John Mnyika, Zitto, Tundu Lisu, Mchg. Natse, Godbless Lema, Wenje, Vincent Nyerere

Nawapongezeni Kwa Ushindi Wenu, Jueni ya Kwamba Kundi Kubwa la Watanzania wanyonge lipo nyuma yenu:
Muingiapo Mjengoni tunawatuma Mtufanyie mambo yafuatayo na roho zetu zitafarijika:

  1. Kupeleka Hoja ya Kubadili Katiba ya Jamhuri ya Muungano bungeni, na kusimamia kidete kuhakikisha mchakato wa maoni nchi nzima unapitishwa. Na hii ni kwasababu katiba ndo chanzo cha matatizo mengi ndani ya nchi yetu.
  2. Hakikisheni mnarudisha hoja za Ufisadi ndani ya Bunge, Kufuatilia progress ya kesi hewa zilizopo mahakamani.
  3. Hakikisheni mnazitumia vizuri report za CAG kuhusu kaguzi mbalimbali zilizokwishafanyika, Kuna harufu mbaya sana hata kwa zile wilaya zilizopata hati safi!
  4. Pelekeni Shnikizo/Hoja ya kuunda Tume huru ya uchaguzi, Restructuring ya Taasisi kama Takukuru, Nafasi za wakuu wa mikoa pamoja na wilaya.

Ulikua sawa kutomweka sugu kwenye distribution list.
Hapa hawezi kuelewa ktu.
 
Ni kweli Shujaa Mwanaharakati Mwanasheria TUNDU LISU ametangazwa MSHINDI? Jameni hebu ni hakikishieni nikatafute eneo lenye madini nikachimbe!
 
Mwanzo Mzuri Kuelekea 2015!
Tunataka PESA za wa-Tanzania zirudishwe! EPA na wenzao wote wasipumue! Ni timu ya kuharakisha mageuzi!
 
Back
Top Bottom