Ukwaju
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 13,370
- 11,090
kumbuka maneno yako ktika thread no 1Mkuu sikiliza,
Mwigulu tangu wakati anaomba mwongozo na sikusikia maneno ya kusamehe.
Hivyo, thread ile ama mleta mada alikurupuka ama amedhamiria kupotosha kilichoelezwa.
Suala la kuvunja Bunge hilo si mada yangu. Tusirefushe thread kwa kuleta hoja ambazo mngeweza kuanzisha thread nyingine ingekuwa ni efficient step.
Hivyo, watanzania tuamke tulitizame jambo hili kwa muono huo na si kulalamika kama tumeishiwa hoja. Tunajadili katiba mpya na hivyo kesi kama hizi ni kipimo kwetu kuona kama kweli tunaelewa tunalojadili au la.
Hatuwezi kuendelea kuona Spika akivunja katiba kwa kutoa upendeleo na ubaguzi ambao umekatanzwa na vifungu tele vya katiba yetu. Sasa tujikite wote tulitizame kuwa ni jambo la katiba.
Wabunge wa CHADEMA watumie nafasi yao kulipeleka hili suala Mahakamani maana nis suala la kuvunjwa kwa katiba. Ushahidi upo mwingi tu kuonyesha Bunge ni taasisi inayoendekeza ubaguzi.
Jamaa yangu huenda wewe sio Mbunge lakini km ni Mbunge kwa nini usitoke nje kwamba hukubaliani na yanayoendelea humo ndani na wanaokukubali nao wafuate nyuma
Lakini km Raia wa kawaida usiwachochee wao wakiona hawaelewani watapatana kwa jambo jingine tu, lakini sio kuwadanganya eti Wamshtaki Spika Anne na Naibu Job ili iweje Bunge livunjwe?
Mbona Kikao kikimalizika wanakusanya Posho zao na wanakutana Chako ni chako kwenye kuku, na hakuna anayekataa eti kakandamizwa na kuanza kupigana vikumbo.
Naomba ya Ngoswe muachie Ngoswe wao kukashifiana watajijua sisi tuangalie Bajeti ya leo ya Ardhi wamepitisha suala la WAPANGAJI NA WENYE NYUMBA?
Kumbuka Ndugai keshasema taarifa anazipata katika mitandao ya kijamii wanazitembelea na kuona tunavyodanganyana
Ushauri wa mwisho chukua fomu za kuingia mjengoni na ukamshitaki Spika mm nitakuunga mkono sio humu hata 0.3% ya Watanzania hawatusikii