John Mnyika ateuliwa kuwa Katibu Mkuu CHADEMA Taifa, Benson Kigaila-NKM Bara na Salum Mwalimu NKM Zanzibar

Acha ulofa wewe mnyika ni wa mwanza??? Mnyika ni wa kaskazini mpare huyo.Kanda ya ziwa hakuna jina mnyika iwe kwa kurya,jita,kerewe,zinza,haya,luo wala sukuma

Mkuu ni mimi umeniquote au umekosea njia? Kuna ajabu gani Mnyika kuwa wa Mwanza wakati Obama Ni wajaluo lakini mpaka US kuna akina Obama?
 
Hili ni swali tu ndugu zangu ambalo nimelileta kwenu na wala sina lengo lingine zaidi ya kutaka kujua maono na utabiri wenu tu.

Ikumbukwe kwamba hii ni nafasi nyeti sana ndani ya chama, inahitaji mtu mwenye uwezo mkubwa sana anayeweza kuunganisha viongozi na wanachama, mwenye uwezo wa kufuta makundi yaliyojitokeza kwenye uchaguzi huko kwenye kanda na kwenye Mabaraza, mbunifu na asiye muoga.
Kwahiyo ndo ulitumwa kuja kupima upepo humu jukwaani. Haya sasa chizi fresh ameshateuliwa msubiri wakati akiwa anakunywa dawa zake aje awavuruge.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
John Mnyika Ni mzuri, ila amekuwa mtulivu sana sijui shida ni nini. Ilikuwa vyema cdm wamchague mtu kama Marcus Albanie ili kuleta chachu mpya na sio sura zile zile kila siku. Sitarajii kuiona cdm mpya kwa mtiririko wa viongozi wale wale.
 
Kigaila mi namfahamu sana tangu mwaka alowatesa ccm Dodoma ni jembe sana. Nafasi kama ya ukatibu mkuu inahotaji mtu alive na mapenzi mema na CHADEMA full stop masuala ni professor, sijui ni Dr. Na blaa blaa nyingi hazina maana. Ukitaka kuamin hili kuna lichama linaongozwa na madokta lakini wanayoyafanya ni aibu hadi nataman kuhama hii nchi au duniaisimame mi nishuke kabisa. Kwelini aibu sana kukosa hoja hadi unagombana na vitambaa vinavyopepea? Aibu.
Naona wamesikia maoni yako mkuu.... Huyu kigaila wamemtendea haki kabisa. Naona chama kimerudi kwa wenyewe
 
Endeleen kukata viuno
Mtakumbuka kipindi ambacho Mnyika alikuwa mwiba mkali kwa Bwana mwenyekiti wa kudumu kwa kuhoji mambo ya siri ambayo wengi wao hawayajui ndani ya chama hicho na kutopata majibu ya kuridhisha kutoka kwa TOP leaders hali iliyompelekea kuonekana yuko kinyume na chama.

Baada ya vurumai kuzidi kuwa kubwa ndani ya chama hicho, hawa jamaa (MNYIKA na wenzake wawili akiwemo HECHE ) walidhamiria kujiengua chamani na kwenda Kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli, kitu ambacho kingekuwa mwiba wa utosi kwa Mzee Baba mwenye chama chake. Baada ya mwenye chama kujua hilo aliwaza na kukuna kichwa ni njia gani atumie ili "SIRI" wanazozijua hawa jamaa zisije zikatoka nje ya mipaka yake ndipo alipoamua kuwapa vyeo vya karibu yake kama njia ya kuwaweka karibu nae na awasuuze nafsi zao pamoja na kuwatoa PEPO la kuhama chama.

Fadhila hii pia ilimkuta Bwana LISSU, mtakumbuka hivi karibuni mipango ya snitch ZITTO KABWE kujikomba na kujipendekeza kwenda Ubelgiji kumsabahi jaamaangu wa Singida mashariki haikuwa ya bure. Kulikuwa na mipango na mikakati iliyofanikiwa kumshawishi LISSU kujiunga nae na kulikuwa na kila dalili za LISSU kujiunga na ACT Wazalendo kwa ahadi ya kuteuliwa kuwa mgombea wa Urais 2020 kwa tiketi ya ACT Wazalendo, Bwana mwenyekiti alivyoona hayo akaamua kumtoa KAFARA bwana PROF SAFARI ili kummezesha ndoano na kumpa fadhila bwana LISSU ili aendelee kusalia chamani. Hii ni njia aliyoitumia Mwenyekiti na kuwafunga midomo kabisa kuhoji mambo ya ndani kabisa ya chama. Kongole kwa Mwenyekiti wa kudumu kwa kuwamezesha ndoano jamaa hawa na lets hope watafunga midomo yao kuhoji mambo mazito ya chama.

Na hii ndio CHADEMA Mpya. Pipooooooo's

Sent using Jamii Forums mobile app
 
John Mnyika Ni mzuri, ila amekuwa mtulivu sana sijui shida ni nini. Ilikuwa vyema cdm wamchague mtu kama Marcus Albanie ili kuleta chachu mpya na sio sura zile zile kila siku. Sitarajii kuiona cdm mpya kwa mtiririko wa viongozi wale wale.
Mkuu Mnyika alishaahidiwa ukatibu mkuu toka enzi za Dr Slaa ndio maana akawekwa katibu. Sasa baada ya kupewa mashinji ni kama alisusa so huenda sasa atarudi Kwenye moto wake maana amepata alichotamani.

Btw mwanzoni alipotea sababu alikua anaugua issue za figo ila sasa naona yupo fiti kukivusha chama.
 
Uchaguzi huu umekuwa na changamoto kubwa kwasababu yakutokuaminiana ndio maana lkn naami mabadiliko yatakuja tu!
John Mnyika Ni mzuri, ila amekuwa mtulivu sana sijui shida ni nini. Ilikuwa vyema cdm wamchague mtu kama Marcus Albanie ili kuleta chachu mpya na sio sura zile zile kila siku. Sitarajii kuiona cdm mpya kwa mtiririko wa viongozi wale wale.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nikupongeze Mnyika kwa imani uliyopewa. Hujapewa ukuu bali utumishi. Hujapewa starehe bali mateso kutoka kwa wadhulumaji. Hujapewa sherehe bali huzuni ya mateso yako na wale utakaowaongoza. Hujapewa utajiri bali kufukarishwa na wenye roho ya ibilisi. Hujapewa utukufu bali udhalilisho unaofanywa na mbweha waliovaa ngozi za kondoo kuwahadaa Watanzania.

Mnyika unayajua hayo, umeyapokea hayo na umekubali kuyabeba. Hakika najua utasimama katika ukweli kama wale mitume waliokuwa wakisimama mbele ya watawala ibilisi wakitakiwa waikane imani yao ili wawe huru ili wapate starehe, lakini wakayakataa ya ibilisi, wakasimama katika ukweli kwa sababu walijua dhamira wanazozitumikia walipewa na zipo chini ya mwenye mamlaka makuu, mamlaka ya juu kabisa katika ukuu. Mtumikie aliye mkuu, japo mbwa kichaa hutisha maana anaweza kukung'ata na kukujeruhi. Lakini ujuacho ni kuwa mbwa kichaa pamoja na kuwa na uwezo wa kung'ata bado yeye ni mbwa kichaa. Watu wote walio wazima wanajua mbwa kichaa ni hatari kwa kila mmoja hata kwa mfugaji. Mbwa kichaa haishi milele, hata asipofanywa chochote, ukichaa unaomfanya ajeruhi watu ndio huo huo humwangamiza na yeye.

Mnyika simama katika ukweli, uuishi ukweli, uupiganie ukweli maana ukweli hauchangamanishwi na ulaghai au unafiki. Utambue hakuna kupigania haki kama hakuna mdhulumaji, hakuna kupigania uhuru kama hakuna mkoloni, hakuna kupigania ukombozi kama hakuna mtesaji, hakuna kupigania demokrasia kama hakuna dikteta. Basi ni mtu mwovu ndiye humtangaza yeye aliye mpambanaji dhidi ya dhuluma.

Tupo katika utawala ambao unafanya kazi ya kuwainua wapigania haki, wapigania uhuru na demokrasia. Hii ni fursa iliyo njema ya kuyainua majina makuu ambayo bila dhuluma, yasingeweza kujulikana. Fahamuni, tajiri hawezi kuwa maarufu kama hakuna maskini. Mpigania demokrasia hawezi kuwepo kama hakuna dikteta.

Mungu akubariki Mnyika, ukasimame kataka uimara.
 
Mkuu Mnyika alishaahidiwa ukatibu mkuu toka enzi za Dr Slaa ndio maana akawekwa katibu. Sasa baada ya kupewa mashinji ni kama alisusa so huenda sasa atarudi Kwenye moto wake maana amepata alichotamani.

Btw mwanzoni alipotea sababu alikua anaugua issue za figo ila sasa naona yupo fiti kukivusha chama.

Sina shaka kabisa na uwezo wa Mnyika, ila huu ukimya wake ingekuwa ni kwenye soka tungesema ni mchezaji aliyeshuka kiwango. Ngoja tuone kama atarudi kwenye ubora wake, japo nina mashaka na hilo. Muda utaamua.
 
Naona wamesikia maoni yako mkuu.... Huyu kigaila wamemtendea haki kabisa. Naona chama kimerudi kwa wenyewe
Yaani nimejisikia amani safu yangu ya uongozi imekamilika. Maana hata Mnyika akilegea Kigaila huwa na udhubutu sana ni jasiri kwa asili sio wa kurithi. Mungu aibariki safu hii. Hasa hawa makatibu ambao ndio watendaji wa chama.
 
Naweza kukubaliana na hoja yako 50% na kuikataa 50% kwan nimewahi kuhudumu ukatibu mahali
Katibu akifikir kinaenda KWA Mkiti hicho tayar kimepita
Naibu inabidi ashauriane na katibu saana ndipo katibu aipokee
Tusubir
Kama ni kweli mmechemsha vilevile, mnyika alikuwa naibu katibu mkuu muda wote kuna nini hajafanya bado? Hana jipya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
M/Mungu awatangulie viongozi wote wa CHADEMA
M/Mungu awalinde na kila shari za Pombe na VIBARAKA wake.
Nasema toka moyoni najivunia kuwa mwana CHADEMA.
 
Back
Top Bottom