Fundi Madirisha
Senior Member
- Jun 30, 2020
- 184
- 987
Kwanza niwape pole sana uongozi na wanachama wa CHADEMA kwa madhila anayopitia kiongozi wao mkuu wa chama, hakika ni majaribu makubwa sana kwake yeye Mbowe binafsi, chama, na familia yake kwa ujumla.
MNYIKA AMEPEWA NINI NA CCM?
Hivi kweli CHADEMA leo ni wa kua wapole kiasi hiki kiongozi wao anateseka mahakamani kwa kesi ambayo inaonekana kabisa ni ya kufikirika, hakuna uhalisia wa kesi hapo ni mabishano tu ya kisheria against ukweli wa jambo lenyewe. Wanachama wa CHADEMA wapo kimya hakuna reactions zozote dhidi ya uonevu huu.
CHADEMA tazameni yalikuwa yakiendelea Kenya wakati Raila Odinga anakamatwa na kuwekwa ndani, angalie yaliyokuwa yakiendelea Afrika kusini wakati Jacob Zuma alipohukumiwa? Kesi zenye janja janja ya kisiasa si za kuvumilia wala kuendekeza. John Mnyika Kama katibu mkuu wa chama nilitegemea afanye organization ya wanachama nchi nzima wawe na amsha amsha ya kukataa uonevu. Mmekaliaooh sijui jambo liko mahakamani, jambo lenyewe lina sura gani?
Napata mashaka sana na John Mnyika Kama si Jasusi ndani ya chama.Ameshindwa kabisa ku-organize katiba mpya akidai eti ni swala la kitaifa kila mwananchi achukue hatua, yaani hata wanaccm wachukue hatua kwenye issue ya katiba mpya? Mnyika naanza kutilia shaka kama system haijamdaka na kuanza kumtumia. Wananchi na wanachama wapo tayari kila mkoa yeye anasubiri nini? Kuna Polisi wa kuwakamata wanachama wote nchi hii kwa sababu wanadai tume huru ya uchaguzi na katiba mpya?
Nimemlenga Mnyika kwa sababu ndiye katibu mkuu wa chama upinzani chenye wanachama na wafuasi wengi nchini, mimemtaja Mnyika kwa sababu ndiye mtendaji mkuu wa chama ambacho ndicho kinaweza kua mbadala wa mawazo ya serikali ya CCM. Yaani tangu Mbowe awe ndani chama ni kama hakina mtu.