John Mashaka Ni Mbunge Mtarajiwa!

Status
Not open for further replies.

Mzee Kifimbo

Senior Member
Mar 25, 2007
153
3
MTANZANIA ANAYEISHI MAREKANI BWANA JOHN MASHAKA AMEKUWA KWENYE VYOMBO VYA HABARI HASA BLOGS MBALIMBALI KUWA NI MTU ATAYEWEZA KUISAIDIA NCHI YETU KWA KIASI KIKUBWA AKIWA MBUNGE 2010.

IKIWA ATAFANIKIWA KUUKWA UBUNGE BASI WATANZANIA TUTAKUWA NA KICHWA KINGINE TOKA MAREKANI BAADA YA AMANI WALID KABOUR MBUNGE WA AFRICA MASHARIKI KWA SASA.

TUNAOMBA MAONI YETU JEE KIZAZI CHA DIASPORA KINA UWEZO MZURI WA KULIKOMBOA TAIFA LETU?
KABOUR ALILETA MABADILIKO YA KWELI?

INTERVIEW YA MASHAKA IKO MICHUZI BLOG AU INAPATIKANA HAPA.

http://issamichuzi.blogspot.com/2008/04/john-mashaka.html#comments
 
Posting zingine bwana......unamfanyia kampeni ama? Watanzania tupo 40 Mil unafikiri wangapi ni vichwa kuliko huyo Mashaka? Jina lake tu lanikwaza, sisi kwetu huamini jina la mtu huendana na tabia zake......
 
Simpigii kampeni nimeuliza maswali ya kujua kama DIASPORA wana uwezo? na Aman Kabour alifanya kweli au laa?

USHIROMBO.

Nataka tutumie mjadala huu kunoa vichwa vyetu.mara nyingi watu toka nje huwa wanatuleta habari za kujikweza zaidi kuliko uhalisia wa mambo.

Bwana Jack Pemba alisema anakuja kusaidia vipaji vya mpira wa miguu matokeo yake sasa hivi anashinda Twanga Pepeta au Akudo Impact.

Jack Pemba ni mwana DIASPORA.

Pitia kwanza interview ya bwana Mashaka kabla hujatia MASHAKA habari yake, usimuhukumu kabla ya kumsikiliza.
 
...not a good start na wengi watakuwa wana wasiwasi na watu kama hawa ingawaje inaonekana ana nia nzuri,ataonekana tuu kama hii ni campaign tuu ya kutaka ubunge/cheo or whatever,bora afanye anachofanya na asiongelee ubunge,namshauri aandike kitabu kwanza tujue vision yake na kusaidia wenzako sio lazima kupitia ubunge au kuanzisha NGO mana hivyo vyote vina reputation ya ufisadi,ana background ya business na kuna chinga na kina mama ntilie kibao wangehitaji msaada wake sana namna ya kuongeza faida zao...ukitaka tukuamini anzia kwenye grassroots maana huko ndio watanzania halisi wanaohitaji msaada wa kweli,lakini story za ubunge na NGOs hapa hazieleweki!
 
Simpigii kampeni nimeuliza maswali ya kujua kama DIASPORA wana uwezo? na Aman Kabour alifanya kweli au laa?

USHIROMBO.

Nataka tutumie mjadala huu kunoa vichwa vyetu.mara nyingi watu toka nje huwa wanatuleta habari za kujikweza zaidi kuliko uhalisia wa mambo.

Bwana Jack Pemba alisema anakuja kusaidia vipaji vya mpira wa miguu matokeo yake sasa hivi anashinda Twanga Pepeta au Akudo Impact.

Jack Pemba ni mwana DIASPORA.

Pitia kwanza interview ya bwana Mashaka kabla hujatia MASHAKA habari yake, usimuhukumu kabla ya kumsikiliza.

Ndg kifimbo

Tupo pamoja kuna watu wengi sana wanapenda cheap popularity, huyu bwana Mashaka amaisha fanya nini cha ajabu kushinda wengine ambao hawapigi kelele ama kujitangaza? nimemsoma kwenye blog nyingi tu.....kwangu mimi Kaborou alikuwa ni opportunist tu alijua kusoma alama za nyakati hakuna cha zaidi. Siwezi mweka kund moja na Mwakyembe, Anne Kilago ama Dr Slaa....ukiona mtu wa namna hii ni kuwa naye makini wakati mwingine anaweza kuwa amevaa ngozi ya chui kwenye kundi la kondoo...umetoa mfano mvuri sana wa Jack Pemba...tuendelee na issue
 
JF wakati mwingine inaudhi, mimi nilifikiri ameukwaa ubunge huko America kumbe yupo katika kampeni!! Sio vibaya kujiuza, lakini sasa hili tangazo lake amelipia au ni hivihivi tu?
 
kupiga kampeni vibaya ? kama hampendi, msifungue huu ukurasa wazee ! keep it moving ! and do the rest of the forum a favor by not posting anything !
 
kupiga kampeni vibaya ? kama hampendi, msifungue huu ukurasa wazee ! keep it moving ! and do the rest of the forum a favor by not posting anything !

..rudi kwenye ukada wa kuganga njaa zako maana wale wajinga unaowadanganya ndio mnaelewana lugha hapa kila ukifungua huo mdomo ni matapishi tuu!
 
Ufisadi wa EPA, Richmond wadhalilisha Watanzania Marekani
Na James Magai (Mwananchi)
�

BAADHI ya Watanzania wanaoishi Marekani, wamesema kashfa ya ufisadi iliyoibuka Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) na Kampuni ya Kuzalisha Umeme wa dharura ya Richmond Development Company LLC, imewadhalilisha.

Katika barua pepe aliyotuma kwa Mwananchi kutoka Jimbo la Carolina kwa niaba ya wenzake, John Mashaka alisema, kutokana na kashifa hizo, wamekuwa wakijiuliza kama wahusika ni wazawa au majambazi kutoka nchi za nje.

Mashaka alisema kutokana na hali hiyo, lazima wahusika wote wakamatwe na isipofanyika hivyo, itakuwa ni kejeli na matusi makubwa kwa walimu, polisi na wafanyakazi wengine wanaofanya kazi katika mazingira magumu.

�Ni jambo la kusikitisha na kutoa machozi, unapowaona watu wachache waliopewa dhamana ya kulinda nchi, wanajaribu kuifilisi na kuchezea jasho la Watanzania wengi, huku watoto wakifa hospitalini kwa kukosa tiba,� alisema Mashaka.

�

Kuhusu ufisadi, Mashaka alisema unasababishwa na watu kukosa uzalendo na kufanya uamuzi ambao hauna maslahi kwa Watanzania.

�Mtu mwenye ubinadamu katika nafsi yake na mwenye uzalendo na uchungu kwa nchi yake, kamwe hawezi kushiriki vitendo vya aibu kama vile vya Richmond na BoT,� alisema Mashaka.

Akitoa mfano wa Israel, Mashaka alisema nchi hiyo ina uwezo mkubwa kitaaluma kuliko mataifa makubwa yenye uwezo wa uchumi, kutokana na viongozi wake kutanguliza maslahi ya taifa mbele.

Mashaka alisema, Watanazania waishio Marekani, wameridhika na juhudi za Rais Jakaya Kikwete kuboresha maisha ya wananchi na kuweka Tanzania katika ramani nzuri.

Pia, alielezea kuridhishwa na jinsi wabunge wa chama tawala na vyama vya upinzani, walivyoungana na kushirikiana katika sakata la Richmond na kufanikiwa kuwang'oa mafisadi.

Licha ya ufisadi, Mashaka alisema wamefurahishwa na juhudi za serikali kutangaza Tanzania kimataifa hasa vivutio vikubwa vya utalii vilivyopo nchini.
 
..rudi kwenye ukada wa kuganga njaa zako maana wale wajinga unaowadanganya ndio mnaelewana lugha hapa kila ukifungua huo mdomo ni matapishi tuu!

am soooo not buying your statement ! kama matapishi ungekuwa una hata hiyo audacity ya kukaribia matapishi wewe ? bad enough, umeniquote, why dont you just ignore me and leave me the hell alone ! bana mie ndio KADA na wewe unaweza kuwa KADA vile vile, lakini UKADA wangu haujaanza jana wala leo ! upo hapo ?

kama kada ana njaa tatizo liko wapi ? nakubali njaa ninayo ! HUNGER FOR MORE !
 
huyo mashaka amekuwa msemaji wa nani na wakati wengine hatumjui,haya mambo ya cheap popularity yanamfanya aonekana kituko tuu...eti tunampongeza JK?kwa lipi au la kuachia mafisadi na kuwaweka kwenye cabinet yake tena.
 
kama hutaki kituko bora ungekaa kimya, lakini trust me kumuongelea ndio utakuwa unamcreate which is good for him ! haya mzee !
 
Mwanakijiji unamjua mheshimiwa Mashaka? ikiwezekana mfanyie interview tumjue zaidi.

makala nyingine inasema kuwa MASHAKA ni mfano wa kuigwa click hapa chini,

http://issamichuzi.blogspot.com/2008/03/mashaka-ni-mfano-wa-kuigwa.html

Vizuri tujue wapi kasaidia kama alivyosema mjumbe mmoja kuwa MAMA THEREZA alikuwa akijitolea na tunajua wapi alisaidia kama vile Mburahati kituo cha Yatima.

haitoshi kwa Mashaka kusema anajitolea ila hataki kusema wapi kapeleka lakini kutokea kwenye mitandao hakatai.

Tanzania kuna NGO karibu elfu hamsini zote zinasema zinasaidia masikini lakini hatujui wapi zinafanya kazi.

turudi kwenye swali la msingi kizazi cha DIASPORA kinaweza kutuongoza?
 
koh koh koh,nasafisha koo kidogo...hii njemba inaonekana ina chumvi nyingi kuliko hizo 30 ilizosema,koh koh koh...
 
Concept nzima ya mbunge mtarajiwa inachekesha.

Kila Mtanzania ambaye ana sifa za kuwa mbunge na si mbunge anaweza kusema ni mbunge mtarajiwa, kama vile kila mtoto wa kike anaweza kusema ni mama mtarajiwa.

Kwa hiyo tuambie kitu ambacho hatukijui, na siyo "Mbunge Mtarajiwa".Sema John Mashaka mshindi wa nishani fulani, au kada wa chama fulani, au iconoclast wa mlengo fulani tutaona distinction yake, lakini mbunge mtarajiwa?

Unamshushia hadhi mtu wako.

Pleease.
 
Tunahitaji kizazi cha wasomi kilicho uamishoni kirudi kusaidia nchi zao Afrika.Mashaka we rudi tu na mungu atakubariki sio wewe tu hatana wengine ila sio lazima uwe kwenye siasa ndio usaidie wenzako
 
Tunahitaji kizazi cha wasomi kilicho uamishoni kirudi kusaidia nchi zao Afrika.Mashaka we rudi tu na mungu atakubariki sio wewe tu hatana wengine ila sio lazima uwe kwenye siasa ndio usaidie wenzako

red- wewe je hurudi ?
blue-hizi imani ndio zinaturudisha nyuma !

Nashauri members wote wa JF mrudi tanzania, na kama mpo tanzania, basi twendeni ugaibuni !
 
Katika barua pepe aliyotuma kwa Mwananchi kutoka Jimbo la Carolina kwa niaba ya wenzake, John Mashaka alisema, kutokana na kashifa hizo, wamekuwa wakijiuliza kama wahusika ni wazawa au majambazi kutoka nchi za nje.
Huyu Mashaka kumbe anatoka Carolina, sasa ana fanya kazi Wall Street NY na kuishi Carolina au vipi? Na haya mambo yakuwasemea kwa niaba wabongo marekani vipi on what capacity and who gave him the mandate to speak on their behalf? Anampongeza mheshimiwa Rais kwa Richmond na EPA, have these issues been closed already au?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom