JOHN MNYIKA: Msimamo wangu wa sasa juu ya Kauli yangu bungeni!

Hapa Jf pia kuna kanuni ni wangapi mods kawabani kwa sababu za kukiuka kanuni? jaribu kutoa lugha iliyokatazwa hapa Jf kama hujapata rungu la mods

Kwanza tukielewe kifungu kilichotoa adhabu kwa mnyika
 
kwa uzoefu wangu hapa wote mpo sahihi, wewe uliyesema raisi dhaifu na huyo aliyesoma kifungu cha kukutoa nje....
 
  • Thanks
Reactions: FJM
habari ndo hiyo...hivo ndivo tulivoelewa toka kitambo..sema naibu spika kaingiza siasa kama kawaida yake...haiwezekani kuzikalia kimya kauli walizotoa wabunge wa chama chake toka jana za kuwaita wabunge wa upinzani machizi wana pepo na leo kashabikia kauli za kibajaji lusinde bila kuwawajibisha then inatoka kauli ya mnyika inakua isue...?? siasa zinaliangamiza taifa letu...ccm siowazalendo....
 
Kuja kutoa ufafanuzi nje ya mbunge haisaidii Mnyika angekiokoa chama chake kwa kutoa maneno ambayo yamepelekea adhabu
 
sawa ni bora isipite bunge livunjwe na uchaguzi uitishwe ccm itoke madarakani aina faida na cc hata kidogo
 
Majebere, Mnyika hajachafua hali ya hewa. Ukweli ni kwamba Rais Kikwete ni dhaifu, ametuletea Bajeti DHAIFU!

Tuna MSIMAMO.

Inawezekana Rais ni dhaifu lakini spika anasema hiyo siyo lugha ya kibunge labda kama atakwenda kusemea mtaani ( nje ya mbunge) kwani bungeni anabanwa na kanuni
 
Sasa mbona anaomba apewe nafasi ya kujitetea? Kama sio woga huo ni nini?

Haki ya kujitetea (kujieleza) ni ya Kikatiba. Si woga kudai haki yako. Naibu Spika hakumtendea haki. Usipindishe maneno. Mnyika hakuomba kujitetea, amedai kupewa nafasi hiyo. Kama angekuwa mwoga, basi angefuta kauli yake.
 
Majebere, Mnyika hajachafua hali ya hewa. Ukweli ni kwamba Rais Kikwete ni dhaifu, ametuletea Bajeti DHAIFU!

Tuna MSIMAMO.
Sasa hivi yuko chooni na Ipad yake, amepata tumbo la kuhara ghafla. Lazima atambua kuwa hata kwenye kuropoka lazima utumie akili.
 
Nitatoa tamko la kina baadae kuhusu kilichotokea lakini kwa ufupi ubovu wa bajeti hii ni matokeo ya udhaifu wa Rais Kikwete, yeye ndiye aliyesaini Mpango wa Taifa wa miaka mitano kama Kiongozi Mkuu wa Nchi tena kwa wino mwekundu kama Amiri Jeshi Mkuu. Na yeye ndiye Mwenyekiti wa baraza la mawaziri, bajeti hii iliyoacha kuzingatia mpango wa Taifa imepita kwenye baraza alilloliongoza, pia kushindwa kutekelezwa kwa bajeti iliyopita ni matokeo pia ya udhaifu wa taasisi ya Urais.

Pia kwa mujibu wa Katiba Rais ndiye ambaye anapeleka bajeti bungeni, Waziri mwenye dhamana anapeleka tu kwa niaba. Rais amepewa mamlaka makubwa juu ya bajeti ibara ya 99 imeweka mipaka kuhusu mambo ambayo bunge lina mamlaka nayo huku ibara ya 90 inasema bunge likikataa bajeti rais ana mamlaka ya kuvunja bunge. Hivyo Rais Kikwete anapaswa kuagiza Waziri wa Fedha bajeti iondolewe irudi kwenye baraza la mawaziri ikafanyiwe marekebisho!

John Mnyika
19 Juni 2012

Hili baraza la JK liliwahi pikwa kuleeee Ngurdoto,, Walipikwa kuja kuiba au kutetea raslimali za Taifaaa??? nyambaf
 
Ameshaanza kujitetea, hii ndio faida ya kuropoka. Sasa woga wa nini wakati umesha chafua hali ya hewa?

Majebere!

Ivi kweli unatizama bunge au unasubiria tuu watu waandike humu ndani mwa jamii forum then nawe uchangie period au???? ungelishuhudia then ungeongea vyema nadhani. kumwita kiongozi JK kuwa ni dhaifu ni kauli chafu? au twaitafisili vibayaaa ina maana rais hana mapungufu yake kiutendaji? tuyaache ya kibinadamu basi

Mfano JK alikuwa nchi za ulaya 2007 akaulizwa na waandishi wa habari kwanini nchi yako ni maskini? wakumbuka jibu? ni alijibu sijui mpaka sasa kanini ni maskini? sasa hebu tupe tathimini yako kwa hilo jibu la rais tena ni kwa ajili ya manufaa ya wote watanzania.

My Take:

Rais wetu either anakuwa na majibu jeuri ya makusudi au haijui vyema nchi anayo iongoza


 
Back
Top Bottom