John Mnyika usitetee uovu, kama kuna mtu anahusika kutafuna mali ya umma acha apate hatua stahiki

Chagu wa Malunde

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
8,708
5,711
Kama mtanzania mpenda ukweli nimefarikija kuona PCCB wakitoa taarifa kuwa bado wanaendelea na uchunguzi juu ya ubadhilifu wa bil 8 zilizotafunwa na viongozi wa Chadema.

Mbali ya hayo wamesisitiza kuwa wataendelea na uchunguzi juu ya ubadhilifu uliokuwa unafanyika kwenye mifuko ya majimbo, ambayo inasadikiwa kuwa wabunge wa upinzani wa bunge la 11 walifanya ubadhilifu.

Jambo ambalo linashangaza ni kitendo cha John Mnyika kama kiongozi wa Chadema kutoa kauli kuwa kuchunguza ubadhilifu wa mifuko ya jimbo ni sahihi lakini kuchunguza michango ya wanaCdm iliyotafunwa na viongozi wa Chadema sio sahihi. Hii kauli sio njema kabisa kwani michango iliyotafunwa na viongozi wa Chadema sio mali ya umma?

Hii ni dhahiri kuwa hapa Tanzania bado hatujapata wapinzani wa ukweli bali tuna wajaza matumbo
 
Kama mtanzania mpenda ukweli nimefarikija kuona Pccb wakitoa taarifa kuwa bado wanaendelea na uchunguzi juu ya ubadhilifu wa bil 8 zilizotafunwa na viongozi wa Chadema..
Ubadhilifu wa taasisi au mtu wa ndani yeyote haukubaliki. Na pia ubadhilifu wa fedha za wafadhili ukifanywa na mtu au taasisi haukubaliki. Trilioni za Assad, Covid 19 na MV. Magogoni ni deni ambalo linatakiwa lilipwe na waliofanya bila kujali sura wala cheo. Double standard is intorelable/unacceptable.
 
Ubadhilifu wa taasisi au mtu wa ndani yeyote haukubaliki. Na pia ubadhilifu wa fedha za wafadhili ukifanywa na mtu au taasisi haukubaliki.Trilioni za Assad,covid 19 na MV.Magogoni ni deni ambalo linatakiwa lilipwe na waliofanya bila kujali sura wala cheo. Double standard is intorelable/unacceptable.
nkese sababu unao ushahidi wa hayo unayoyasema basi jilipue uweke ushahidi hadharani kama Waitara. Pia fika ofisi za Pccb ili ulisaidie taifa lako kupambana na ubadhirifu.
 
Katibu wa sasa wa Chadema ni dhaifu kuliko makatibu wote dhaifu waliowahi kushika nafasi hiyo kwenye chama hicho. Udhaifu wake unajidhihirisha kwenye kauli yake hiyo ya kipuuzi uliyonukuu!
Ila akiunga juhudi anakuwa SHUPAVU. CCM bado mnaweweseka na bado mtahangaika sana.
 
nkese sababu unao ushahidi wa hayo unayoyasema basi jilipue uweke ushahidi hadharani kama Waitara. Pia fika ofisi za Pccb ili ulisaidie taifa lako kupambana na ubadhirifu.
Nisipowapa mie huo ushahidi hawachunguzi? Ushahidi gani zaidi wanasubiri mbali ya taarifa ya CAG waliyemfanyia mizengwe hadi kumtengua? Tr. zile hazifutiki kwa kiki na mbwembwe za madaraka na majukwaani. WE EXPECT THEM TO LIVE UP TO THEIR SLOGANS!
 
Nisipowapa mie huo ushahidi hawachunguzi? Ushahidi gani zaidi wanasubiri mbali ya taarifa ya CAG waliyemfanyia mizengwe hadi kumtengua? Tr. zile hazifutiki kwa kiki na mbwembwe za madaraka na majukwaani. WE EXPECT THEM TO LIVE UP TO THEIR SLOGANS!
Kwani mimi na wewe tulijua kuwa bil 8 zimetafunwa? Mwita Waitara ndio aliibua hii kitu.
 
Back
Top Bottom