John Mnyika na CHADEMA nendeni Mahakamani. Anne Makinda na Job Ndugai wamevunja Katiba bungeni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

John Mnyika na CHADEMA nendeni Mahakamani. Anne Makinda na Job Ndugai wamevunja Katiba bungeni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nikupateje, Jul 12, 2012.

 1. N

  Nikupateje JF-Expert Member

  #1
  Jul 12, 2012
  Joined: Dec 22, 2009
  Messages: 1,314
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Leo Mwigulu Mchemba ameomba mwongozo kuhusu ushahidi wa John Mnyika alioufikisha kwenye ofisi za Bunge.

  Cha msingi hapa ni kwamba Job Ndugai ameeleza kuwa wabunge waache tabia ya uongo na kujiamini kwamba wana ushahidi. Ndugai ameeleza kwamba wote ambao waliwahi kufikisha ushahidi kwa Spika Hakuna hata mmoja aliyeleta ushahidi unaokidhi vigezo vya ushahidi.

  Kuhusu ushahidi alioleta Mnyika, Ndugai kasema kwamba Mnyika ameleta maelezo ya utangulizi na wala si ushahidi halisi. Hivyo, kwa suala hili la Mnyika ameamua kulifikisha kwenye Kamati ya Maadili ya Bunge na huko Mnyika ataandikiwa barua kama hatua ya kwanza.

  Binafsi hapa sina matatizo na uamuzi wa Job Ndugai, uamuzi wa kiti cha Spika. Sitetei uhalisi wa ushahidi aliowasilisha John Mnyika.

  Hoja yangu ni jinsi Ofisi ya Spika inavyoshughulikia masuala haya.

  Tangu Bunge hili la 10 limeanza chini ya Anne Makinda kama Spika, sikumbuki ni idadi gani ya wabunge hasa wa CHADEMA wameombwa kuleta ushahidi na wakaleta. Kwa kutaja ninaojua ni Godbless Lemma, Zitto Kabwe, Ezekah Wenje nk.

  Lakini leo ni miezi 17 imepita tangu mtu wa kwanza kuambiwa alete ushahidi na haukushughulikiwa. Ushahidi huo ni ule wa Godbless Lemma ambaye sasa hauhitajiki kwa sababu mbunge hoja yake inakufa anapokoma kuwa mbunge na hivyo suala la Lemma limefungwa hivyo.

  Lakini bado kuna ushahidi mwingi wa wengine una zaidi ya mwaka hatuoni kasi yoyote ya kushughulikia.

  Sasa umekuja ushahidi wa John Mnyika. Haujamaliza hata siku mbili Kiti cha Spika kimetoa maamuzi kwamba upelekwe Kamati ya Maadili na haki ili Mnyika aanze kuwajibika kwa kuandikiwa barua. Narudia simetetei Mnyika na inawezekana kabisa ushahidi wake ni hafifu na ikibidi ni wa uongo.

  Taaabu yangu ni kwamba kiti cha Spika kimeonyesha double standards ambazo watazania wote tunaendelea kuangalia kana kwamba tunaangalia ngumi za jogoo wawili wakipigana na kama vile sisi haituhusu.

  Iwapo John Mnyika ataandikiwa barua, bais huo ni ushahidi tosha kwamba Spika amefanya amevunja katiba. Je, Spika kavunja katiba kwa namna gani?

  Ibara ya 9(h) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano inasema hivi: { Kwa hiyo, Mamlaka ya Nchi na vyombo vyake vyote vinawajibika kuelekeza sera na shughuli zake zote katika lengo la kuhakikisha kwamba aina zote za dhuluma, vitisho, ubaguzi, rushwa, uonevu au upendeleo zinaondolewa nchini }.

  Ibara ya 13(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano inasema hivi: {Watu wote ni sawa mbele ya sheria, na wanayo haki, bila ya ubaguzi wowote, kulindwa na kupata haki sawa mbele ya sheria}.

  Wakati humohumo katibani Ibara ya 13(2) inasema hivi: {Ni marufuku kwa sheria yoyote iliyotungwa na mamlaka yoyote katika Jamhuri ya Muungano kuweka sharti lolote ambalo ni la ubaguzi ama wa dhahiri au kwa taathira yake}.

  Kama yapo mengine yanayotaja neno ubaguzi au upendeleo basi mtaonyesha lakini kwa hoja yangu hapa inanitosha. Sasa ubaguzi unaokatazwa na katiba unaigusaje issue hii ya ushahidi wa John Mnyika?

  Ubaguzi ni kwamba Ofisi ya Spika wa bunge lilelile ameonyesha sura mbili kwa suala lilelile yaani kushughulikia ushahidi. Ni kweli kuwa kanuni hazitaji ni lini na kwa haraka gani Spika anatakiwa kushughulikia masuala haya ya kuuanika ushahidi au kuushughulikia.

  Lakini hapa tumeona kuwa suala la ushahidi wa John Mnyika Spika hakusubiri hata masaa 48 yapite.

  Hivyo, hii ni nafasi ya kulichukulia jambo hili kuwa ni la katiba. Kuna watu watakuja na hoja kwamba Bunge lina kinga. Hawa ni wale ambao hawajui maana ya kinga na hawajsoma utaratibu wa kinga au sheria ya kinga.

  Hakuna mtu hapa nchini aliye juu ya katiba. Hakuna taasisi iliyo juu ya Katiba, siyo Ikulu au Ofisi ya Bunge, siyo Rais wan chi siyo Spika au Naibu Spika. Kinga ya bunge ni kinga kwa ajili ya kuendesha majadiliano maadamu majadiliano hayo hayavunji haki ya mtu yeyote duniani.

  Bunge, mbunge, Spika, Naibu Spika wote hao waliapa kulinda katiba na si kuvunja hata kipengele kimoja.

  Je, uvunjaji wa Katiba ni uhalifu wa aina gani? Kwa kiingereza wapo wanaouita “treason”. SIna hakika kama “Uhaini” ndilo neno sahihi kwa dhambi ya uvunjaji wa katiba.

  Kuvunja katiba si lazima uvunje vipengele vyote. Na mara nyingi si rahisi kuvunja katiba yote maana hiyo sasa itakuwa si uvunjaji wa katiba bali hayo ni “Mapinduzi” kama mapinduzi yoyote duniani.

  Kuvunjwa katiba ni pale kinapovunjwa kipengele kimoja au kadhaa vya katiba.

  Kwa hoja hii ya John Mnyika, vipengele vyote vinavyozuia ubaguzi ndani ya Jamhuri yetu vimevunjwa. Hii sasa ni kesi ya kikatiba. Mahala pake ni mahakamani. John Mnyika akipata barua basi huo ndiyo mwanzo wa kulipeleka suala hilo Mahakamani.

  Ninaweza kutaja mifani mingi ya mambo ya mabunge ya Commonwealth kufikishwa mahakamani lakini hata hapa Augustine Mrema alishawahi kupinga adhabu yake bungeni kwa kwenda mahakamani. Japo Mrema alishindwa kwenye kesi ile iliyoendeshwa na Jaji Katiti lakini Mahakama haikuzuia case ile eti tu kwa sababu ni jambo limetokea bungeni.

  Hata msingi wa kesi ya Mrema ilijikita kwenye misingi ya Katiba kwamba pamoja na kutoridhika na adhabu ya kufungiwa ile adhabu ilikuwa inamnyima haki yake ya kikatiba kushiriki vikao vya Bunge. Pendekezo ambalo lilikataliwa na Jaji Katiti kwamba kuhudhuria vikao vya Bunge si haki ya kikatiba.


  Hivyo, watanzania tuamke tulitizame jambo hili kwa muono huo na si kulalamika kama tumeishiwa hoja. Tunajadili katiba mpya na hivyo kesi kama hizi ni kipimo kwetu kuona kama kweli tunaelewa tunalojadili au la.

  Hatuwezi kuendelea kuona Spika akivunja katiba kwa kutoa upendeleo na ubaguzi ambao umekatanzwa na vifungu tele vya katiba yetu. Sasa tujikite wote tulitizame kuwa ni jambo la katiba.

  Wabunge wa CHADEMA watumie nafasi yao kulipeleka hili suala Mahakamani maana nis suala la kuvunjwa kwa katiba. Ushahidi upo mwingi tu kuonyesha Bunge ni taasisi inayoendekeza ubaguzi. Ukianzia na suala la Tundu Lissu ambapo Spika alilidanganya Bunge kuwa Tundu Lissu ni mshtakiwa wa mauaji. Kuna suala la kufikishwa kwa ushahidi wa Zitto Kabwe. Kuna suala la ushahidi kuhusu uongo wa Waziri Mkuu kuhusu mauaji ya Arusha hadi Lemma amepoteza ubunge.

  CHADEMA wakienda mahakamani tutakuwa tumenyoosha adabu kwamba katiba si ya kuchezewachezewa kwa dhana ya kwamba kuna chama kina wabunge wengi na kinaweza kujivunia hilo kwa kudhani kiko juu ya katiba kwa sababu Rais, Spika, Naibu Spika wanatoka chama hicho.

  Ninaamini wanasheria mliomo humu JF na kokote mnalijua hili kunizidi.

  CHADEMA mkishindwa hapa basi inabidi watu tufungue macho na kuwakamia nyinyi wala si Anne Makinda au Job Ndugai. Mara nyingi mmekuwa mkitutangazia magazetini kuhusu upendeleo wa Spika na mnamuacha hivyohivyo wakati uwezo uko mikononi mwenu.

  Mwaka jana Tundu Lissu alitutangazia kuwa amempeleka Spika Anne Makinda kwenye Kamati ya Kanuni za Bunge baada ya kuzuia swali lake kwa kisingizio kwamba ana kesi Mahakamani wakati Tundu Lissu hakuwa na kesi ya mauaji ya Tarime. Tukasubiri kwa hamu matokeo ya kesi ile maana tulijua hapa ndipo Spika Anne Makinda angekiona cha moto maana ushahidi wa hili ilikuwa wazi na asingekwepa kibano kile.

  Lakini kwa mshangao wa watu kama mimi hadi leo hakuna lolote kuhusu suala lile kana kwamba Kamati ya Kanuni za Bunge haikumjadili Spika Makinda kwa kumpendelea Waziri Mkuu na kumzuia Tundu Lissu kujibu swali.

  Hivyo ndivyo ninaona dawa inaweza kupatikana kwa masuala haya kwani tumechoshwa na marudio ya haya mambo.
   
 2. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #2
  Jul 12, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Mkuu katiba hiyo hiyo inasemaje kuhusu kuingilia mhimili mwingine? I mean Bunge VS Mahakama?
   
 3. m

  mob JF-Expert Member

  #3
  Jul 12, 2012
  Joined: Dec 4, 2009
  Messages: 2,028
  Likes Received: 511
  Trophy Points: 280
  mkuu umenena ninachokiona wanapendeleana wakiamini na sisi huku hatujui mambo ila inabidi waelewe watanzania wa leo sio wa mwaka 67
   
 4. N

  Nikupateje JF-Expert Member

  #4
  Jul 12, 2012
  Joined: Dec 22, 2009
  Messages: 1,314
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Mkuu POMPO,

  Neno "Mhimili" halimo ndani ya Katiba.

  Tusirefushe thread wakati nimeshaeleza ndani ya post yangu kwamba Maamuzi ya mashauri ya kikatiba ni mahakamani.

  Nikaonyesha jinsi kesi ya Augustine Lyatonga Mrema akiwa mbunge wa Temeka, ilivyokubaliwa Mahakamani na akashindwa kwa msingi wa kushindwa kujieleza Mahakamani lakini si kwa msingi wa case kukataliwa kwa sababu ya neno "Mhimili".
   
 5. b

  buyegiboseba JF-Expert Member

  #5
  Jul 12, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 535
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tusubiri kwanza maamuzi ya hiyo kamati ndo tutajadili hiki ulichokipendekeza
   
 6. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #6
  Jul 12, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Hivi na ile KESI ya kupinga uteuzi wa Wabunge wa East Africa imefikiwa wapi?

  Maana CCM kwa wingi wao walipindisha sheria za utezi wa wabunge hao.
   
 7. a

  aduwilly JF-Expert Member

  #7
  Jul 12, 2012
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 1,182
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Unadhani MAHAKAMANI ndo kupo salama, ubaguzi ni kila pala kaka, we kamua zako ugali tu cku ziende ungojee kifo tu, ukitaka haki duniani unajipotezea muda tu kwani hutaipata popote pale
   
 8. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #8
  Jul 12, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,280
  Trophy Points: 280
  Nitarudi hapa.
   
 9. G

  Gulwa JF-Expert Member

  #9
  Jul 12, 2012
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 2,797
  Likes Received: 1,973
  Trophy Points: 280
  Mahakama zetu zinaaminika? Majaji wetu niwaadilifu kiasi gani? Je uteuzi wao si wa kisiasa zaidi? Tafakari
   
 10. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #10
  Jul 12, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Nimekusoma mkuu, ila mahakam zetu si unazijua? altenative ni NGUVU YA UMMA tu ifanye kazi
   
 11. Makala Jr

  Makala Jr JF-Expert Member

  #11
  Jul 12, 2012
  Joined: Aug 25, 2011
  Messages: 3,397
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Ni suala la msingi sana,hata leo hii mi sijamwelewe J.Ndugai. Anadai ushahidi haujajitosheleza kwani amejadili na nini? Je,yeye anajua nini kuhusu EPA? Yeye anao ukweli kadiri gani kuhusu EPA na anawaambia nini Watanzania?
   
 12. Ukwaju

  Ukwaju JF Bronze Member

  #12
  Jul 12, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 8,287
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Jamaa yangu mbona umetutoa kwenye utamu unatuleta huku ambako siko (tuanchokifuata ni kweli MWIGULU kamsamehe MNYIKA? basi)
  Haya mambo unayoyaleta kabisa hayaingiliani na Mihimili mitatu
  Nakuuliza ni nani anayelivunja Bunge na wote wakarudi majimboni kuomba kura upya?
  usiwape wasomaji habari za uchochezi, eti waende mahakamani wakashtakiwe Anne na Job
  turudishe kwenye mada
   
 13. k

  kimeloki JF-Expert Member

  #13
  Jul 12, 2012
  Joined: Jul 9, 2012
  Messages: 1,932
  Likes Received: 957
  Trophy Points: 280
  Kiti cha spika inawayawaya.
   
 14. JamboJema

  JamboJema JF-Expert Member

  #14
  Jul 12, 2012
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,148
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Double starndard ipo na inategemewa. Ninachowasihi hawa jamaa ni kuwa makini na 'actions' zao dhidi ya CDM...wanawapaisha bila kujijua. Kwa sasa ilivyo, hata kama Mnyika kawasilisha ushahidi 'nyanya' vipi, jamii itaamini anaonewa kama ilivyofanyika kwa Zitto alipomtuhumu Karamagi.
  Ni huyu huyu Ndungai alimtoa nje Lisu eti kwa kuwasha 'mic'. Alipobanwa kuwa hakuna kifungu kinachosema hilo ni kosa akabadilika...... Ni aibu tupu. Wanatakiwa wawe na weledi zaidi kupambana na CDm ili CDM waonekane 'malimbukeni' lakini kwa mwendo huu watashangaa wanabaki wenyewe!
   
 15. N

  Nikupateje JF-Expert Member

  #15
  Jul 12, 2012
  Joined: Dec 22, 2009
  Messages: 1,314
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Unapotafakari kuhusu imani kuhusu mahakama zetu usiache kutafakari hukumu ya kesi ya Ubunge ya John Mnyika iliyofunguliwa na Hawa Ng'umbi.

  Usisahau pia hukumu kesi ya Oscar Mukasa wa CCM kupinga ubunge wa Dr. Mbasa wana-CHADEMA mbunge wa Biharamuro.
   
 16. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #16
  Jul 12, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Mahakama gani wataenda kila siku wanasema hawana imani na mahakama. na polisi.
   
 17. N

  Nikupateje JF-Expert Member

  #17
  Jul 12, 2012
  Joined: Dec 22, 2009
  Messages: 1,314
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Mkuu sikiliza,

  Inawezekana aliyeanzisha ile thread alituma wakati nina-edit hii yangu. Lakini nimesoma thread yake sielewi kwa nini ameamua kuongopa kwani nimesikiliza Mwigulu tangu wakati anaomba mwongozo na sikusikia maneno ya kusamehe.

  Hivyo, thread ile ama mleta mada alikurupuka ama amedhamiria kupotosha kilichoelezwa.


  Suala la kuvunja Bunge hilo si mada yangu. Tusirefushe thread kwa kuleta hoja ambazo mngeweza kuanzisha thread nyingine ingekuwa ni efficient step.
   
 18. N

  Nikupateje JF-Expert Member

  #18
  Jul 12, 2012
  Joined: Dec 22, 2009
  Messages: 1,314
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Maadam hukanushi hoja zangu basi nakukaribisha kwa mara ya kwanza umekubaliana na hoja yangu.
  Sijatamka neno "Polisi" kwenye thread yangu.

  Na zaidi, kwa sababu hoja zenu zimeanza kujirudia soma post namba 15 hapo juu nilivyomjibu mwenzako.
   
 19. Biohazard

  Biohazard JF-Expert Member

  #19
  Jul 12, 2012
  Joined: Aug 21, 2011
  Messages: 2,002
  Likes Received: 287
  Trophy Points: 180
  HApo umenena mkuu
   
 20. N

  Nikupateje JF-Expert Member

  #20
  Jul 12, 2012
  Joined: Dec 22, 2009
  Messages: 1,314
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160


  Mkuu buyegiboseba,

  Nakubaliana na wewe. Ndiyo maana nimeleta thread kiasi kwamba wenye mawazo kama wewe muweze kuiboresha na pia mtumie muda wenu kuwaelimisha kama wenzako hapo juu ambao wanaleta kesi ya ubunge wa East Africa ambapo tukiishia kutaja kesi basi tutataja nyingi na mimi nimetaja ya Mrema nikidhani ilikuwa ni rahisi kueleweka.
   
Loading...