Lu-ma-ga
JF-Expert Member
- Sep 21, 2010
- 4,780
- 3,227
Sijui EU wataficha wapi misura yao.Walitaka Tanzania 🇹🇿 imwage damu.Sasa waje kujifunza siasa Tanzania 🇹🇿 na pia wajifunze kupambana na kaugonjwa ka Corona kalikowashindaChadema kususia bunge au kutotambua matokeo ya uchaguzi walioushiriki ni
1. Kuwadharau raia wa Tanzania 1.8m walio amka mapema Nov 28, 2020 kuwapigia kura. Kama ambavyo Lissu na Kabwe wamefanya. Kwa upande wa ACT ambayo siitofautishi na Maalim Seif ni kama Maalim hajataka kujifunza makosa aliyoyafanya 2015 kususia uchaguzi ambapo kwa hesabu za haraka kosa hilo limegharimu kwa kupata asilimia 19 ya kura visiwani tofauti na miaka iliyopita.
2. Kususia Bunge kwa CDM kungeikosesha sauti bungeni na ndio ungekuwa mwisho wake kama wangebaki kushikilia mawazo ya Lissu ambayo kisiasa yanakiua chama. Pia Chadema wangepoteza haki yao ya gawio la ruzuku kutoka Bungeni kwa miaka mitano mfululizo. Hii ingeathiri sana shughuli za chama nchi nzima na pia viongozi wa chama kukosa nguvu ya kimaamuzi hasa Mbowe. ( Huu ni mradi wake huo ndio ukweli) amewekeza sana so kufuata mawazo ya kina Lissu kungeiua biashara yake ambayo kwa namna yoyote Mbowe hawezi kuiacha (akakimbilia ughaibuni) ... Wakati Lissa anamahali pa kushikilia hana uchungu na uwekezaji wa Mbowe and Co. Na ndio sababu Mbowe alikuwa kimya anatafakari atoke vipi mtegoni.
Lissu alikitumia Chadema kumchafua Magufuli kwa kutumia tiketi ya urais (kwa ufadhili wa ulaya ....sina ushahidi ila natumia common sense) ambao kwa hakika alijua haupati ....ili adhima yake ya kuichafua serikali itimie rejea kampeni zake hakukuwa na kuzungumzia sera zaidi ya matusi kwa rais ya serikali yake... Na kwa kuthibitisha ufadhili wake ulitoka wapi umoja wa ulaya kupitia ubalozi wa Ujerumani ulimpa kinga ya kidiplomsia aweze kukimbia nchi.
3. Namshauri Maalim na Zitto kuepa Lissu's trap wakubali kushiriki serikali ya umoja wa kitaifa kule Zanzibar ili wasifutike kisiasa na ikiwezekana waipiku CDM ili wao wawe leading opposition party. Siasa ni kazi kama zilivyo kazi nyingine uki fail mbinu ya huku unahamia plan B kung'ang'ania mawazo ya Lissu, Fatma Karume na Lema ni kujimaliza. Kabudi alijua nini anachoongea na hakuna cha Sanction wala mdogo wake toka ulaya maana nguvu hiyo imemalizwa na CDM kukubali kurudi Bungeni.
Hongera Mbowe na Kongole viti maalum kwa kukwepa mtego wa Lissu.