JOHN MNYIKA: Salamu Za Mshikamano Kuunga Mkono Maandamano Ya Wadau Wa Habari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JOHN MNYIKA: Salamu Za Mshikamano Kuunga Mkono Maandamano Ya Wadau Wa Habari

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Simba mnyama, Aug 1, 2012.

 1. Simba mnyama

  Simba mnyama JF-Expert Member

  #1
  Aug 1, 2012
  Joined: Jul 14, 2012
  Messages: 348
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kwa niaba ya Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) tukiwa ni sehemu ya wadau wa sekta ya habari nchini, tunaunga mkono maandamano ya amani mliyoitisha ya kupinga hatua ya serikali kulifungia gazeti la MwahaHALISI.

  Tunawapongeza wahariri kwa mshikamano wenu katika kipindi hiki cha majaribu; endeleeni kusimama pamoja, ni umoja wenu ndio utakaokuwa kinga ya pamoja dhidi mtu au chombo chombo chochote kinachoingilia uhuru wenu. Mshikamano wenu ni ishara ya kushindwa kwa mkakati wa ‘wagawe uwatawale' na imani kwamba umoja ni nguvu. Wahariri wote hawapaswi kukaa kimya kuhusu kufungiwa kwa MwanaHALISI kwa kuwa leo ni kwa gazeti hilo, kesho itakuwa kwa gazeti lingine; hivyo ni vyema kuungana pamoja kulinda uhuru, taaluma na sekta ya habari nchini.

  Kwetu sisi hatua hiyo ya serikali tunaitafsiri zaidi ya kufungia gazeti la MwanaHALISI; ni hatua ya kufungia uhuru wa kusambaza habari na uhuru wa kupokea habari. Hivyo hatua hiyo ni kinyume cha haki za binadamu, kinyume cha utawala bora na ni kikwazo kwa demokrasia na maendeleo. Hakika serikali na viongozi wake wamevuka mstari wa kukubali kukosolewa na sasa wameamua kuanza kufungia uhuru wa fikra mbadala.

  Hatua ya Waziri mwenye dhamana na sekta ya habari kugeuka mlalamikaji, mwendesha mashtaka na mfungaji ni mwelekeo mbovu wa kupuuza taasisi za kusimamia uwajibikaji na haki. Uamuzi uliofanywa na serikali hauna tofauti na unaofanywa na raia wanaojichukulia sheria mikononi(mob justice). Kwa serikali inayoheshimu misingi ya asili ya haki, tulitarajia chombo chochote cha habari, kikivunja sheria ama kukiuka maadili dhidi ya serikali, viongozi wake ama watu binafsi mashtaka ama malalamiko yangepelekwa kwa taasisi zinazohusika mathalani Baraza la Habari(MCT) ama Mahakama.

  Hatua ya serikali kufungia gazeti la MwanaHALISI pamoja na kuwa imechukuliwa kwa mujibu wa sheria iliyopo, imekiuka misingi ya asili ya utawala wa sheria. Kwani kulikuwa na sheria nyingine nzuri ambazo serikali ingeweza kutumia kupitia mahakama lakini ikaamua kuchagua kutumia sheria mbaya kwa kutumia mamlaka ya Waziri. Itakumbukwa kwamba wadau wa sekta ya habari na hata serikali yenyewe imekuwa ikikiri kwamba Sheria hiyo iliyotumiwa ni sheria mbovu inayohitaji kufutwa ama kufanyiwa marekebisho makubwa ikiwemo kupunguza mamlaka makubwa ya viongozi wa serikali dhidi ya vyombo vya habari.

  Sheria yoyote inayotambulika kuwa mbovu katika jamii yoyote, inapoteza uhalali wa kihaki(legitimacy) miongoni mwa umma na hivyo kuendelea kuitumia ni kuteteresha misingi ya utawala wa sheria na kutoa mfano mbaya kwa vijana nchini na wananchi kwa ujumla. Hivyo, tunachukua fursa hii kuitaka serikali kuharakisha mchakato wa kupitisha sheria ya vyombo habari na sheria ya uhuru wa taarifa.


  Aidha tumeshangazwa na uamuzi wa serikali kufanya maamuzi yake kwa ubaguzi kwa kulichukulia hatua gazeti la MwanaHALISI na kukwepa kuyachukulia hatua magazeti mengine ambayo yameandika habari inayoshabihiana na maudhui ya habari iliyoandikwa na gazeti hilo. Kwa muda mrefu sasa, habari za uwepo wa viongozi ama makundi ndani ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) yenye kupanga ‘kumng'oa' Rais Jakaya Kikwete miongoni mwa wanaotarajiwa kugombea urais kupitia chama hicho mwaka 2010 zimeandikwa na magazeti mbalimbali.

  Hatua hii ya kibaguzi inaibua maswali kuhusu dhamira ya serikali kulifungia gazeti hilo wakati huu ambapo mchango wa gazeti hilo na mengine yaliyo mstari wa mbele kupinga ufisadi na kutetea rasilimali za taifa unahitajika kwa kiasi kikubwa. Hata baada ya kulifungia gazeti la MwanaHALISI, habari za aina hiyo zimeendelea kuandikwa ikiwemo na vyombo vya habari vya nje; mathalani tarehe 24 Oktoba, 2008 kutoka Ufaransa gazeti la Africa Intelligence inayomtaja Rostam Aziz kukusanya fedha kwa ajili ya kufadhili kundi lake katika uchaguzi huo. Katika muktadha huo, serikali inapaswa kulifungia gazeti la MwanaHALISI mara moja, kama imeonyesha wazi kushindwa kuyachukulia hatua magazeti mengine.


  Kadhalika kwa mtiririko wa matukio katika taifa letu, kuna mwelekeo wa Serikali na CCM kuminya maoni yenye kumkosoa au kumgusa Rais Kikwete. Mjadala wa Rais Kikwete ‘kung'olewa' katika uchaguzi mwaka 2010 unaelekea kuichukiza kwa kiasi kikubwa Serikali na CCM. Gazeti la MwanaHALISI liliandika habari ya namna hiyo, likafungiwa na Serikali. Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe akiwa katika ‘Operesheni Sangara', alitoa hoja hiyo na matokeo yake CCM ikaibuka na kujibu kwa vitisho na vioja.

  Vijana wa Tanzania wangependa kupata mfano uongozi bora wenye kukubali kukosolewa na kukubali mabadiliko badala ya uongozi legelege wenye kuendeleza udikitekta wa kimawazo na hivyo kuminya fikra huru. Si dhambi kwa CHADEMA ama mtu yoyote kutaka kuiondoa CCM ama kiongozi wake yoyote madarakani mwaka 2010 kupitia njia za kidemokrasia.

  Mwisho, tunatoa mwito kwa watanzania wote kusoma alama za nyakati na kuunga mkono harakati hizi za wahariri na wadau wa sekta ya habari kutetea uhuru wa kweli katika taifa letu. Jamii itambue kwamba kitisho cha uhuru na haki kwa mtu Fulani au mahali Fulani ni tishio kwa watu wote na mahali pote. Yanayofanywa kwa vyombo vya habari, yanaweza pia kufanywa kwa watetezi wengine kwani hivi karibuni taifa limeshuhudia Asasi ya HAKIELIMU ikitishiwa kutokana na jitihada zake za kuhamasisha mabadiliko ya fikra katika sekta ya elimu na kupiga vita ufisadi unaoathiri sekta hiyo. Tuko katika kipindi cha majaribu; kuibuka kwa mijadala yenye kuchochea mgawanyiko/ubaguzi, kuongezeka kwa matabaka na malalamiko juu ya hali za maisha. Katika wakati huu ambapo misingi ya nchi yetu iliyopo katika Ngao ya Taifa ya Uhuru na Umoja inapotikiswa ni wakati wa kuunganisha "Nguvu ya Umma" kupinga aina zote za ufisadi na kutetea rasilimali za taifa kwa kuhamasisha maadili, fikra mbadala na mabadiliko ya kweli. Kuunga mkono maandamano ya wadau wa sekta ya habari ni sehemu ya azma hiyo. Mshikamano, daima; pamoja, tutashinda!


  Wasalaam,


  John Mnyika
  Mkurugenzi wa Vijana Taifa.
   
 2. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #2
  Aug 1, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,945
  Likes Received: 1,270
  Trophy Points: 280
  walaaniwe Magamba
   
 3. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #3
  Aug 1, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  safi sana Jembe JJ, Serikali inafungia gazeti FIKRA je?
   
 4. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #4
  Aug 1, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Leo hii serikali za uk au marekani wangekua wanafungia magazeti yanayoandika habari zao ungekuta leo hii hizo nchi hazina gazeti hata moja... Bt wao wana practice freedom of press ambayo hapa tz hakuna.
   
 5. t

  thatha JF-Expert Member

  #5
  Aug 1, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Lakini kama mlimsikiliza Kubenea akihojiwa na BBC alisema ni Mwanahalisi pekee ndo wenye kuandika habari za kiuchunguzi kwa kwamba vyombo vingine ni vioga, sasa je Jasiri ataweza kuungwa mkono na mwoga? Yangu macho.
   
 6. t

  thatha JF-Expert Member

  #6
  Aug 1, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Simba mnyama Lakini ni Kubenea huyo huyo aliyesema wakati akihojiwa na BBC juzi kuwa ni Mwanahalisi pekee ndilo lenye uwezo wa kuandika habari za kiuchunguzi na kwamba vyombo vingine ni vioga. Je hao waoga wako tayari kummunga mkono Jasiri Kubenea?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #7
  Aug 1, 2012
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,344
  Likes Received: 3,111
  Trophy Points: 280
  Serikali ya ccm inafungia gazeti letu pendwa mwanahalisi?......walaaniwe hawa mafisadi
   
 8. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #8
  Aug 1, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,671
  Trophy Points: 280
  Chadema pamoja na Mnyika lazima waandamane gazeti la Mwanahalisi linamilikiwa na kiongozi wa Chadema.
   
 9. h

  hans79 JF-Expert Member

  #9
  Aug 1, 2012
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 3,802
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  Acha ukuwadi kwani unakusaidia nini?Jenga hoja acha kutoka hewa chafu hima.
   
 10. d

  dotto JF-Expert Member

  #10
  Aug 1, 2012
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  N imani radio inamilikiwa na kiongozi wa ccm
   
 11. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #11
  Aug 1, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,671
  Trophy Points: 280
  Dogo JF sio mali ya Chadema hiyo ndio hoja unataka hoja gani nimsifie Mbowe...narudia tena Mwanahalisi R.I.P ni mali ya kiongozi wa Chadema...wewe Chadema wanakusaidia nini.
   
 12. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #12
  Aug 1, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,671
  Trophy Points: 280
  Mkuu tutajie jina tumfahamu.
   
 13. 2

  21DEC2012 Senior Member

  #13
  Aug 1, 2012
  Joined: Oct 25, 2011
  Messages: 116
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mheshimiwa John Mnyika hapo kwenye red sijapaelewa vizuri.
   
 14. s

  sweke34 JF-Expert Member

  #14
  Aug 1, 2012
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 2,533
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Hivi una umri gani weye? mbona unaandika utumbo tuu?
   
 15. PMNBuko

  PMNBuko JF-Expert Member

  #15
  Aug 1, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 971
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Si sawa kulifungia Gazeti hilo. Habari zile zinatusaidia sisi wananchi. Tumenyima uhuru wa kupata taarifa. Ni mwendelezo wa udhaifu wa JK na serikali yake.
   
 16. K

  KEBUKA New Member

  #16
  Aug 1, 2012
  Joined: Aug 1, 2012
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naamini ukweli utamweka kila mtu huru!! Kufungia mwanahalisi sio kufungia watu kufikiri hapa serikali inayajaza maji kwenye wavu!
   
 17. Tutafika

  Tutafika JF-Expert Member

  #17
  Aug 1, 2012
  Joined: Nov 4, 2009
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 160
  Kumbe hiyo ndio sababu ya kufungiwa, basi maandamano ni muhimu
   
 18. Domy

  Domy JF-Expert Member

  #18
  Aug 1, 2012
  Joined: Dec 12, 2011
  Messages: 4,702
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Tuko pamoja Mwanahalisi mtashinda tu
   
 19. mangikule

  mangikule JF-Expert Member

  #19
  Aug 1, 2012
  Joined: Jun 11, 2012
  Messages: 3,162
  Likes Received: 1,251
  Trophy Points: 280
  Uhuru na habari leo linamilikiwa na CC Mabwepande!!
   
 20. Wile GAMBA

  Wile GAMBA JF-Expert Member

  #20
  Aug 1, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 1,809
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  kuna kitu kibaya sana kinaendelea, hauwezi kutawala kwa hila kwa kuwafunga watu midomo, kweli utafanikiwa kuwafanya usoni wakuchekee lakini kwenye roho zao watakuwa wanaomba usiku na mchana upotee katioka uso wa dunia hii... kusema kweli mwana halisi lilikuwa halina unafki katika kuandika... kufungiwa kwake imeniuma sana. hii ni aibu kubwa sana kwa serikali goigoi,
   
Loading...