Uchaguzi 2020 John Mnyika, Uchaguzi huu msifanye masikhara na maslahi ya Mawakala

chakii

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
19,685
22,694
Kwako Katibu Mkuu wa CHADEMA Ndg John Mnyika.

Mwaka 2015 uligombea ubunge Jimbo la Kibamba, hongera ulifanikiwa kupita kutokana na mawakala waliojitoa kufa kupona kwa ajili yako, wapo waliokataa kuhongwa, wapo walioumizwa na wapinzani wako, na wengine walitaka mpaka kuondolewa Uhai kwa kulinda kura zako na CHADEMA.

CHADEMA Mwaka 2015 mlicheza sana na maslahi ya mawakala wenu, chakula kilikuwa cha kubabaisha sana, mawakala wa vyama vingine waliwahishiwa chakula kwa wakati huku mawakala wenu wakipiga miayo tu, hii siyo sawa kabisa na ni kuwatia majaribuni Mawakala wenu.

Pia posho hamkuwa tiyari kuwalipa, Mnyika unakumbuka vizuri mawakala wako uliwafanya wakakesha pale Ngome mpaka saa sita usiku wakikusubiri wewe ili walipwe posho zao na wakati unajua kabisa ulishashinda bado hukujali mawakala wako ukawalipa elfu 10 TU, na wengine walichoka kukusubiri wakaondoka wenyewe kwa gharama zao bila kupata chochote!

Sasa endelezeni tena huu Uhuni kwenye Uchaguzi huu wa 2020.
 
Nimesikia leo mawakala wa CCM wameambiwa wakiona kwenye kituo CCM wamezidiwa kura kwenye kuzihesabu basi waanzishe fujo ambapo polisi watakuja na kuwatoa nje mawakala wote huku nyuma kura zilichochakachuliwa zikiingizwa vituoni. Mawakala wakirudi watakuta kuna kura mpya na zikihesabiwa tena itaonekana CCM wameshinda.

CHADEMA wekeni mkakati kudhibiti hili
 
Nimesikia leo mawakala wa Ccm wameambiwa wakiona kwenye kituo Ccm wamezidiwa kura kwenye kuzihesabu basi waanzishe fujo ambapo polisi watakuja na kuwatoa nje mawakala wote huku nyuma kura zilichochakachuliwa zikiingizwa vituoni. Mawakala wakirudi watakuta kuna kura mpya na zikihesabiwa tena itaonekana Ccm wameshinda.

Chadema wekeni mkakati kudhibiti hili
Hii yote itatokana na utimamu wa Mawakala
 
Duuu, Mungu anawaona ,arawadhalilisha kabla mapema.hujuma yoyote ile toka kwa chama chochote kile,ita-kikost hicho chama
 
Nimesikia leo mawakala wa Ccm wameambiwa wakiona kwenye kituo Ccm wamezidiwa kura kwenye kuzihesabu basi waanzishe fujo ambapo polisi watakuja na kuwatoa nje mawakala wote huku nyuma kura zilichochakachuliwa zikiingizwa vituoni. Mawakala wakirudi watakuta kuna kura mpya na zikihesabiwa tena itaonekana Ccm wameshinda.

Chadema wekeni mkakati kudhibiti hili
2015 kuna MTU alichezewa huo mchezo sikumbuki ni Wenje ama nano,Ila natumaini watajifunza safari hii.
 
Vyama vihakikishe vinawajali mawakala, mawakala wenye njaa ni tatizo kubwa.
Wakala anajua hatalipwa, wakala hata haletewi chakula ale, mwisho wa siku ni shida tu.

Sent from my Infinix X603 using JamiiForums mobile app
 
Nimesikia leo mawakala wa Ccm wameambiwa wakiona kwenye kituo Ccm wamezidiwa kura kwenye kuzihesabu basi waanzishe fujo ambapo polisi watakuja na kuwatoa nje mawakala wote huku nyuma kura zilichochakachuliwa zikiingizwa vituoni. Mawakala wakirudi watakuta kuna kura mpya na zikihesabiwa tena itaonekana Ccm wameshinda.

Chadema wekeni mkakati kudhibiti hili
Acha siasa maji taka, CHADEMA walishashindwa kabla ya kuanza kampeni za Uchaguzi. Yaani LISSU huyu huyu awe Rais wa Jamhuri? Tuwe serious kidogo.
 
Acha siasa maji taka, CHADEMA walishashindwa kabla ya kuanza kampeni za Uchaguzi. Yaani LISSU huyu huyu awe Rais wa Jamhuri? Tuwe serious kidogo.
8A93FE9B-DB1A-4CD3-AA5A-44E6140B4C27.jpeg
 
2015 chadema waliwalipa elfu10
2020 wanawalipa sh ngapi? Au ndio wameahidiwa teuzi?
 
Nimesikia leo mawakala wa Ccm wameambiwa wakiona kwenye kituo Ccm wamezidiwa kura kwenye kuzihesabu basi waanzishe fujo ambapo polisi watakuja na kuwatoa nje mawakala wote huku nyuma kura zilichochakachuliwa zikiingizwa vituoni. Mawakala wakirudi watakuta kuna kura mpya na zikihesabiwa tena itaonekana Ccm wameshinda.

Chadema wekeni mkakati kudhibiti hili
NEC bana kunawakati walipiga marufukku simu mimi nikabaki nashanga baadae nikasikia wameruhusu
 
Majimbo yaliyoongozwa na Chadema tumeshudia wakitunyanyasa Watanzania
Mkuu huna hoja now dayz umeshapitiwa na genge la walopokaji...... bukoba... watu wamemkataaa shetan na kaz zake live asa sijui na Meko ni CDM
 
Chadema wakitunyanyasa sana Watanzania, sasa basi bukoba wanamlilia Rais Magufuli awakomboe
Mkuu huna hoja now dayz umeshapitiwa na genge la walopokaji...... bukoba... watu wamemkataaa shetan na kaz zake live asa sijui na Meko ni CDM
 
Back
Top Bottom