John Mnyika awaokoa Mawaziri wa JK wasiendelee kuzomewa kwenye mikutano ya CCM

Dr Matola PhD

JF-Expert Member
Oct 18, 2010
55,792
90,593
Kwa sababu ilichokisema Mnyika ni sahihi, basi sasa Mawaziri wamepata upenyo wa kuzikataa ziara za CCM kwamba sheria inawabana, hii ndio njia pekee ya wao kuepukana na zomea zomea.

Soma hapa hoja ya Mnyika......

[h=5]Balozi Sefue na Yambesi watoe kauli iwapo Serikali imetoa waraka wa maagizo kwa watumishi wa umma kutoa taarifa katika mikutano ya CCM kinyume cha maadili

Katibu Mkuu Mkuu Kiongozi (Ofisi ya Rais-Ikulu) Balozi Ombeni Sefue na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nchi (Ofisi ya Rais) Menejimenti ya Utumishi wa Umma George Yambesi watoe kauli kwa umma iwapo Serikali imetoa waraka mpya kwa watumishi wa umma kuhudhuria mikutano ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kutoa taarifa kama sehemu ya kazi zao kama walivyotakiwa na chama hicho katika tamko lake la tarehe 2 Disemba 2012.

Kwa sasa utumishi wa umma katika nchi yetu unaongozwa na Sheria ya Utumishi wa Umma na. 8 ya mwaka 2002 pamoja na marekebisho yake ya mwaka 2007 pamoja na kanuni za utumishi wa umma za mwaka 2003 kama zilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2009 na kanuni za maadili ya utendaji katika utumishi wa umma za mwaka 2005.

Itakumbukwa kwamba awali utumishi wa umma Tanzania ulikuwa ukiongozwa na Sheria ya Utumishi Serikalini namba 16 ya mwaka 1989 na Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma Toleo la 1994 pamoja na marekebisho yake. Kifungu cha 4(1) cha Sheria hiyo kilimpa mamlaka Mkuu wa Utumishi wa Umma, ambaye ni Katibu Mkuu kiongozi kutoa waraka kuhusu taratibu mbalimbali za utumishi wa umma.

Chini ya Mamlaka hayo, aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Martem Y.C. Lumbanga tarehe 26 Juni, 2000 alitoa Waraka wa Mkuu wa Utumishi wa Umma na. 1 wa mwaka 2000 wenye kumb. Na. SHC/C.180/2/113 uliohusu maadili ya Watumishi wa Umma katika mfumo wa vyama vingi vya siasa.

Waraka huo unawataka watumishi wa umma kutekeleza wajibu wao wa utumishi bila kufanya upendeleo wala ubaguzi wa chama chochote cha siasa. Waraka huo unawakataza watumishi wa umma kuzungumza na kutoa taarifa kwenye mikutano ya vyama vya siasa na haujatoa ruhusa kwa watumishi hao kuzungumza katika mikutano ya CCM pekee; hivyo Balozi Sefue na Yambesi wanapaswa kutoa kauli kwa umma iwapo Serikali imetoa waraka mwingine kwa siri wenye kuagiza watumishi wa umma kutoa taarifa katika mikutano ya CCM.

Izingatiwe kwamba kanuni za maadili ya utendaji katika utumishi wa umma hazielekezi watumishi wa umma kuwa na utii au kuwajibika kwa CCM bali zinaeleza kwamba watumishi wa umma watawajibika kwa umma na watakuwa na utii kwa Serikali na sio chama kinachotawala na zimeweka mipaka ya matumizi sahihi ya taarifa za kiserikali wanazowajibika kuzitoa kwa nafasi zao.

Izingatiwe kuwa mapendekezo ya Tume ya Nyalali ya mwaka 1991 na marekebisho ya Katiba ya mwaka 1992 kuingia katika mfumo wa vyama vingi na marekebisho ya sheria yaliyofuata yameweka uhuru wa watumishi wa umma katika kujiunga na vyama vya siasa (isipokuwa watumishi wa kada maalum) na mipaka ya mahusiano kati ya kazi zao za kiserikali na shughuli za vyama vya siasa kikiwemo chama kinachotawala.

Hivyo maagizo au waraka wenye kuwalazimisha watumishi wa umma kuhudhuria mikutano ya CCM na kutoa kutoa taarifa ni kinyume cha uhuru wa kikatiba, sheria za nchi, kanuni za utumishi wa umma na misingi ya utawala bora.

Imetolewa na:
John Mnyika (Mb)
Mkurugenzi wa Habari na Uenezi
[/h]
 
hahahahaaa kweli bhana amewaokoa, wamepata pa kusimamimia maana inaoneka waliotumwa(Mawaziri) na aliyewatuma (Kaka Alfani) wote hawajui hizo Nyaraka ambazo waliziandaa wenyewe...............
 
Kichwa cha habari cha huu uzi na kilichoandikiwa ndani ni vitu viwili tofauti. Thread kama hizi zinaitwa "rukurunguru au kamchape"
 
Naamini nchi hii ina sheria, kanuni na taratibu nzuri sana lakini kwasasbabu ya ufyatu na ukilaza wa viongozi tulionao hawazifuati au hawazifahamu kabisa.
 
Kichwa cha habari cha huu uzi na kilichoandikiwa ndani ni vitu viwili tofauti. Thread kama hizi zinaitwa "rukurunguru au kamchape"
67886_10200250819699472_671353626_n.jpg
 
CDM wameanza kuogopa hizi ziara za mawazir naamini ndo wakatafuta njia za kuzuia laiti wangekuwa hayo yakuzomewa wanafanyiwa kweli hao mawaziri basi CDM wangetumia kama nafasi ya kuiondosha CCM,lakini ni kinyume chake

Kwa bahati mbaya wameona nguvu ya Mawaziri ni kubwa wanaona bora wajipange hahahaha

Wazee wa muongozo hadi uku munataka muongozo?
 
CDM wameanza kuogopa hizi ziara za mawazir naamini ndo wakatafuta njia za kuzuia laiti wangekuwa hayo yakuzomewa wanafanyiwa kweli hao mawaziri basi CDM wangetumia kama nafasi ya kuiondosha CCM,lakini ni kinyume chake

Kwa bahati mbaya wameona nguvu ya Mawaziri ni kubwa wanaona bora wajipange hahahaha

Wazee wa muongozo hadi uku munataka muongozo?
chadema tunaheshimu kanuni, taratibu na sheria however crazy they look kwa sababu tunajiandaa kuwa chama tawala makini.
tunataka utaratubu wa kanuni ufwatwe.
Nimeamini
John Mnyika ni mbunge makini sana.
 
Last edited by a moderator:
Kichwa cha habari cha huu uzi na kilichoandikiwa ndani ni vitu viwili tofauti. Thread kama hizi zinaitwa "rukurunguru au kamchape"

Tofauti yake ni nini kilichozungumziwa hapa ni sheria za utumishi wa Umma na mawaziri ni watumishi hivyo kujihusisha katika Ziara za Kinana na Nape ni makosa na wamekuwa wakizomewa sana katika ziara hizo hivyo kwa ufafanuzi wa sheria hii watakuwa wameepukana na kuongozana na akina Nape. kwa hiyo heading haina makosa
 
Hapo ndo unapojua umakini wa Viongozi. Nape hajawah kuongea jambo la maana toka amepewa cheo.

hakuna kitu kibaya kama hujielewi,nape anapaswa kuangalia alama za nyakati,na upepo unakoenda,wale wanaomshabikia wanapata maslahi kwa nape,mtanzania wa leo si wa jana
 
Kichwa cha habari cha huu uzi na kilichoandikiwa ndani ni vitu viwili tofauti. Thread kama hizi zinaitwa "rukurunguru au kamchape"

umepata darasa huru la bure na magamba wengine.Ndipo utaona magamba hayafikilii.Itakuwaje mkuu wa magamba hajui hizo sheria,kanuni na taratibu? Au ndo mambo yenu ya kuwa wasaidizi wake wanamwangusha? Mi niseme hivi,farasi na mpanda farasi wakitumbukia mtoni mjinga ni mpanda farasi
 
CDM wameanza kuogopa hizi ziara za mawazir naamini ndo wakatafuta njia za kuzuia laiti wangekuwa hayo yakuzomewa wanafanyiwa kweli hao mawaziri basi CDM wangetumia kama nafasi ya kuiondosha CCM,lakini ni kinyume chake

Kwa bahati mbaya wameona nguvu ya Mawaziri ni kubwa wanaona bora wajipange hahahaha

Wazee wa muongozo hadi uku munataka muongozo?

we ndo umetoka milembe juzi au? Umeambiwa walikuwa wanazomewa kwa sababu wananchi wanajua kuwa wanatumia kodi zetu hovyo.Isitoshe huo ni uamuzi wa kipuuzi uliofikiwa na dhaifu na kundi lake. Waswahil wanasema 'chema cha jiuza kibaya cha jitembeza' wanachofanya chama cha magamba ni kujitembeza kwa sababu hawauziki.Mambo mema si huwa yanaonekana hauhitaji kutafuta darubini ili kuyaona
 
Safi sana J.J. Mnyika kwa kuwakumbusha sheria hao vilaza kina Nape! Kazi yao kukurupuka tu na kupanga mikakati ya kummaliza Dr Slaa kila siku.Tangu Nape apewe cheo sijawahi kumsikia akiongea point, hiyo ni kutokana na kusoma hadithi za shigongo halafu anazifanyia kazi kwenye chama ndio maana chama kimekufa bado mazishi tu.
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom