John Mnyika awatembelea gerezani Viongozi wa CHADEMA waliofungwa Maisha huko Bariadi

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
116,496
215,338
FB_IMG_1657463806369.jpg


Leo Tarehe 10/07/2022 , Katibu Mkuu wa CHADEMA John Mnyika, amefika kwenye gereza la Bariadi kuwajulia hali Viongozi wa Kata ya Dutwa , Jimbo la Bariadi Waliofungwa kifungo cha Maisha Gerezani.

Wafungwa hao wa kisiasa KATALA KIKAJA na NG'ULIMA LILANGA , walibambikwa makosa ya Uongo ili kuwakomoa na ile Serikali ya Kikatili ya awamu ya 5 kwa vile Walikuwa viongozi wa Chadema , waliokataa siasa za kishamba za kuunga mkono Juhudi , zilizokuwa zinasimamiwa na kuratibiwa na Humphrey Polepole aliyekuwa Katibu wa Uenezi wa CCM , ukiacha aliyewatuma ambaye alikwishafariki , lakini Wahusika wote wa unyama huo bado wako hai na wanafahamika .

Hata hivyo Chadema imekwishakata Rufaa na tayari rufaa hiyo imepangwa kuanza kusikilizwa tarehe 20/07/2022

KILA UBAYA UTALIPWA .
 
"Waliofungwa maisha" uzito wa hiyo kauli haupimiki.

Ina maana hao viongozi wa Chadema ni sawa na wahaini, au wauaji.

Hebu basi hayo maridhiano yenu yarudishe tabasamu la haraka kwa familia za hao wafungwa, waachiwe huru.

Sijui kwanini inachukua muda mrefu sana kwa mambo ya msingi kama haya kumalizwa haraka.
 
CHADEMA Wana mbinu za hovyo za kisiasa, ona Sasa, hao wananchi wanaojifanya kuwapigania Wala hawana habari nao, watoto wao na wake zao wanaishi maisha ya shida.

Kila mtu atauchukua mzigo wake mwenyewe, CDM msijifanye mnamudu mizigo ya wengine
 
Leo Tarehe 10/07/2022 , Katibu Mkuu wa Chadema John Mnyika, amefika kwenye gereza la Bariadi kuwajulia hali Viongozi wa Kata ya Dutwa , Jimbo la Bariadi Waliofungwa kifungo cha Maisha Gerezani.

Wafungwa hao wa kisiasa KATALA KIKAJA na NG'ULIMA LILANGA , walibambikwa makosa ya Uongo ili kuwakomoa na ile serikali ya Kikatili ya awamu ya 5 kwa vile Walikuwa viongozi wa Chadema , waliokataa siasa za kishamba za kuunga mkono Juhudi , zilizokuwa zinasimamiwa na kuratibiwa na Humphrey Polepole aliyekuwa Katibu wa Uenezi wa CCM , ukiacha aliyewatuma ambaye alikwishafariki , lakini Wahusika wote wa unyama huo bado wako hai na wanafahamika .

Hata hivyo Chadema imekwisha kata Rufaa na tayari rufaa hiyo imepangwa kuanza kusikilizwa tarehe 20/07/2022

KILA UBAYA UTALIPWA .

Hiyo umevuruga; kubambikwa makosa ya uwongo siyo lugha sahihi inaondoa objectivity ya hoja yako. Kuna rufaa, na CHADEMA ina jopo la mawakili wazuri akina Kibatala na Lissu wangewakatia rufaa. Kufungwa maisha ni kosa kubwa sana, siyo la kubambikizwa kisiasa hata kidogo. Kama viongozi hao walifanya makosa ya kisheria, acha sheria ichukue mkondo wake. Viongozi wa mtaa siyo watu wa kuitisha serikali hadi iwapanie kiasi hicho; kwanza serikali siyo inayotoa hukumu, bali ni mahakama.
 
CDM Wana mbinu za hovyo za kisiasa, ona Sasa, hao wananchi wanaojifanya kuwapigania Wala hawana habari nao, watoto wao na wake zao wanaishi maisha ya shida.

Kila mtu atauchukua mzigo wake mwenyewe, CDM msijifanye mnamudu mizigo ya wengine
Hili Jambo hata Mimi linanipaga ukakasi sisi wananchi wabinafsi Sana ..hapa mitandaoni huwa tunajifanya mdomo mwingi na wamoja Ila uhalisia hakuna hiko kitu ndo maana watu wakipata matatizo tunawaacha peke yao.

NB:Waache wakina Halima Mdee watafune pesa maana sisi wananchi hatuna jema kwao.
 
24 Reactions
Reply
Back
Top Bottom