John Mnyika, Zitto, Tundu Lisu, Mchg. Natse, Godbless Lema, Wenje, Vincent Nyerere

payuka

JF-Expert Member
Jun 17, 2010
829
127
Nawapongezeni Kwa Ushindi Wenu, Jueni ya Kwamba Kundi Kubwa la Watanzania wanyonge lipo nyuma yenu:
Muingiapo Mjengoni tunawatuma Mtufanyie mambo yafuatayo na roho zetu zitafarijika:
  1. Kupeleka Hoja ya Kubadili Katiba ya Jamhuri ya Muungano bungeni, na kusimamia kidete kuhakikisha mchakato wa maoni nchi nzima unapitishwa. Na hii ni kwasababu katiba ndo chanzo cha matatizo mengi ndani ya nchi yetu.
  2. Hakikisheni mnarudisha hoja za Ufisadi ndani ya Bunge, Kufuatilia progress ya kesi hewa zilizopo mahakamani.
  3. Hakikisheni mnazitumia vizuri report za CAG kuhusu kaguzi mbalimbali zilizokwishafanyika, Kuna harufu mbaya sana hata kwa zile wilaya zilizopata hati safi!
  4. Pelekeni Shnikizo/Hoja ya kuunda Tume huru ya uchaguzi, Restructuring ya Taasisi kama Takukuru, Nafasi za wakuu wa mikoa pamoja na wilaya.
 
tundu lisu ndani ya nyumba?? oh my GOD what a parliament:smile-big::smile-big::smile-big:
 
100% nakubaliana na wewe! Hususani value for money kwa nafasi za ukuu wa wilaya na mikoa. Haya mambo yanawezekana si mpaka waje wageni na misaada ndio tubadili mambo ya msingi.!
 
Mnyika ameshatangazwa mshindi?! Niko interior sipati nyuuzi jamani hebu tupashane nasi tushehereke.:israel:
 
Highnes Wilson,Freeman Mbowe,Philemon Ndesamburo,John Shibuda na wengine mpaka nashindwa kuwamention kwa wingi wao,pls nawaombeni sana nendeni mkatutumikie wananchi mana najua mnajua kiu yetu ni mabadiliko,mmemuona Dr.Slaa yeye ni kama chachu amewaongoza vyema nyinyi kupata ushindi,pls tena pls mkatutetee najua nyinyi kwa uchache wenu mna nguvu kiliko huo utitiri wa wabunge wa ccm mana binfsi mbunge mmoja wa chadema naona ni zaidi ya wabunge 30 wa ccm.Mungu ibariki Tanzania Mungu wabariki wabunge wote wateule wa Chadema.:smile::smile::smile::smile::smile::smile::smile:
 
Wawe na malengo katika kutimiza ahadi - waweke mpango kazi (action plan) wa ahadi walizotoa ili waweze kuzifuatilia kwa umakini ili 2015 iwe mteremko.
 
Waheshimiwa Silinde, Wenje, Ndesamburo, Freeman Mbowe, John Shibuda, Mpendazoe
Vilio vya wananchi Kukaa barabarani, Kupigwa mabomu ya machozi kwa kutetea Kura Zao si bure....Wameona mbali juu ya mwenendo mzima wa serikali yetu Na majinamizi ya Rushwa na Kashfa mbalimbali. Pls Pls Jitahidini kufanya kila namna kuiweka serikali kwenye Hot Seat ili iwajibike!
 
Asante mpayukaji kwa kujali kwako. Hoja yangu kubwa ipo katika kurekebisha tume ya uchaguzi ya tanzania. Kama umefutailia vizuri, ni zaidi au karibu nusu ya wapiga kura walioandikishwa hawakuweza kutimiza haki yao ya msingi kwa sababu za kisiasa zaidi. Ukiangalia kwa mfano jimbo la kyela, 90% ya waliojiandikisha waliweza kupia kura.hii ni kwa sababu CCM ilikua na uhakika wa kura kupitia mgongo wa Mwakyembe. Lakin jaribu kufuatilia maeneo ambayo upinzani ni mkubwa,wapiga kura hawajafika hata nusu ya idadi waliyoandikishwa. Maana yake ni kuwa, tume ya uchaguzi imetumiwa na CCM kuhakikisha kuwa wapiga kura wa maeneo hayo ya wapinzani wanakuwa na kasoro katika vipengele vya namba ya kuandikishwa,kubadili jina, kutoyakuta majina kabisa, kukosa picha katika daftari hali ambayo imetuchangia kupunguza kura za upinzani. Lakini CCM wajue kuwa this is just the beginning of the end.They can fool us sometimes,but cant fool all of us ALL THE !TiME


[Justice Delayed,is justice denied. William E. Gladstone. UK PM 1868-1894]
 
Jamani igeni na mfuate nyayo za baba yetu dr slaa msiende kulala kwenye viti wanavyofanya wengine na mfano mzuri ni mramba piganeni kiume jamani taifa la tanzania liko mikononi mwa chadema na nyuma yenu jamani msitusaliti wanyone tunalia .
 
Ifike wakati wabunge wawe wanalipwa ela majimboni kwao ili ukilala unaambulia patupu
 
NMEIPENDA HIYO YA SILINDE SASA NAJUA ANAENDA KUPAMBANA NAO NDANI AO CCM WALIOMSIMAMISHA SKULI MDA MREFU..
big upppppppp
 
Msijione ni wachache eti sababu mnatoka kambi ya upinzani, ninyi ni wengi sana!

As a rule of thumb fanya yafuatayo:
  1. Kuwa na confirmed evidence kwa kila hoja unayojenga, Usikurupuke.......
  2. Kuwa na reliable sources of info ndani ya CCM, Wizara nyeti, Kwenye Private institutions na Hata Askari Wa Usalama itawasaidieni sana.
 
nawapongezeni kwa ushindi wenu, jueni ya kwamba kundi kubwa la watanzania wanyonge lipo nyuma yenu:
Muingiapo mjengoni tunawatuma mtufanyie mambo yafuatayo na roho zetu zitafarijika:
  1. kupeleka hoja ya kubadili katiba ya jamhuri ya muungano bungeni, na kusimamia kidete kuhakikisha mchakato wa maoni nchi nzima unapitishwa. Na hii ni kwasababu katiba ndo chanzo cha matatizo mengi ndani ya nchi yetu.
  2. hakikisheni mnarudisha hoja za ufisadi ndani ya bunge, kufuatilia progress ya kesi hewa zilizopo mahakamani.
  3. hakikisheni mnazitumia vizuri report za cag kuhusu kaguzi mbalimbali zilizokwishafanyika, kuna harufu mbaya sana hata kwa zile wilaya zilizopata hati safi!
  4. pelekeni shnikizo/hoja ya kuunda tume huru ya uchaguzi, restructuring ya taasisi kama takukuru, nafasi za wakuu wa mikoa pamoja na wilaya.

asante sana , mabadiliko yatakuja tz kwa kubadilika katiba, the true change
 
hao mimi sina wasiwasi nao lazima wawakilishe vizuri maana nawaaminia
 
Sugu najua wasanii wote utawatetea kwa nguvu sana ukiwa na 1st hand experience ya uchakachuaji unaofanywa hasa na wabiashara wa kiasia katika kuwanyonya hasa kazi za wasanii. Kuwe na mfumo wa kueleweka wa nyie kupata royalties zenu. Pia toa singo moja Kali kuliko ile ya uliyotaka "kuua mtu"! Maana ukishaingia mjengoni ukiimba vya ndani vyaweza kukurudi, lakini makuaminia kwa mafumbo ndio maana hata ruge akakosa kukupin down! Mimi na wewe twajua ulitaka kumuua nani! Peace.
 
Back
Top Bottom