hilo. Tena ukae ukae kimya kabisa.
   
 14. T

  Toshack Kibala Member

  #14
  May 27, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 67
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Afadhari mkubwa kwa ufafanuzi hawa wanaodai wachaga wamejaa chadema huo ni ujinga tu
   
 15. M

  Mercyless JF-Expert Member

  #15
  May 27, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 652
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Haitatokea tena mimi nikaja kumkuheshimu **** kama shibuda. He is BOGUS and USELESS!!!!!
   
 16. Mkereketwa_Huyu

  Mkereketwa_Huyu JF-Expert Member

  #16
  May 27, 2012
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 5,099
  Likes Received: 1,199
  Trophy Points: 280
  Najiuliza. Hivi Mjengwa, we ni Mungu? Pengine nimekosea kwa kutumia hii analogy ila Maggid kwa kweli napenda sana makala zako both in your blog and herein. You are NOT biased kama baadhi ya some notable bloggers hapa Bongo wanao base kupromote CCM wakandamizaji. Viongozi wengi tu CCM wanatumia hii strategy kwa sasa ili kuiyumbisha Chadema. Si huyu panya tu kuna wengine wanasukwa kuja kuivuruga Chadema. #2015 lazima CCM ife tu. Kama tuliteseka miaka ya nyuma na utawala wa JK sasa ndo tutateseka zaidi kwani wanajuwa come #2015 watashindwa, hivyo wanaishia kuiba bila huruma.
   
 17. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #17
  May 27, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Kibaraka mkubwa usio na haya wala hujui vibaya.
   
 18. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #18
  May 27, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145

  Apige mswaki anao?....huyu huwa analala na kuamkia kwenye ofisi za chama cha magamba.....hakumbuki hata kupiga mswaki.
   
Loading...