John Mnyika ateuliwa kuwa Katibu Mkuu CHADEMA Taifa, Benson Kigaila-NKM Bara na Salum Mwalimu NKM Zanzibar

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
WanaJF Salaam

Ni siku nyingine muhimu kabisa katika historia ya chama kikuu cha upinzani nchini CHADEMA.

Baraza Kuu jipya la Chadema linakutana leo maalum kuichagua sekretariati mpya ya chama hicho itakayokivusha katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

Kwa mujibu wa Katiba ya chama hicho Mwenyekiti wa Taifa atapaswa kupendekeza majina kwa nafasi tatu za Katibu Mkuu na Manaibu wake wawili wa Tanganyika na Zanzibar.Kisha Baraza Kuu litapigia kura mapendekezo ya Mwenyekiti na kuwachagua rasmi watendaji hao.

Kwa sasa habari kuu hapa katika viwanja vya Mlimani City ni kuhusu jina la Katibu Mkuu mpya.Huku majina kadhaa yakitajwa na wajumbe kwa kubashiri.

Majina yaliyoko vinywani vya wajumbe na kuonekana kutajwa sana ni John Mnyika,John Heche,Salum Mwalim,Lazaro Nyalandu na Vicent Mashinji ambaye ni Katibu Mkuu anayemaliza muda wake.

Tunatarajia kuwaletea taarifa kamili ya uteuzi utakaofanywa na Mwenyekiti na tunawaahidi wasomaji wetu wa Jamii Forum kuwa wa kwanza kupata taarifa.

Asanteni sana
Wasalaam
Molemo wa JF

Updates Saa 11 Alfajiri - 20.12.2019

Freeman Aikael Mbowe Mwenyekiti wa chama Taifa amemteua John John Mnyika kuwa Katibu Mkuu Chadema

Pia Mbowe amewateua Benson Kigaila kuwa Naibu Katibu Mkuu Bara na Salum Mwalimu Naibu Katibu Mkuu Zanzibar

Katika uteuzi mwingine Kiongozi huyo mkuu wa Chadema amemteua John Heche kuwa mjumbe wa Kamati Kuu

Baraza Kuu kwa kauli moja limeridhia uteuzi huu wa Mwenyekiti wa chama na shangwe zimetawala katika ukumbi huu wa Mlimani city.

Screenshot_20191220-062134_Facebook.jpg
 

Attachments

  • VID-20191220-WA0080.mp4
    33.2 MB
Hili ni swali tu ndugu zangu ambalo nimelileta kwenu na wala sina lengo lingine zaidi ya kutaka kujua maono na utabiri wenu tu.

Ikumbukwe kwamba hii ni nafasi nyeti sana ndani ya chama, inahitaji mtu mwenye uwezo mkubwa sana anayeweza kuunganisha viongozi na wanachama, mwenye uwezo wa kufuta makundi yaliyojitokeza kwenye uchaguzi huko kwenye kanda na kwenye Mabaraza, mbunifu na asiye muoga.
 
Hili ni swali tu ndugu zangu ambalo nimelileta kwenu na wala sina lengo lingine zaidi ya kutaka kujua maono na utabiri wenu tu .

Ikumbukwe kwamba hii ni nafasi nyeti sana ndani ya chama , inahitaji mtu mwenye uwezo mkubwa sana anayeweza kuunganisha viongozi na wanachama , mwenye uwezo wa kufuta makundi yaliyojitokeza kwenye uchaguzi huko kwenye kanda na kwenye Mabaraza , mbunifu na asiye muoga .
Mkuu..kwa sasa pale anatakiwa mtu jabali kwelikweli type ya John Heche.
 
Back
Top Bottom