Uchaguzi 2020 John Shibuda apitishwa kugombea Urais wa Tanzania kwa Chama cha ADA-TADEA

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,500
9,279
1596033119204.png

Chama cha ADA -TADEA kimempitisha John Shibuda kuwa mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kupata kura 120 kati ya kura 130 zilizopigwa na wajumbe wa mkutano mkuu wa chama hicho huku mgombea mwenzake Mastadia Hilari akiambulia kura 10

Aidha, Chama hicho kimechangua Juma Ali Khatib kuwa mgombea wa urais kwa upande wa Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu

Shibuda ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa amesema akishinda Urais atahakikisha anaweka usawa kwa wananchi ikiwemo kuendesha shighuli za kisiasa pasipo kuweka upendeleo kwa yeyote.

=====

KATIBU Mkuu wa Chama cha ADA-Tadea, John Shibuda amepitishwa na wajumbe wa mkutano mkuu wa chama hicho, kugombea urais wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa tarehe 28 Oktoba 2020.
Pia, Juma Ali Khatib ambaye ni waziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar asiyekuwa na wizara maalum amepitishwa na wajumbe hao kugombea Urais wa Zanzibar huku Hassan Karonel Kijogoo atakuwa mgombea mwenza wa Urais wa Tanzania.
Akizungumza katika mkutano mkuu uliofanyika leo Jumanne tarehe 28 Julai 2020 jijini Dar es Salaam, Katibu wa Oganaizesheni ya uchaguzi wa chama hicho, Zuberi Hamis amesema, wagombea nafasi ya urais wa Tanania walikuwa wawili, Shibuda na na Mastadia Hilali Munika na upande wa Zanzibar alikuwa mmoja Khatib.

Amesema wanachama waliopiga kura walikuwa 130 kati ya hizo, Shibuda amepata kura 120 na Mastadia akiambulia kura 10.

Katibu huyo amesema, Khatibu amepata kura 126 na kura nne zilipigwa hapana.
Baada ya kutangazwa mshindi, Shubuda ambaye ni mwenyekiti wa Baraza la vyama vya siasa nchini amesema, akishinda Urais wa Tanzania atahakikisha anaweka usawa kwa wananchi ikiwemo kuendesha shughuli za umma pasina upendeleo wa aina yoyote.

Naye, Khatibu amesema atahakikisha wanawake wanaoishi mazingira magumu hususan wanaopata mimba na wale wenye tabia za kuwakimbia waume zao anawashughulikia katika kipindi kifupi.
 
Ni jambo jema na yeye anaweka historia kwenye maisha yake kuwa amewai kuwa mgombea wa urais tanzania ila naamini hana uhakika wowote kuwa atashinda au atapata hata kura 1000
 
Huyu hajaomba nafasi za wabunge na madiwani kwa "jiwe" ????






Let's meet at the top, cheers 🥂
 
Back
Top Bottom