John Mwambigija atoa hadharani Ujumbe wa Freeman Mbowe kwa Watanzania kutoka gereza la Ukonga

Mwenyekiti wa Chadema Mbeya Mjini , Mh John Mwambigija alikuwa miongoni mwa wanachama wa Chadema waliosafiri hadi gereza la Ukonga kumuona Mwamba Freeman Mbowe anayeshikiliwa kwenye gereza hilo kwa makosa yanayoitwa ya Ugaidi.

Baada ya kuonana naye Mh Mbowe alimpa ujumbe Maalum Mwambigija ili auweke hadharani kwa manufaa ya Watanzania wote .

Hebu jionee mwenyewe

View attachment 1934830
Peopleeeeees!!! Mbowe aachiwe mara moja!!!
 
..Ni kwasababu CCM bado inaongoza serikali, inaamua vipaumbele vyote vya nchi, na inapanga bajeti.

..mabadiliko yatawezekana kama asilimia 40% ++ ya WABUNGE watatokana na VYAMA MBADALA.

..hilo likitokea CCM na VYAMA MBADALA watakaa meza moja na kuamua kwa pamoja muelekeo wa nchi yetu.

..Na hapo ndipo tutaweza kuvuna MATUNDA ya Demokrasia ya vyama vingi.
Chama mbadala kipi Cha mlevi na mpanga mikakati ya gizan dj

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Mwenyekiti wa Chadema Mbeya Mjini , Mh John Mwambigija alikuwa miongoni mwa wanachama wa Chadema waliosafiri hadi gereza la Ukonga kumuona Mwamba Freeman Mbowe anayeshikiliwa kwenye gereza hilo kwa makosa yanayoitwa ya Ugaidi.

Baada ya kuonana naye Mh Mbowe alimpa ujumbe Maalum Mwambigija ili auweke hadharani kwa manufaa ya Watanzania wote .

Hebu jionee mwenyewe

View attachment 1934830
Mungu ibariki CHADEMA
 
Yule askari Magereza Magereza ulomwambia Peter Madeleka kuwa hawezi kumuona Mbowe kisa anaishi condemn basi achukuliwe hatua kwa sababu aliongea jambo la uongo na la kutia aibu Magereza zetu.
Au wamemtoa kwenye chumba cha condemn wakampeleka pazuri kwa muda.
Mbowe sio gaidi.
 
MBOWE haijarishi Uhuru utakukuta ukiwa gerezani au mahabusu,au hospital au uraiani ukiwa raia huru au kaburini ila utabaki kuwa ALAMA muhimu ya mabadiliko.Tunajua umekuwa mbuzi wa kafara ila USIOGOPE wa usihuzunike Uhuru kamili ya nchi yetu utapatikana.Kuwa kwako gerezani kumenifanya nitoke usingizini kwenye blanket zito niungane na wengine katika harakati za Uhuru.Hakuna njia ya mkato ya kupata Uhuru zaidi ya kudai katiba mpya.katiba mpya lazima ipatikani iwe jua au mvua,by force by power,usiku au mchana,masika au kiangazi ikishindikana italazimika kupita kwenye kivuli Cha mauti au kupita hata kwenye Moto.
 
Huyo John Mwambighija ni mwanachadema mkomavu toka kitambo na ni wale waliokataa kununuliwa enzi za Diwani wa Chadema akimwaga manyanga na kuunga juhudi Geoffrey Kajigili..sijui yupo wapi sasa hivi upepo ushamtoa bara barani..
 
Watu wa Mbeya wamebarikiwa kwa ardhi safi, mvua za kutosha, vyakula kama vyote lakini hawaitaki CCM.

Dodoma kwa wagogo wana shida za kila aina njaa, maradhi, milembe, ukame, kusahauliwa na serikali, viongozi wa ajabu ajabu kama Lusinde na Ndugai ila bado wameikumbatia CCM.

Inahuzunisha ndugu
 
Back
Top Bottom