John Mnyika: Hatutoi sasa majina ya walioficha fedha Uswisi

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,296
2,000
mnyika.jpg
MBUNGE wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika (Chadema) amesema licha ya kuwa na orodha ya vigogo walioficha fedha Uswiss, lakini hawezi kutoa orodha ya majina hayo kama Serikali inavyotaka kwa vile orodha ya vinara wa ufisadi ambayo ilitajwa Mwembe Yanga bado haijashughulikiwa.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Sahara jijini Mwanza, Mnyika alisema kwamba kama Serikali ya CCM inasisitiza kutaka majina ya walioficha fedha huko Uswiss yatajwe, wanapaswa kusimama na kueleza ile orodha ya mafisadi ambayo Chadema waliitaja pale Mwembe Yanga imefanyiwa kazi gani.

"Watu wanapotutaka tutaje majina, na sisi tunawambia kwanza wasimame na kutueleza ile ‘list' (orodha) ya mafisadi ambayo tuliitaja kwa majina wameishughulikia vipi?" alihoji Mnyika na kuongeza kwamba wanajua jinsi ambavyo CCM wanalivyonufaika na ufisadi kupitia Kampuni ya Kagoda jambo ambalo linadhihirisha kuwa haiwezi kuwa rahisi kwao kushughulika na vita ya ufisadi.

Alisisitiza kuwa wanaotaka majina yatajwe wanayo ajenda yao na wao wameshaifahamu hivyo hawatashughulika nayo na kusema ukifika wakati ambao wao wanautambua wataweka kila kitu nje, lakini siyo kwa kushinikizwa na Serikali ya CCM.

"Tunajua serikali hii inayoundwa na Chama Cha Mapinduzi haina dhamira ya kushughulika na ufisadi, na hili ndilo litakalowaondoa madarakani," alifafanua.

Hata hivyo mkutano huo uliingia dosari wakati Mnyika akiendelea kuhutubia ambapo mawe yalianza kurushwa na vijana wanaodaiwa kuwa ni vijana wa Diwani wa Kata ya Kitangiri kwa tiketi ya Chadema, Henry Matata aliyevuliwa uanachama.

Kutokana hali hiyo vijana wa Chadema walizungumza katika maeneo mbalimbali na kufanikiwa kuwanasa vijana wawili ambao walishambuliwa na kueleza na kunusuriwa na Mbunge wa Nyamagana Ezekiel Wenje aliyeita polisi na kuwaomba waache kuwashambulia.


Awali akizungumza katika mkutano huo Mbunge wa Jimbo la Nyamagana,Wenje alieleza wananchi kuwa katika mkakati wake wa kuboresha elimu ya msingi na sekondari amefanikiwa kutengeneza madawati mengine 400 baada ya madawati ya awali 500 kugawiwa katika shule.

Alisema madawati hayo yatagawanywa kwa shule 30 za wilaya ya Nyamagana na kubainisha kwamba kutokana na madaati ya awali 500 kutolewa bila utaratibu na Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza,Wilson Kabwe hivyo madawati haya alieleza kuwa yatasambazwa na madiwani wa Chadema katika shule pamoja na katibu wa ofisi yake ili kuhakikisha yanafika katika shule husika iliyopangwa.

Mwananchi
 

Ritz

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
43,121
2,000
Kwa hiyo hayo majina ni siri Chadema bana kila kitu siri. Dr Slaa alisema anataka kuuliwa na usalama wa taifa majina ya wana usalama ni siri yake. Mnyika naye kaja na sarakasi zile zile.
 

2hery

JF-Expert Member
May 27, 2011
4,701
2,000
acheni kumwiga rubani wa ndege aliye sema anawafahamu wauza unga kwa majina lakini mpaka leo hatuoni chochote.katika hili tumeshuhudia tu kifo cha Amina Chifupa kwa kudandia hoja.
 

Kimbunga

Platinum Member
Oct 4, 2007
14,862
2,000
MBUNGE wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika (Chadema) amesema licha ya kuwa na orodha ya vigogo walioficha fedha Uswiss, lakini hawezi kutoa orodha ya majina hayo kama Serikali inavyotaka kwa vile orodha ya vinara wa ufisadi ambayo ilitajwa Mwembe Yanga bado haijashughulikiwa.

Mkuu Mnyika hapo kwenye wekundu: Ile list of shame haijashughulikiwa kweli? Unataka ishughulikiwe na nani? Mimi nina hakika kabisa wananchi kwa umoja wao wameishughulikia ile list of shame ambayo ilitajwa.

Mbona ushahidi wa kushughulikiwa kwao uko wazi kabisa. Wengine hadi wamejiondoa kwenye siasa kwa kelele za wakulima, wakwezi, wawindaji na wafanyakazi. Huoni kwamba kutajwa kwa ile list kuliisaidia CDM kufika hapo ilipo?

Watajeni kama mna majinayao na kama serikali haitawashughulikia basi wananchi watawashughulikia.
 

Kimbunga

Platinum Member
Oct 4, 2007
14,862
2,000
Kwa hiyo hayo majina ni siri Chadema bana kila kitu siri. Dr Slaa alisema anataka kuuliwa na usalama wa taifa majina ya wana usalama ni siri yake. Mnyika naye kaja na sarakasi zile zile.

Hivi hii hoja ni ya CDM au ya Mnyika ama ya Zitto?
 

Leak

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
49,626
2,000
Kweli kabisa maana tutaishia kuwajua kwa majina na hakuna kinacho fanyika! Yani wanavyo omba majina utafikiri hawayajui! Cccmweli wanafiki sana!
 

amkawewe

JF-Expert Member
Dec 9, 2011
2,024
1,195
Kula timing.

Subirini 2014/15 majina yatamwaga ili washughulikiwe wakati wa uchaguzi
 

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
39,081
2,000
Kwa hiyo hayo majina ni siri Chadema bana kila kitu siri. Dr Slaa alisema anataka kuuliwa na usalama wa taifa majina ya wana usalama ni siri yake. Mnyika naye kaja na sarakasi zile zile.

Kwani Dr.Slaa ni Kamanda Barlow mpaka muhangaike kutafuta wabaya wake..........wako wapi wanaCCM waliomjeruhi Machemli na Kamanda H.Kiwia
 

Mangimeli

JF-Expert Member
Sep 15, 2011
1,153
1,250
kutokushughulikiwa kwa oroza ya mafisadi ilyotajwa mwembe yanga sio suluhu ya nyie kutokutaja oroza ya walioficha hela urusi,kama majina mnayo tajeni watu wyaone na kuyasikia,vinginevyo hizo tunaziita bla bla za,kisiasa
 

Muke Ya Muzungu

JF-Expert Member
Jun 17, 2009
3,444
0
Strategically CDM should not name the Swiss account holders. Let this be a weapon to slash the corruption Kingpins in CCM for the next two years. Names these people A year to election so they can remain on defence. Keep a list of their dirty laundry based on gravity until them. in the meantimes, scrutinize on the regular issues
 

raymg

JF-Expert Member
Jun 30, 2012
843
195
Nakubaliana kabisa na Mnyika.....hii list ya majina ni silaha ya maangamizi ya 2015 kwa hiyo kuitumia saiz bado mapema sana, hivyo hakuna kuitaja mpaka mda mwafaka utakapofika!
 

meningitis

JF-Expert Member
Nov 17, 2010
8,351
2,000
Kwa hiyo hayo majina ni siri Chadema bana kila kitu siri. Dr Slaa alisema anataka kuuliwa na usalama wa taifa majina ya wana usalama ni siri yake. Mnyika naye kaja na sarakasi zile zile.

orodha hii ni siri mpaka 2015 katikati ya mwezi wa tisa
 

Pancras Suday

JF-Expert Member
Jun 24, 2011
7,862
2,000
Kwa hiyo hayo majina ni siri Chadema bana kila kitu siri. Dr Slaa alisema anataka kuuliwa na usalama wa taifa majina ya wana usalama ni siri yake. Mnyika naye kaja na sarakasi zile zile.
Kwani Mwakyembe si alitaja hadi majina ya wabaya wake kwani serikali na usalama wa taifa waliyafanyia nini? si huyu huyu Mwakyembe alikuja kufanyiwa nini baadae?
 

AdvocateFi

JF-Expert Member
Jan 15, 2012
11,492
2,000
Yes! Si muda wa kutoa majina sasa koz CCM wanayamendea ili wafanikishe malengo yao kibinafsi ktk makundi ya chama chao.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom