John Mnyika atafuna mifupa migumu iliyomshinda Keenja

diwani ubungo

New Member
Sep 14, 2012
4
2
Leo ilikuwa vifijo na nderemo kwa wakazi wanaoishi kata ya Makuburi na Ubungo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika maeneo ya Riverside, baada ya Mnyika kuwapa taarifa kwa upande wa Makuburi kuwa fidia ya wakazi waishio kwenye nyumba tatu pembeni ya mto gide kuwa imeshalipwa na wamepewa notisi ya siku 60 kupisha ujenzi wa barabara ya kwenda Makoka na ikiwa imeshatengewa kiasi cha shilingi milioni 110 soon baada ya nyumba hizo kuvunjwa.

Kwa upande wa wakazi wa kata ya Ubungo barabara inayounganisha barabara ya Mandela na Maziwa Road imeshapata mkandarasi wa kujenga kwa kiwango cha rami pamoja na daraja la double road, ikiwa na mafanikio ya kuibana TANROADS pamoja na Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni.
 
Kanyaga twende kamanda Mnyika hatua za kinyonga zinakishindo kirefu usikatishwe taamaa na mavuvuzela stay focus n objective
 
Kale kadaraja katapunguza msongamano wa external kwenda Maziwa.
Kumbe wengi tunaitegemea hii barabara?

Lakini mbona nahisi kama bajeti ya 110m kwa barabara ya kwenda Makoka ni ndogo sana? Au ni phase I kuna phase II inakuja?

Hivi barabara ya kuunganisha Mbezi Beach (kuanzia Massana Hosp) kwenda Mbezi ya Kimara ipo Jimbo gani? Au inaunganisha majimbo? Hii barabara ingewekewa lami ingesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza misongamano pale Ubungo. Hata ile ya Mbezi (ya Kimara) hadi Tabata
 
Kumbe wengi tunaitegemea hii barabara?

Lakini mbona nahisi kama bajeti ya 110m kwa barabara ya kwenda Makoka ni ndogo sana? Au ni phase I kuna phase II inakuja?

Hivi barabara ya kuunganisha Mbezi Beach (kuanzia Massana Hosp) kwenda Mbezi ya Kimara ipo Jimbo gani? Au inaunganisha majimbo? Hii barabara ingewekewa lami ingesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza misongamano pale Ubungo. Hata ile ya Mbezi (ya Kimara) hadi Tabata
Mkuu nimesoma mipango mingi ya barabara hapa dar hasa ule mpango wa kupunguza msongamano. Mpango ni mzuri kwa kuwa barabara zote unazozitaja zimo tatizo ni utekelezaji ambalo kila siku tunamuomba mnyika alisimamie. Nina hakika mipango ipo na hata kwenye ilani ya CCM kuna hizo barabara za kupunguza msongamano kama ukizozitaja. Mfano Maramba Mawili - Kinyerezi, Kimara Korogwe - External, Bunju - Mbezi ya Kimara, Kimara - Chuo Kikuu, nk. Kuna ring roads na bypass roads ambazo zote zina lengo la kupunguza msongamano.

Mkuu nadhani hizo million 110 ni kwa ajili tu ya kuichonga barabara hiyo na kuweka vifusi kwenye maeneo korofi. Million 110 haiwezi kuweka lami sehemu inayoeleweka vinginevyo iwe ni uji wa lami ambao hata kilometa moja haiwezi kwisha.
 
Back
Top Bottom