Monitoring thread: John Pombe Magufuli katika Awamu ya Nne

@alles..
Dunia ina badilika kwa kasi ya ajabu..Lakini hawa jamaa hata hawaoni- Yaani aibu wanazo zitengeneza...Kuzibomoa itaitaji vita... watambue kwamba Jamii ina ona na kusikia...

Ni kipimo gani cha akili tunapaswa kukitumia kama kigezo cha mtu kuruhusiwa kugombea Ubunge...?

Jamaa yupo kimya hata ajibu lolote..Ili tuangalie uwezekano wa Kuuunda wizara mpya.. Nafikiri Hii itakua Wizara ya matapeli waoga ...
 
Mzee Mwanakijiji said:
Wakati mwingine huwa najiuliza kama Rais ana washauri au wapambe tu na wapiga debe?


Mzee Villager,

Tanzania pale hakuna washauri wala watendaji wenye kufanya kazi zao kwa makini na akili. Wote ni wapambe na wapiga debe wanaotaka kupalilia upande wao tu; hapo ndipo tulipoliwa.
 
2006-11-12T21_36_01-08_00.jpg


Kwa wengine ni shujaa na kwa wengine hana tofauti na viongozi wengine wabinafsi na wanaotumia nafasi zao kujinufaisha. Hata hivyo suala zima uuzaji wa nyumba za serikali na maswali yanayohusiana nalo lingeweza kuepukika endapo mambo manne ninayoyazungumzia yangefikiriwa!!! But then, wangeyafikiria ingekuwa ni ajabu!!!

http://mwanakijiji.podOmatic.com/entry/eg/2006-11-12T21_36_01-08_00
 
Mwanakijiji
Nashukuru umeiweka hiyo picha; sipendi kurudiarudia mambo niliyosema huko nyumba. Mimi napinga kwa 100% urudishaji wa nyumba zilizouzwa nina sababu ambazo mimi nadhani ni za msingi. Ni kweli serikali ilichemka katika utaratibu wa kuziuza lakini what is the solution? Kwa mfano watu wengi walionunua nyumba kama hizo kwenye picha hizo nyumba hazipo tena, sasa sijui watarudisha nyumba gani au watawanyang'anya hizo nyumba walizojenga? Kuna vigogo ambao hawakuwa watumishi wa umma waliuziwa hizo nyumba, ni nani atakayewanyang'anya hizo nyumba? Je, ni sheria gani ya nchi ambayo itatumika kuwang'anyanga hizo nyumba au tutahija Azimio jingine la Arusha? Jamani, nchi yetu ina matatizo mengi tukianza kufuatilia matatizo ya nyumba ni miaka 20 hiyo ya kumaliza hayo matatizo pia ukiangalia serikali inafaidika nini na hizo nyumba hakuna lolote lile ni hasara kubwa sana inaingia kwenye hizo nyumba, anyway mimi ni 1 kati ya 100 watanzania amueni wenyewe kwenye hili jambo. Ila mimi nasema no it is more political than the real situation.
 
sam, ni kweli kuwa kunyang'anya hizo nyumba itakuwa jambo gumu hasa kama hakuna utaratibu uliovunjwa. Ndo maana nimependekeza kwanza kabisa kusitisha zoezi zima hadi utaratibu unaoletata utata uondolewa na utaratibu wa wazi zaidi kuwekwa.
 
Mwanakijiji
Bado sijasikiliza maelezo yako nitasikiliza baadaye. Uamuzi wa kuuza hizi nyumba ulitokana na shinikizo la World Bank. Unajua siku hizi hawa jamaa wana watu wao Hazina baada ya kuaona hela nyingi walizokuwa wanatoa zinayeyuka. Baada ya kupitia mahesabu yao wakaona serikali inatumia hela nyingi katika kuhudumia hizi nyumba chakavyo wakaishauri serikali iziuze. Baraza la mawaziri lilikaa na kutua utaratibu wa kuziuza hizi nyumba ambao kwa wakati ule niliuunga mkono kwani sikuona njia nyingine lahisi ya kufanya hili jambo. Nyumba zilitakiwa kuuzwa kwa watumishi wa umma tu siyo viongozi wa kisiasa kama ambavyo imefanyika. Pia baraza la mawaziri lilieleza ni nyumba gani zinatakiwa kuuzwa sasa zimeizwa hadi zili nyumba ambazo hazikutakiwa kuuzwa. Sasa kama watu hawakubaliana na uamuzi wa baraza la mawaziri hilo litakuwa shauri jingine. Kama mtu alipewa maelekezo ya ya usimamizi wa uuzaji na yeye hakufuata kila mtu anajua huyo mtu kazi imemshinda anatakiwa aachishwe kazi mara moja kama kuna namna fulani ya rushwa au ukiukwaji wa sheria huyo mtu anatakiwa apelekwe mahakamani. Baraza la mawaziri halikuamua kuuzwa kwa nyumba ya Ikulu! Huo ni uamuzi wa mtu binafsi. Na kama nchi tutamfanya nini mtu aliyeuza Ikulu bila idhini ya mamlaka yoyote iliyowekwa na wananchi au tutaishia kulalamika kwenye forums? Nakubaliana na wewe kuwa utaratibu uliotolewa na baraza la mawaziri haukuelewaka kwa watendaji wake au waliamua kujinufaisha na huo utaratibu. Nitakusikiliza baadaye niwezo kutoa maoni yangu na mimi.
 
Ukinunua mali ya wizi ni halali unyang'anywe. Wote walionunua nyumbani hizo wameiba jasho la wananchi wa TZ. Kwa kuwa ziliuzwa kwa mlango wa nyuma ni haki ya wote walionunua kufa natai shingoni. Hakuna namna. Acha koleo libakie kuwa koleo. Woote wanyang'anywe. Siyo mangufuli peke yake. Orodha tumeion. Na bado haijakamilika.
 
Kama nilivyokuaidi Mzee Mwanakijiji nimemaliza kusikiliza maoni yako kabla sijasahau napenda kuchukua nafasi hii kuwashauri watu wengine wasikilize pia.

http://mwanakijiji.podOmatic.com/entry/2006-11-12T21_36_01-08_00

Kuhusu magufuli kuandamwa na vyombo vya habari, nadhani ni kweli ni maswala ya kisiasa zaidi nafuatilia litaishia wapi.

Kuna issue ambayo hujaigusia kuna nyumba ambazo zilinunuliwa halafu zikabomolewa ili kujenga nyumba za kisasa wewe unasemaje kuhusu hilo?

Kuna watumishi wa umma walinunua hizo nyumba na baadaye kuwauzia watu wengine na hili tutalitatua vipi?

Na watu wengi walionunua hizi nyumba wame invest (weka hela) kwenye hizo nyumba. Hao watarudishiwa hizo hela au warudishiwe hela walizonunulia?

Mwisho, serikali yetu imeamua kujenga uchumi kwa kutegemea external
investors na hili suala la nyumba ni suala ambalo na wao na wao wanalifuatilia kwani ni wazo toka kwao, je tutawezaji kuwashawishi kuwa tunarudisha nyumba tu hatuwezi kuchukua investments zao mara watakapokuja huku hasa ukizingatia tumeshafanya hivyo mara kadhaa?

Nadhani huu ni wakati muafaka wa kurudisha ile topic yako ya makazi. kama alivyosema mkandara kwenye topic nyingine halmashauri za miji zipewe ruzuku au zimewe ruhusa kukopa kwenye vyombo vya fedha kujenga nyumba za bei rahisi na kuzikodisha na kuweka utaratibu utakaowawezesha watu wasio na makazi kama watumishi wanaoamia miji fulani kupata hizo nyumba kirahisi na hata watu wenye kipato cha chini nadhani hii itakuwa ni muhimu sana katika maendeleo. Halmashauri ya jiji la Dar limeruhusiwa kukopa hela ya jengo la wamachinga 10,000 hivi kila halmashauri inahitaji nyumba 100 nadhani hizo ni nyingi sana. Nadhani serikali irudishe zile nyumba ambazo ni lazima kuwa chini ya serikali kama ile nyumba ya rafiki wako wa Ikulu na hizo nyumba nyingine ziendeshwa na halmashuri za miji. Lazima tukubali makosa yametendeka watu waliohusika kama walivyunja sheria za nchi tunajua kitu cha kuwafanya na kama yalikuwa makosa ya utendaji, hawawezi kazi zao wote waondolewe.
 
Ngoja nimalizizie kabisa!!-1.Magufuli unatakiwa Kujiuzulu...
2.kabla hujafanya hilo jambo la muhimu-Mh-Magufuli Tunaomba ututofautishie Zipi bado ni nyumba za serikali!! na zipi si Nyumba za serikali..najua unajua sana..
Nina maana zile zote zilizo uzwa na kununuliwa kwa mizengwe..Zirudishwe kwa serikali--Fanya haya kabla JK hajarudi-Hii ndiyo iwe style yako ya kutema ngazi...
 
Magufuli ana matatizo kama wenzake, lakini si mchafu kama wao. Hata hiyo habari ya Magufuli katika magazeti ya Rostam Aziz, inatia shaka. Ndivyo walivomfanya Sumaye...wakamalizia na Dk. Salim. Ni watu wachafu, hata kama wameshikilia dola. Na ipo siku...hii ya Magufuli ni cha mtoto.

Tulishasema wananunua hisa katika vyombo vya habari ili kuwaziba waandishi midomo wasiiseme serikali, lakini pia wawatumie waandishi hao hao kuwashambulia wabaya wao ndani ya system, hasa wanaoonekana mashuhuri, ili wakakti ukifika waingize majina yao kugombea urais. Wasivyo na aibu, wameshaanza kampeni. Ndiyo sababu ya Lowassa kuwa mbabe hivyo anaposema, Ndiyo sababu ya popularity anayoijenga kwa kujizunghushia waandishi wa habari, ambao amewaingiza kwenye mtandao kama vibaraka tu!

Ni watu wachafu. Wanatafuta wachafu wenzao na kuwasema sana ili kuficha usafi wao. Kumbuka kuwa Magufuli wa leo hana sababu ya kuandamwa...kama wakubwa wake wanaofanya maamuzi mazito, wanakula na wahindi na waarabu (tazama ziara za urarabuni zimeshafanyika ngapi tangu JK aingie madarakani)..kumbuka ya Mchuchuma na mhindi wa Seacliff aliyewapatia mamilioni ya dola kwa ajili ya kampeni...sasa Richmond.Ushiriki wao ni mchafu na unaua Watanzania. Wao wanamn'ng'ania Magufuli.......i
 
Kumbuka Magufuli alipewa wizara (waliyodhani ni ya pembezoni) ili kutowashtua wananchi kwa nini wanamtema. Lakini hawamtaki, maana likwamisha mambo yao binafsi alipokuwa waziri wa ujenzi, wote wakiwa mawaziri; na hakuwa mwanamtandao - alikuwa anampinga Kikwete; naJK alijua hivyo. Ila kwa kuwa amekuwa na jina kubwa, waliona kumnyima kungezua mazswali kwa wananchi. Sasa wanammaliza pole pole, wamuue baadaye wamzike kisiasa. Kila habari inayoandikwa katika RAI sasa ichunguzwe kwa upande wa pili, ndipo utajua kwa nini wameiandika. Lile gazeti wamelimaliza, sasa limekuwa mdomo wa serikali! Waandishi makini wanalikimbia, wapya hawataki kujiunga, labda wenye njaa...nakwambia. Balaa tupu!
 
Mzee Es,

Waandishi hawawezi kuzigusa za Magufuli. Hawazijui. Wanasubiri kuletewa na kina Rostam, au kuagizwa mahali pa kuzipata. Si unajua tena?
 
Ilitakiwa Magufuli mwenyewe ajibu shutuma hizi na kudhihirisha kuwa ni za uongo.

Maana kwa kweli kama ni propaganda inawork. Mimi binafsi nlikuwa a big fun, lakini u-fun umepungua ingawa bado nampa benefit of doubt.

Angetusaidia sana kama angetoa ufafanuzi kuwa ndugu yake hakupewa ajira ya miezi mitatu na kuuziwa nyumba within hiyo miezi mitatu, akiwa bado ni mwanafunzi. Au adhihirishe kuwa huyu ndugu kachakarika mwenyewe, yeye hakuhusika. Pengine jamaa walitia chumvi kudai eti
Magufuli alikuwa na hilo faili kwapani kulisimamia mwenyewe lipitishwe.

Au sijui hiyo habari ya kimada nae kumuuzia nyumba ya serikali ... vyote hivi avitolee maelezo kujisafisha.

Au labda bado anapanga strategy on how best to counter this. Kukaa kwake kimya kunafanya ziaminike.
 
kichwa maji nakupa five,magufuli ni anaandaliwa political suicide na wanamtandao na wamembana kweli ,siku hizi hasikiki na hata akiongea haiandikwi wanaandika ya ritha,siku hizi hata mkuu wa wilaya anapimana ubavu na magufuli,hata mrema walianza kumfrustrate kidogo kidogo kwa state machinery alipomuhamishia wizara ndogo ya vijana hadi akaondoka,lakini magufuli amechelewa angetakiwa awe anajibu jibu...

magufuli is just good,uamuzi wa kuuza nyumba ulikuwa wa baraza la waziri... akiwemo kikwete sasa kwa nini kumuhukumu mmoja ,,wawajibike wote.
 
I agree with you Kulikoni. Magufuli kama yupo clean anapaswa kuwaumbua hawa wanamtandao. Anavyokaa kimya ni kwamba amekubali! Pamoja na ugomvi wake na wanamtandao,kama alifanya wanayoandika hao Rai, basi naye ana shida kubwa sana. Ni walewale tu!
 
Hivi ili suala la kuondolewa kwa katibu mkuu wa wizara ya miundombinu Eng. Kijazi linaweza kuwa na uhusiano wowote na hii issue ya Magufuli?
 
wazee leteni nyeti.huyu alikuwa right hand wa magufuli pamoja na eng. ndunguru pale ujenzi.let us believe the removal is just in line of duty....
 
President reshuffles permanent secretaries
2006-11-30 10:21:00
By Guardian Reporter
President Jakaya Kikwete yesterday reshuffled permanent secretaries, switching them to different ministries and promoting deputy PSs.

A statement issued by the State House in Dar es Salaam yesterday said the former Infrastructure Development Ministry’s Permanent Secretary, John Kijazi, has been transferred to the Foreign Affairs Ministry, where he would be assigned special duties.

Kijazi’s former position has been taken over by Dr. Enos S. Bukuku, who was formerly in the Ministry of Planning, Economy and Empowerment.

The President has also transferred Ambassador Charles K. Mutalemwa from the Foreign Affairs and International Cooperation Ministry’s PS docket to the Planning Ministry.

Kikwete has promoted the former Deputy Permanent Secretary in the Ministry of Foreign Affairs, Ambassador Patrick C. Mombo, to Permanent Secretary in the same ministry.
The appointments take effect immediately, according to the statement.

### END###

Ni rahisi kuona hapa JK ameua ndege wawili kwa jiwe moja. Kwanza ni kuwaongezea Ulaji Washikaji zake aliowaacha pale Foreign Affairs na pili ni kumpa joto ya jiwe huyu John Kijazi aliyekuwa Infrastructure Development. what is the meaning of "would be assigned special duties." The dude was Ministry’s Permanent Secretary now you are giving him transfer and then tell us he will be assigned "Special Duties"; ukisikia "Afukuzwaye Haambiwi Toka ndio Huku".
 
Back
Top Bottom