John Mnyika: Siri hadharani kuwezesha hatua za ziada za kisheria kuchukuliwa dhidi ya Mhando

Fredrick Sanga

JF-Expert Member
Jan 27, 2011
3,153
697
Na JOHN MNYIKA

Nimeamua kuchukua hatua ya kuiweka hadharani ripoti hii ya SIRI ya ndani ya Shirika la Umeme (TANESCO) ya maoni ya kisheria juu ya ukaguzi maalum uliofanywa na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi niliyoitoa tarehe 1 Novemba 2012.

Kwa mujibu wa nyaraka hii ni wazi aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme (TANESCO) William Mhando amefanya makosa mengi yanayohitaji hatua za ziada za kisheria ikiwemo ya mgongano wa maslahi, utovu wa uaminifu, kushindwa kutangaza maslahi na matumizi mabaya ya ofisi; matendo ambayo ni ya kifisadi.

Makosa hayo na mengine ni kinyume cha sheria mbalimbali za nchi ikiwemo Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini, Sheria ya Ununuzi wa Umma na sheria nyingine.

Hivyo, kwa kuwa Bodi imekataa kuwa haitachukua hatua za zaidi za kisheria juu yake natoa kauli ya ziada kwamba mamlaka zingine zinazohusika zichambue Taarifa hii sanjari na Taarifa ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) na kuchukua hatua za kisheria zilizochini ya mamlaka hizo.

Mamlaka hizo ni pamoja na Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Mamlaka ya Ununuzi wa Umma (PPRA), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Sekretariati ya Maadili ya Umma zote kila moja kwa nafasi yake zichunguze ukiukwaji wa sheria katika masuala yaliyo kwenye majukumu yao na kuchukua hatua za ziada.

Aidha, wakati mamlaka na taasisi hizo zikiendelea kuchukua hatua za kisheria naitaka kwa mara nyingine bodi ieleze hatua ilizochukua dhidi ya watendaji wengine wa TANESCO walioshirikiana naye kwa namna moja au nyingine na iwapo bodi hiyo haitachukua hatua za haraka, ukiondoa majina ya maafisa watatu waliosimamishwa mpaka sasa nitataja majina ya ziada ya maofisa wengine waliohusika na kutaka Rais Jakaya Kikwete kuingilia kati kwa mamlaka yake ya kikatiba na kuchukua hatua ikiwemo dhidi ya bodi yenyewe.

Ikumbukwe kwamba kufuatia kufukuzwa kazi kwa Mhando kwa nafasi yangu ya Waziri Kivuli wa Nishati na Madini tarehe 1 Novemba 2012 nilitoa kauli ya awali kwamba hatua hiyo pekee haitoshi bali Serikali irejee katika hotuba niliyotoa tarehe 27 Julai 2012 bungeni kwa niaba ya kambi rasmi ya upinzani na kuchukua hatua zaidi za kuwezesha Mhando na wenzake kufikishwa mahakamani.

Aidha, pamoja na hatua za ziada nilitaka bodi ya TANESCO kueleza hatua ilizochukua dhidi ya watendaji wengine wa TANESCO walioshirikiana naye kwa namna moja au nyingine na iwapo bodi hiyo haitachukua hatua za haraka niliahidi kuiweka hadharani taarifa ya kamati iliyoundwa na bodi hiyo kuchambua taarifa ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na kueleza hatua ambazo zinapaswa kuchukuliwa na Rais Jakaya Kikwete dhidi ya Bodi yenyewe.

Kufuatia kauli yangu hiyo tarehe 3 na 7 Novemba 2012 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) Jenerali Mstaafu Robert Mboma alinukuliwa baadhi ya vyombo vya habari akisema kwamba aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo William Mhando hawezi kushitakiwa mahakamani kwa sababu kosa alilofanya la kuingia kwenye mikataba yenye mgongano wa kimaslahi ni kosa la kiuadilifu.

Mwenyekiti wa Bodi ametaja kosa moja tu la mgongano wa kimaslahi wakati ambapo yapo makosa mengine na naamini kauli yake imetokana na ushauri wa kwenye kipengele cha 36 na 37 cha nyaraka niliyoambatanisha; maoni ambayo bodi ilipaswa kuyachukulia kwa tahadhari na kutaka mamlaka na vyombo vya uchunguzi kuendelea na hatua zao za ziada kuwezesha hatua za kisheria kuchukuliwa.

Aidha alieleza kwamba kuhusu maofisa wengine watatu waliosimamishwa sambamba na Mhando bodi yake inasubiri taarifa ya ukaguzi unaofanywa na Mkaguzi Mkuu na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG) ili kubaini kama wana makosa wachukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria na kuahidi kwamba uchunguzi dhidi yao ungekamilika ndani ya wiki moja na kueleza kuwa hatma yao ingejulikana tarehe 16 Novemba 2012 ahadi ambayo mpaka leo tarehe 23 Novemba 2012 haijaitekeleza.

Katika muktadha huo kwa kuwa suala hili tayari limeshatolewa kauli kwenye vyombo vya habari kwa nyakati mbalimbali na Wizara ya Nishati na Madini pamoja na TANESCO, mawasiliano ya kawaida ya kiofisi na kuendelea kuficha taarifa za siri kama hii hakutalisaidia taifa kujinusuru kwa haraka na ufisadi. Hivyo, kusambaza taarifa hii hadharani na kutaka majibu ya wazi toka kwa mamlaka zote zinazohusika kutawezesha hatua za haraka kuchukuliwa kwa maslahi ya umma.

Wenu katika uwakilishi wa wananchi,

John Mnyika (Mb) Waziri Kivuli wa Nishati na Madini.

NOTE: Download attachment chini

My take:
Mwaka huu kuna mengi sana, wananchi tusome sana.
 
Attachments

  • An-Opinion-in-Respect-of-the-Report-of-Cag-12-10-2012-Final.pdf
    382.4 KB · Views: 487
Kuhamishana na kuoondoana madarakani bila sheria kuchukuwa mkondo wake nikulindana.

Kama kiongozi kahujumu shirika la umma kwanini asifungwe japo kwa uchache miaka minne?

Wanaendeleza madudu kila siku kwasabab wanajuwa watahamishwa au kuondolewa madarkani bila hatua kali zaidi juu yao.
 
Na JOHN MNYIKA

Nimeamua kuchukua hatua ya kuiweka hadharani ripoti hii ya SIRI ya ndani ya Shirika la Umeme (TANESCO) ya maoni ya kisheria juu ya ukaguzi maalum uliofanywa na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi niliyoitoa tarehe 1 Novemba 2012.

Kwa mujibu wa nyaraka hii ni wazi aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme (TANESCO) William Mhando amefanya makosa mengi yanayohitaji hatua za ziada za kisheria ikiwemo ya mgongano wa maslahi, utovu wa uaminifu, kushindwa kutangaza maslahi na matumizi mabaya ya ofisi; matendo ambayo ni ya kifisadi.

Makosa hayo na mengine ni kinyume cha sheria mbalimbali za nchi ikiwemo Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini, Sheria ya Ununuzi wa Umma na sheria nyingine.

Hivyo, kwa kuwa Bodi imekataa kuwa haitachukua hatua za zaidi za kisheria juu yake natoa kauli ya ziada kwamba mamlaka zingine zinazohusika zichambue Taarifa hii sanjari na Taarifa
 
Asante sana mkuu kwa doc.hii
Kusema kweli hawa Wanasheria waliopewa kazi ya kuandaa maoni ya Kisheria kwa Board ya Tanesco wamefanya Kazi Nzuri sana.

Kwa upande wa Board nawapa big Up kwa Uamuzi wao wa Kuishia kwenye -termination ya Mhando na lazima wamalizie na wengeine waliobaki.

Mhe.J.Mnyika kwa nafasi yake kama Mbunge anaweza sasa kupitia Bunge kuleta hoja ya kutaka Mhando na wengine wa chukuliwe hatua za Kisheria na Mamlaka zingine zinazotakiwa kulinda/kusimamia Sheria kama alivyodokeza hapa chini.
Hii ni Demokrasia na natural justice lazima ifanye kazi na ionekane inafanya kazi.

Mamlaka hizo ni pamoja na Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Mamlaka ya Ununuzi wa Umma (PPRA), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Sekretariati ya Maadili ya Umma zote kila moja kwa nafasi yake zichunguze ukiukwaji wa sheria katika masuala yaliyo kwenye majukumu yao na kuchukua hatua za ziada.
 
Ili taifa liweze kuheshimiwa,lazima adhabu kali zitolewe kwa wanao lihujumu.Kwa hekima za raisi wetu, naamini hao watawajibishwa.This time anawafanyia timing kwanza.HONGERA KIJANA MWENZETU MNYIKA,KWA JUHUDI KAMA HIZI TAIFA LITAPONA
 
tatizo Watz walio wengi hawana access na social media ili kujua/kufahamu uhalifu unaofanywa na watawala na wengi wao ni wale tuliowachagua kitu ambacho kina/ kitachelewesha harakati za kuleta mabadiliko kwenye huu mfumo tulionao
 
Naomba muisome kwa makini hiyo document, opinion iliyotolewa na wanasheria hao watatu inaashiria ugumu Fulani wa ushahidi kukubalika mahakamani kwa kuwa haukidhi vigezo kadha wa kadha.
 
Back
Top Bottom