John Mnyika: Mambo CHADEMA tuliyozungumza na wenzetu wa CCM

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,269
Mkutano ule wa Mei 20,2022 ,ni mwanzo wa mazungumzo ya timu mbili. Upande wetu CHADEMA tuliwasilisha ajenda mbili ya kwanza ni kurejeshwa kwa mchakato wa katiba ya nchi yetu na ya pili ni kujadili madhara ya miaka sita iliyogubikwa na ukiukwaji wa haki

Itakumbukwa Aprili 07, 2021 Mwenyekiti Freeman Mbowe alimuandikia barua Rais Suluhu Samia, pamoja na mambo mengine alimweleza haja ya kufungua ukurasa mpya wa maridhiano na haki katika Taifa letu kupitia mazungumzo, pia akawasilisha ombi la CHADEMA kukutana naye Rais

CHADEMA na wananchi wengi tunaamini kuwa katiba mpya ni nyenzo ya kilipelekea Taifa letu mbele na kufungua ukurasa mpya wa kimfumo na kitaasisi katika nchi yetu, katika mkutano wetu Ikulu Dodoma tulitoa mapendekezo yetu ya jinsi yakukwamua mchakato wa katiba mpya

Tumependekeza iundwe Tume ya Ukweli na Upatanishi itakayoshughulikia madhara ya watu walioumizwa ndani ta miaka iliyopita 6, pia tulipendekeza madhara yaliyotokea katika uchaguzi wa mwaka 2019 na 2020 yashughulikiwe na kuhakikisha chaguzi zijazo zinakuwa huru na haki

Kwa miaka sita ofisi ya msajili wa vyama vya siasa, imepandikiza migogoro kwenye vyama takribani vitano, natoa wito kwa mamlaka husika kuchunguza mwenendo wa ofisi ya msajili wa vyama vya siasa na kumchukulia hatua msajili wa vyama vya siasa

Mambo mengine tuliyojadili ni kutaka kufutwa kwa kesi za kisiasa na kuachiwa kwa wafungwa wa kisiasa, uhuru wa vyama vya siasa kufanya shughuli zake ikiwemo mikutano ya siasa, kufuta sheria kandamizi nchini kwetu, kufuatilia watu walioshughulikiwa kupotea au kuuawa

Jambo lingine tuliloongea ni juu ya hakikisho la usalama kwa viongozi wetu ambao kwa sasa ni wakimbizi katika nchi nyingine, kuondolewa bungeni kwa waliokuwa wanachama wetu 19

Mwanzo huu wa mazungumzo, utafuatiwa na hatua nyingine za mazungumzo, ombi langu kwa wana-CHADEMA na Watanzania kuendelea kuwa watulivu na wavumilivu katika hatua hizi zilizoanza, kwa sababu mchakato wa mazungumzo, kujenga maridhiano na mwafaka sio tukio la siku moja

Hatma ya nchi hii, haiko kwa CCM na CHADEMA pekee hususan katika suala muhimu kama katiba, hatua kwa hatua umma utashirikishwa lengo likiwa ni kufika mwaka 2025 tukiwa na katiba mpya

Watanzania wanapaswa kufahamu kwamba Katika mazungumzo yote, tutatanguliza maslahi ya Taifa na si kitu kingine. BRAVO
 
Upinzani wa bongo kwishney, wao walidhani mwendazake ndio atakaeua upinzani kumbe mama ndio anauua mazima. hamna upinzani bongo na nimegundua NJAA iliopo kwa viongozi wa upinzani ndio chimbuko la kutokuwepo huo upinzani. Twende mbele turudi nyuma, Kenya ina upinzani imara kwa kua waliopo upinzani wana fwedha na serikali haina uwezo wa kuwanunua, sio bongo njaa tupu wapinzani wanaangalia matumbo yao na familia zao...
 
Upinzani wa bongo kwishney, wao walidhani mwendazake ndio atakaeua upinzani kumbe mama ndio anauua mazima. hamna upinzani bongo na nimegundua NJAA iliopo kwa viongozi wa upinzani ndio chimbuko la kutokuwepo huo upinzani. Twende mbele turudi nyuma, Kenya ina upinzani imara kwa kua waliopo upinzani wana fwedha na serikali haina uwezo wa kuwanunua, sio bongo njaa tupu wapinzani wanaangalia matumbo yao na familia zao...
Kayafa Ltd
 
Bumbav, Chadema kwisha habari yao,

Mtarudi jukwaan humu kulialia ,tupo hapa
Mjane utaki kuamini kama Shetani Magufuli na Samia ni vitu viwili tofauti. Mnawaza ubaya tu legacy ya HAYAWANI.
Samia aliposema yeye na Magufuli ni kitu kimoja alitaka wajane mpate nguvu ya kuanua matanga. Umeshindwa kuelewa kwa kua akili yako haina akili.

Mtake msitake…
Katiba mpya ni lazima na ni sasa.
 
Back
Top Bottom