Kuna jambo ambalo naamini Chadema wanalisimamia ingawa sidhani kama wataweza ku achieve wanachoamini katika siku za karibuni.Pia naamini kuna jitihada behind the scene kulimaliza hili jambo bila kuonekana kuwa serikali ilkuwa na makosa!!Comred Mnyika mdogo wangu na Katibu Mkuu wa chama kikuu Cha upinzani CHADEMA tunataka tuuone utashi na hekima na busara zako katika kipindi hiki kigumu, chama chako kina Kariba kubwa ya vijana ambao bado wana mihemko.
Mkeka uliolalia umechanika Sana, usitumie nguvu kubwa utauchana zaidi. Maneno yako yawe na busara ya kiuongozi tunachotaka Mbowe aachiwe hayo mengine tunayoyasikia kwa vijana wenu mtayafanya akiishaachiwa.
Isingekuwa maneno yenu ambayo nasema yametokana na mihemko ya vijana wenu huenda krismass hii Mbowe tungekuwa nae.
Ukiwa na njaa usichague mkono utakaokulisha kula ili ushibe mengine yatafuata. Kumshambulia Zitto na Rais Samia kumerudisha nyuma mchakato wa kumtoa Mbowe hata mamlaka zinaweza kuhisi mna kiburi.
Mjumbe hauawi.
Ikiwa serikali inaweza kufanya maamuzi kwa mihemko ya "machizi" then hiyo serikali ijitathmini