John Mnyika: Naibu spika Job Ndungai ni dhaifu

John W. Mlacha

JF-Expert Member
Oct 4, 2007
3,504
1,341
Mnyika kumkatia rufaa Naibu Spika Send to a friend
Monday, 25 June 2012 08:30
0digg

Raymond Kaminyoge
MBUNGE wa Ubungo, John Mnyika amesema anakusudia kukata rufaa kwa Kamati ya Bunge ya Kanuni dhidi ya Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai kutokana na uamuzi wa kumtoa bungeni wiki iliyopita.

Wiki iliyopita Mnyika alitolewa bungeni baada ya kukataa kufuta kauli yake kuwa ‘Rais Jakaya Kikwete ni dhaifu’.
Jana, katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Mnyika alisema anakusudia kukata rufaa dhidi ya Ndugai, ili kuwe na mjadala mpana wa kibunge utakaoweka kumbukumbu sahihi.

Alisema uamuzi huo wa kukata rufaa kwa Kamati ya Kanuni za Bunge, unalenga kupata haki.
Mnyika alisema kutamka kuhusu udhaifu wa Rais, si kumtukana wala siyo kutumia jina lake kwa dhihaka.
“Pamekuwapo na propaganda za kudai kuwa kauli hiyo ni matusi, chanzo ni udhaifu wa Naibu Spika Ndugai, kwa kunihukumu kwa kutumia kanuni tofauti na tuhuma iliyotolewa,” alisema.

Alifafanua kwamba, “Naheshimu taasisi ya urais na umri, naamini pia katika matumizi ya lugha za kidiplomasia, hata hivyo, niliamua kuusema ukweli kwa lugha ya moja kwa moja ili ujumbe ufike kwa mamlaka zote.”
Alisema hata viongozi wa dini na taasisi mbalimbali, wamekuwa wakisema hadharani kuhusu udhaifu huo wa rais.
Kuhusu Bajeti, Mnyika alisema wabunge wamekuwa na udhaifu kutokana na Katiba kuweka nguvu kubwa kwa Rais, kwamba wasipopitisha Bajeti anaweza kulivunja Bunge.
“ Woga huo wa Rais kulivunja Bunge ndiyo maana wamekuwa wakipitisha Bajeti kwa kauli za `ndiyo’ kwa asilimia 100, hata kama kuna maeneo ambayo wanayapinga,” alisema Mnyika katika taarifa yake hiyo.
Mbali na kukata rufaa, aliongeza, “Bunge litakapokuwa likijadili utekelezaji wa bajeti katika Ofisi ya Rais 2012/13, nitaeleza hatua ambazo Rais anapaswa kuchukua kufanikisha ahadi alizozitoa kwa Watanzania.”
Alisema anaamini, Rais Kikwete anayo fursa ya kurekebisha, ili kuongeza nguvu zake katika kupanua wigo wa mapato na hatimaye kuongeza kiwango cha fedha za maendeleo.
 
Monday, 25 June 2012 08:30

Raymond Kaminyoge

MBUNGE wa Ubungo, John Mnyika amesema anakusudia kukata rufaa kwa Kamati ya Bunge ya Kanuni dhidi ya Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai kutokana na uamuzi wa kumtoa bungeni wiki iliyopita.
Wiki iliyopita Mnyika alitolewa bungeni baada ya kukataa kufuta kauli yake kuwa ‘Rais Jakaya Kikwete ni dhaifu'.
Jana, katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Mnyika alisema anakusudia kukata rufaa dhidi ya Ndugai, ili kuwe na mjadala mpana wa kibunge utakaoweka kumbukumbu sahihi.
Alisema uamuzi huo wa kukata rufaa kwa Kamati ya Kanuni za Bunge, unalenga kupata haki.
Mnyika alisema kutamka kuhusu udhaifu wa Rais, si kumtukana wala siyo kutumia jina lake kwa dhihaka.
"Pamekuwapo na propaganda za kudai kuwa kauli hiyo ni matusi, chanzo ni udhaifu wa Naibu Spika Ndugai, kwa kunihukumu kwa kutumia kanuni tofauti na tuhuma iliyotolewa," alisema.
Alifafanua kwamba, "Naheshimu taasisi ya urais na umri, naamini pia katika matumizi ya lugha za kidiplomasia, hata hivyo, niliamua kuusema ukweli kwa lugha ya moja kwa moja ili ujumbe ufike kwa mamlaka zote."
Alisema hata viongozi wa dini na taasisi mbalimbali, wamekuwa wakisema hadharani kuhusu udhaifu huo wa rais.
Kuhusu Bajeti, Mnyika alisema wabunge wamekuwa na udhaifu kutokana na Katiba kuweka nguvu kubwa kwa Rais, kwamba wasipopitisha Bajeti anaweza kulivunja Bunge.
" Woga huo wa Rais kulivunja Bunge ndiyo maana wamekuwa wakipitisha Bajeti kwa kauli za `ndiyo' kwa asilimia 100, hata kama kuna maeneo ambayo wanayapinga," alisema Mnyika katika taarifa yake hiyo.
Mbali na kukata rufaa, aliongeza, "Bunge litakapokuwa likijadili utekelezaji wa bajeti katika Ofisi ya Rais 2012/13, nitaeleza hatua ambazo Rais anapaswa kuchukua kufanikisha ahadi alizozitoa kwa Watanzania."
Alisema anaamini, Rais Kikwete anayo fursa ya kurekebisha, ili kuongeza nguvu zake katika kupanua wigo wa mapato na hatimaye kuongeza kiwango cha fedha za maendeleo.

Source: Mwananchi
 
Hakika mbunge wa ubungo anasumbuliwa na laaana ya Kikwete anaendelea kuweweseka na jambo ambalo kimsingi limeshapita! Mnyika fanya mambo mengine hasa kutatua kero za jimbo la ubungo kama ulivyo waahidi wananchi!
 
usiwe mvivu wa kufikiri, Ndugai kamhukumu kwa kutumia kanuni tofauti na tuhuma iliyotolewa jombaa
 
Udhaifu wa Ndugai ni pale alipomtaka Mnyika atoke nje ya VIWANJA VYA BUNGE KABISA badala ya NJE YA UKUBMBI WA BUNGE TU.
Hapo anaweza kufunguliwa mashitaka ya UDHALILISHAJI na bwana Mnyika na katika hilo anaweza hata kumdai fidia kama akitaka.
 
Hakuna lolote hapo zaidi yakutafuta umaarufu wa kisiasa. Na hata huko hakuna atakae kusikiliza zaidi yakujichoresha na kujifutia hadhi yako km mbunge kijana. Kijana mwenzetu shughulikia matatizo ya wan a ubungo, kuliko kutafuta umaarufu
 
sasa mnataka aongeze pesa kwenye bajeti ya maendeleo alafu yeye safari zake za nje ya nchi zilipiwe na nani? lazima wajifikirie kwanza wao..maendeleo mumsubiri Rais mwingine 2015
 
Dalili zinaonesha anajejua maana halisi ya Kauli ya huyu Kijana ni yeye Mwenyewe.
 
Mnyika kumkatia rufaa Naibu Spika Send to a friend
Monday, 25 June 2012 08:30
0digg

Raymond Kaminyoge
MBUNGE wa Ubungo, John Mnyika amesema anakusudia kukata rufaa kwa Kamati ya Bunge ya Kanuni dhidi ya Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai kutokana na uamuzi wa kumtoa bungeni wiki iliyopita.

Wiki iliyopita Mnyika alitolewa bungeni baada ya kukataa kufuta kauli yake kuwa ‘Rais Jakaya Kikwete ni dhaifu'.
Jana, katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Mnyika alisema anakusudia kukata rufaa dhidi ya Ndugai, ili kuwe na mjadala mpana wa kibunge utakaoweka kumbukumbu sahihi.

Alisema uamuzi huo wa kukata rufaa kwa Kamati ya Kanuni za Bunge, unalenga kupata haki.
Mnyika alisema kutamka kuhusu udhaifu wa Rais, si kumtukana wala siyo kutumia jina lake kwa dhihaka.
"Pamekuwapo na propaganda za kudai kuwa kauli hiyo ni matusi, chanzo ni udhaifu wa Naibu Spika Ndugai, kwa kunihukumu kwa kutumia kanuni tofauti na tuhuma iliyotolewa," alisema.

Alifafanua kwamba, "Naheshimu taasisi ya urais na umri, naamini pia katika matumizi ya lugha za kidiplomasia, hata hivyo, niliamua kuusema ukweli kwa lugha ya moja kwa moja ili ujumbe ufike kwa mamlaka zote."
Alisema hata viongozi wa dini na taasisi mbalimbali, wamekuwa wakisema hadharani kuhusu udhaifu huo wa rais.
Kuhusu Bajeti, Mnyika alisema wabunge wamekuwa na udhaifu kutokana na Katiba kuweka nguvu kubwa kwa Rais, kwamba wasipopitisha Bajeti anaweza kulivunja Bunge...

Hakuna lolote hapo zaidi yakutafuta umaarufu wa kisiasa. Na hata huko hakuna atakae kusikiliza zaidi yakujichoresha na kujifutia hadhi yako km mbunge kijana. Kijana mwenzetu shughulikia matatizo ya wan a ubungo, kuliko kutafuta umaarufu
 
Hakika mbunge wa ubungo anasumbuliwa na laaana ya Kikwete anaendelea kuweweseka na jambo ambalo kimsingi limeshapita! Mnyika fanya mambo mengine hasa kutatua kero za jimbo la ubungo kama ulivyo waahidi wananchi!
Ni lini mwenye dhambi akawa na uwezo wa kutuma laana ikafika. Kikwete ana laana ya kudanganya watz wakampa Urais akawageuka na kula na wezi na familia yake hii pekee ni LAANA. pole wewe
 
Tena ni wote DHAIFU.... Ukitaka kujua Job, Anne na wenyeviti wao ni dhaifu angalia wanavyoendesha bunge
 
Hakuna lolote hapo zaidi yakutafuta umaarufu wa kisiasa. Na hata huko hakuna atakae kusikiliza zaidi yakujichoresha na kujifutia hadhi yako km mbunge kijana. Kijana mwenzetu shughulikia matatizo ya wan a ubungo, kuliko kutafuta umaarufu
Rudisha pesa ya Nepi tafadhali,mwache kijana wetu na kamanda wetu atuongoze kwenye mapambano...kwa taarifa yako majority tuliopigika na wenye akili zao wanamsupport mwazo mwisho....
 
Eti anatafuta umaarufu mbona ni maarufu kitambo sana tulie bwana wenu apigwe sindano za moto mnaweweseka wote nnaotetea UDHAIFU wa yule DHAIFU wa magogoni ningeweza msingeandikishwa kwenye vitambulisho vya uraia....Laana kum nyie.
 
Ondoa wehu wako na upumbavu wako hapa . Nyie vibaraka wa ccm mnakera sana kwa kutumia masaburi kufikiri na kuendekeza njaa kwa kujipendekeza hata Kama ukweli mnaujua but mko tayari kuupotosha kwa maslahi yenu binafsi. Halafu kwa bahati mbaya mnawaza sawa, si mbunge, waziri, mwananchi wa kawaida, profesa, dokta, na hata yule wa form two Kama katibu wenu aliyepita.

Inshallah siku yenu inakuja tena I karibu sana, mtaenda kunyea debe wote bila kujali jana unakisukari wala kiharusi. Shame on you all magambazi. I hate you I can't even explain.

Mnyika huu upuuzi utaucha lini aiseee? sijui ni utoto , sijui nikutafuta umaarufu, sijui ni ulimbukeni wa siasa na uzoefu wa siasa nk. Hili jambo ulilitaka mwenyewe kwa kuvunja kanuni ya 64 ya kulitumia jina la rais vibaya, sasa unalalamika nn hapo zaidi yakujichoresha tu?.Watu wa ubungo, wan a matatizo makubwa na mpaka sasa hujatekeleza hata ahadi moja, badala yaku concentrate na jimbo lako una ung'ang'ania vitu simple and shallow. Kweli sasa naanza kuamini mnyika unatafuta umaarufu wa kisiasa.
 
mnyika achana na suala hili. kwa mujibu wa kanuni za bunge, ulivunja kanuni. naibu spika vilevile alitumia kanuni za bunge kukuadhibu. mimi binafsi nakukubali mnyika. nakushauri uachane na kadhia hii. endeleza jitihada za kulijenga jimbo lako la ubungo
 
Hakuna lolote hapo zaidi yakutafuta umaarufu wa kisiasa. Na hata huko hakuna atakae kusikiliza zaidi yakujichoresha na kujifutia hadhi yako km mbunge kijana. Kijana mwenzetu shughulikia matatizo ya wan a ubungo, kuliko kutafuta umaarufu

Mh. Lukuvi, mwanasiasa mzoefu, aliyepita bila kupingwa jimboni kwake, alikiri, wakati akimuomba Mh. Mnyika afute kauli yake, kuwa katika wabunge makini na wenye uwezo wa kuchambua mambo ni Mnyika. Wewe ambaye hata maana ya siasa hujui, bila aibu unaamua kuaanika upeo wako mdogo wa kufikiri. Umewahi kujiuliza kwa nini Mnyika pamoja na umri wake alishinda jimbo kama la ubungo? Sitaki kuamini kuwa uwezo wako wa kufanya analysis hata nje ya siasa utashindwa kuchanganua hili. Pole!!!
 
Back
Top Bottom