Etwege
JF-Expert Member
- Jul 4, 2018
- 5,701
- 15,149
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika amewataka viongozi wa chama hicho mkoani Simiyu kutokaa kimya badala yake wapaze sauti kueleza changamoto zinazowakabili wananchi.
Mnyika ametoa kauli hiyo leo alipokuwa akizindua Tawi la Chadema Lamadi wilayani Busega mkoani Simiyu huku akisema wajibu wa viongozi wa chama hicho ni kuikumbusha Serikali changamoto zinazowakabili wananchi wake.
"Tunapokabiliwa na matatizo ya kupanda kwa bei za bidhaa na mafuta usafiri na huduma nyingine za msingi zinazowagusa wananchi Chadema tuendelee kuwa sauti ya wananchi ili kutetea haki zao," amesema
Ameongeza; "Tunapokabiliwa na matatizo mbalimbali kwenye bei za pamba na mambo mengine Chadema iwe sauti katika kutetea wananchi. Tufanye majukumu ya chama lakini rai yangu kwenu pamoja na kupambania Katiba Mpya na Tume huru ya uchaguzi kazi ya kuwatetea wananchi endeleeni nayo," amesema Mnyika
Mnyika amesema Serikali itachukua hatua zinazoleta mabadiliko kwa jamii iwapo itakumbushwa majukumu yake jambo ambalo litafanikiwa iwapo viongozi hao wakitimiza wajibu wao.
Katibu wa Chadema Kanda ya Victoria, Zakaria Obadi amesema Chama hicho kimeandaa mpango wa kuwakutanisha wanachama wake ili kuwajengea uwezo wa kuwapambania wananchi.
"Tunaendelea kuandaa mpango wa kuwaandaa kuwasemea wananchi na kupaza sauti zenu kwa niaba ya wananchi," amesema Obadi