JOHN MNYIKA: Msimamo wangu wa sasa juu ya Kauli yangu bungeni! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JOHN MNYIKA: Msimamo wangu wa sasa juu ya Kauli yangu bungeni!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kiganyi, Jun 19, 2012.

 1. Kiganyi

  Kiganyi JF-Expert Member

  #1
  Jun 19, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 1,244
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nitatoa tamko la kina baadae kuhusu kilichotokea lakini kwa ufupi ubovu wa bajeti hii ni matokeo ya udhaifu wa Rais Kikwete, yeye ndiye aliyesaini Mpango wa Taifa wa miaka mitano kama Kiongozi Mkuu wa Nchi tena kwa wino mwekundu kama Amiri Jeshi Mkuu.

  Na yeye ndiye Mwenyekiti wa baraza la mawaziri, bajeti hii iliyoacha kuzingatia mpango wa Taifa imepita kwenye baraza alilloliongoza, pia kushindwa kutekelezwa kwa bajeti iliyopita ni matokeo pia ya udhaifu wa taasisi ya Urais.

  Pia kwa mujibu wa Katiba Rais ndiye ambaye anapeleka bajeti bungeni, Waziri mwenye dhamana anapeleka tu kwa niaba.

  Rais amepewa mamlaka makubwa juu ya bajeti ibara ya 99 imeweka mipaka kuhusu mambo ambayo bunge lina mamlaka nayo huku ibara ya 90 inasema bunge likikataa bajeti rais ana mamlaka ya kuvunja bunge.

  Hivyo Rais Kikwete anapaswa kuagiza Waziri wa Fedha bajeti iondolewe irudi kwenye baraza la mawaziri ikafanyiwe marekebisho!

  John Mnyika
  19 Juni 2012
   
 2. K

  Kyatsvapi JF-Expert Member

  #2
  Jun 19, 2012
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 305
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Haya mkuu.

  Tunaisubiria hiyo baadaye kwa hamu. utujuze zaidi...

  Pamox
   
 3. m

  majebere JF-Expert Member

  #3
  Jun 19, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 4,329
  Likes Received: 331
  Trophy Points: 180
  Ameshaanza kujitetea, hii ndio faida ya kuropoka. Sasa woga wa nini wakati umesha chafua hali ya hewa?
   
 4. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #4
  Jun 19, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 13,002
  Likes Received: 5,885
  Trophy Points: 280
  uko sahihi, usiogope sura ya yeyote. CCM NI UPUUZI!!!!!
   
 5. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #5
  Jun 19, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,971
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Kanuni za bunge ziko wazi kama wabunge wanataka mabadiliko ni bora wakaanza na kanuni badala ya kumlaumu spika ambaye amesoma kifungu cha adhabu ambacho kiko wazi.

  Inawezekana itikadi za CCM na chadema zikatupeleka kwenye malumbano lakini ukweli uko wazi Mnyika alikuwa na nafasi moja tu ya haraka ya kuondoa maneno yake ili kifungu cha 64 (b) cha kanuni za bunge kisimwangukie.
   
 6. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #6
  Jun 19, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mnyika hajakosea.
   
 7. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #7
  Jun 19, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 13,002
  Likes Received: 5,885
  Trophy Points: 280
  Kama vipi andaa mdahalo na wananchi/wasomi wa taasisi yoyote kuujadili udhifu wa jk.
   
 8. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #8
  Jun 19, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 24,925
  Likes Received: 1,982
  Trophy Points: 280
  Tunasubiri tamko udhaifu wa kikwete ndio umetufikisha hapa,haujakosea kabisa hakuna kufuta kauli hata kidogo udhaifu(weakness) sio tusi!! Mbona kwenye interview tunaulizwa,what are your strength and weakness? Kikwete asiwe na weakness kwani ye ni malaika?
   
 9. TWIZAMALLYA

  TWIZAMALLYA JF-Expert Member

  #9
  Jun 19, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 399
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  We trust you
   
 10. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #10
  Jun 19, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 12,810
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Lakini Mnyika si mnajua namna nyie CHADEMA mnavyochangia kwenye udhaifu wa Rais wetu? au mnajitoa akili, nyie ndio chanzo cha matatizo yote haya.
   
 11. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #11
  Jun 19, 2012
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,353
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  yawezekana hata hizo kanuni huzifahamu.
   
 12. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #12
  Jun 19, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,971
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Hata spika hajakosea kasoma kifungu kilichotoa adhabu kiko wazi
   
 13. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #13
  Jun 19, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,563
  Likes Received: 785
  Trophy Points: 280
  ch*izi
   
 14. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #14
  Jun 19, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,971
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  unayezifahamu tufundishe ambao hatuzijui
   
 15. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #15
  Jun 19, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 24,925
  Likes Received: 1,982
  Trophy Points: 280
  Acha kuarisha kwenye sredi za watu,wewe una guts za kumwambia spika sifuti kauli?
   
 16. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #16
  Jun 19, 2012
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,353
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0

  na lile la kuwaambia walioiba fedha za EPA warudishe alishauriwa na CDM?
   
 17. Wingu

  Wingu JF-Expert Member

  #17
  Jun 19, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,326
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Kumbe wewe ndo mnyika sawa kiganyi
   
 18. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #18
  Jun 19, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 20,629
  Likes Received: 3,128
  Trophy Points: 280
  Wow.....:flame:
   
 19. E

  ESAM JF-Expert Member

  #19
  Jun 19, 2012
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 963
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  Safi sana dogo wangu waingize darasani maghamba
   
 20. MAFILILI

  MAFILILI JF-Expert Member

  #20
  Jun 19, 2012
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 1,847
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  Huo ni msimamo wa chama au wako binafsi. Kwa nini Zito yuko tofauti nawe juu ya msimamo wako wa kumsuta Rais
   
Loading...