Mdau
JF-Expert Member
- Mar 29, 2008
- 1,789
- 470
Ndugu wadau, kwa mtizamo wangu, naona kwamba huyu mheshimiwa anajipendekeza mno kwa CCM/serikali.... Chukulia mfano wa matukio haya:....jinsi alivyocheza ngoma wakati wa ziara ya Rais na kumsifu sana, kana kwamba serikali imetimiza yote kwa wananchi, wakati ukweli ni kwamba hata jimboni kwake Bariadi Mashariki, hali ya kipato cha mwananchi wa kawida inasikitisha sana.......pia kitendo cha kupingana na wenzake wa kambi ya Upinzani Bungeni ktk kikao kinachoendelea,ambapo alifukuzwa toka kambi ya upinzani na pia Sitta leo, kuthibitisha adhabu hiyo kimezidi kunipa wasiwasi....
Kama mchambuzi wa siasa,nachukulia mambo haya anayofanya kama ni kutojiamini, woga, kujipendekeza, na kutaka CCM wamuonee huruma ili wasimpe upinzani wa dhati jimboni kwake...(nakumbuka katika moja ya mikutano yake ya kampeni, aliwahi kudai kwamba CCM ni wezi sana,waliwahi kukosea ktk kuiba kura kwenye kituo alichopigia kura yeye na familia yake na wakamuachia kura moja tu!!!). Kwa hali hii,nathubutu kusema Cheyo kageuza ubunge wake kama ajira na si mtumishi wa kweli wa wananchi,jimboni na hata taifani pia....Watanzania tuzidi kuamka,tuweze kutofautisha sasa wanasiasa njaa na wa kweli...