John Mnyika nini mkakati wako ukiwa Mbunge wa Ubungo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

John Mnyika nini mkakati wako ukiwa Mbunge wa Ubungo?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mstahiki, Mar 31, 2010.

 1. m

  mstahiki JF-Expert Member

  #1
  Mar 31, 2010
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 310
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kijana John Mnyika,

  Naomba utueleze una mpango,mikakati gani ya kutatua kero za Wananchi wa Ubungo ikiwa ukishinda Uchaguzi?
   
 2. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #2
  Apr 1, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Kuanzisha mahakama ya kadhi maana JK kashindwa ...u happy now?!
   
 3. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #3
  Apr 1, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,598
  Likes Received: 3,890
  Trophy Points: 280
  Swali zuri sana mstahiki, je unaishi hapo ubungo?

  Unaweza kuorodhesha matatizo ya hapo ubungo unayoyaona yapo? ili kusudi Mnyika akija ajue ataweza lipi?
   
 4. Mndundu

  Mndundu JF-Expert Member

  #4
  Apr 1, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 225
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Swali la kwanza, jimbo letu linakituo kikubwa na mabasi yanayounganisha jiji na mikoa mingine, je ana mpango gani wa kuhakikisha kwamba mapato yanayopatikana kutokana na kituo hicho sehemu yake pia yanachangia maendeleo ya jimbo letu (kuongeza huduma za kijamii kama vyoo, miundo mbinu ya na kadharika).
   
 5. John Mnyika

  John Mnyika Verified User

  #5
  Apr 1, 2010
  Joined: Jun 16, 2006
  Messages: 715
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0

  Mstahiki, Asante kwa swali lako, naomba nirudie nilichosema Machi 21: Wakati wa kampeni bado, hivyo sitazungumzia kwa sasa ahadi zangu kwenu wala ilani ya chama; lakini inatosha kuwaambia tu kwamba: ni wakati wa mabadiliko; tuwajibike. Naamini katika kuwa na uongozi bora wenye dira na uadilifu wa kuwezesha uwajibikaji katika kusimamia rasilimali za umma ikiwemo kodi zetu na mali asili za nchi yetu kwa ajili ya kujenga taifa lenye kutoa fursa kwa wote.

  Ningeshauri pia thread hii iunganishwe na hii ambayo ipo tayari hapa: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/56794-natangaza-rasmi-dhamira-ya-kugombea-ubunge-2010-a.html

  Siku njema

  JJ
   
 6. John Mnyika

  John Mnyika Verified User

  #6
  Apr 1, 2010
  Joined: Jun 16, 2006
  Messages: 715
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Mndundu

  Asante. Swali la kuahidi nitafanya nini naomba nisilijibu kwa ukamilifu kwa sasa mpaka wakati wa kampeni. Lakini naomba urejee msimamo wangu kuhusu kituo hiki toka mwaka 2005 unaweza ukapata mwelekeo kidogo wa msimamo gani nitauchukua: http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=7604

  ama unaweza kusoma hapa pia: http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=11005

  Pamoja na kuwa huu mradi umerudishwa kwa serikali, bado kuna hatua zinapaswa kuchukuliwa: Mosi, kuhusu tuhuma za ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka na kusababisha hasara kwa serikali katika kipindi cha 2004-2009. Pili; kuweka mpango mbadala wa uendeshaji wa kituo husika katika kipindi cha 2010 na kuendelea utakahakikisha wananchi wanapata huduma bora wakati huo huo yanapatikana mapato ya kutosha. Sasa ni mpango gani huo? Na nini naahidi kuwawakilisha wananchi kuhakikisha kwamba kinafanyika kama sehemu ya kuiwajibisha serikali ndio naomba nisizungumzie kwa sasa mpaka wakati muafaka.

  Pamoja na hayo, bado nashauri tena thread hii iunganishwe na hii: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/56794-natangaza-rasmi-dhamira-ya-kugombea-ubunge-2010-a.html ambayo imebeba masuala na maswali yenye mwelekeo kama wa thread hii.

  Nawatakia mjadala mwema

  JJ
   
Loading...