Elections 2015 John Magufuli: Waziri wa Ujenzi

Qualcomm

Senior Member
Nov 27, 2013
177
138
Mtatiro: Mjue John Magufuli Nani ni Nani Uraisi:

Historia yake

John Pombe Joseph Magufuli alizaliwa tarehe 29 Oktoba 1959 huko wilayani Chato Mkoani Kagera (hivi sasa Chato ni wilaya ya mkoa mpya wa Geita) na atatimiza miaka 56 Oktoba mwaka huu.

Magufuli alianza elimu ya msingi katika Shule ya Msingi Chato wilayani Chato mwaka 1967 na alihitimu mwaka 1974. Alifaulu na kujiunga na Shule ya Seminari Katoke, Biharamulo ambako alisoma kidato cha Kwanza na cha Pili mwaka 1975 - 1977, akahamishiwa Shule ya Sekondari Lake, Mwanza ambako alisoma kidato cha Tatu na Nne mwaka 1977 - 1978.

Masomo ya kidato cha Tano na Sita aliyapata mkoani Iringa katika Shule ya Sekondari Mkwawa kati ya mwaka 1979 na 1981. Halafu alirudi Chuo cha Ualimu Mkwawa kusomea Stashahada ya Elimu ya Sayansi akibobea kwenye masomo ya Kemia, Hisabati na Elimu; hii ilikuwa mwaka 1981 – 1982.

Alipopata stashahada yake, moja kwa moja alikwenda kuanza kazi ya ualimu katika Shule ya Sekondari Sengerema, akifundisha masomo ya Kemia na Hisabati. Ajira hii aliifanya kati ya mwaka 1982 na 1983.

Kisha alijiunga na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa mujibu wa sheria akianzia Makutupora, Dodoma (Julai - Desemba 1983), kisha akaenda kambi ya Makuyuni, Arusha (Januari hadi Machi 1984) na akamalizia katika kambi ya Mpwapwa mkoani Dodoma (Machi – Juni 1984).

Mwaka 1985 alijiunga Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akisomea Shahada ya Sayansi ya Elimu akibobea kwenye masomo ya Kemia na Hisabati na alihitimu mwaka 1988.

Mwaka 1989 - 1995 alifanya kazi katika kiwanda cha Nyanza Cooperative Union (Ltd.) akiwa mkemia na wakati huohuo alianza masomo ya shahada ya uzamili ya Sayansi katika Chuo Kikuu cha Salford nchini Uingereza, kikishirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambako alisoma kati ya mwaka 1991 na 1994.

Magufuli aliendelea na elimu ya juu zaidi kwa maana ya Shahada ya Uzamivu ya Kemia kuanzia mwaka 2000 hadi 2009 ambayo aliihitimu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kuwa mhitimu wa shahada ya udaktari. Dk Magufuli ana mke, watoto na familia imara.

Mbio za ubunge

Dk Magufuli alianza mbio za ubunge mwaka 1995, alipojitosa katika jimbo la Chato kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kushinda wakati akiwa na miaka 36. Rais Benjamin Mkapa akamteua kuwa Naibu Waziri katika Wizara ya Miundombinu. Kazi ya Ubunge na unaibu waziri ilimpeleka salama hadi mwaka 2000.

Uchaguzi wa mwaka 2000 ulipoitishwa, Dk Magufuli aligombea na kushinda kwa mara ya pili. Rais Mkapa akamteua kuwa Waziri wa Wizara ya Miundombinu na akakaa hapo hadi kipindi cha uongozi wa Mkapa kilipokamilika.

Mwaka 2005 aliendelea kutupa karata jimboni kwake kuwania ubunge kwa kipindi cha tatu. Akaingia kwenye orodha ya wabunge waliopita bila kupingwa. Lakini safari hii, Rais Jakaya Kikwete alimteua kuongoza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi hadi mwaka 2008 alipohamishiwa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, ambayo aliiongoza hadi mwaka 2010.
Mwaka 2010 wana CCM wa Chato hawakuchoka kumpa ridhaa Dk Magufuli, hii ikiwa mara ya nne. Mara hii hakupita bila kupingwa, alipambana na mgombea kutoka Chadema, Rukumbuza Vedastus Albogast ambaye alifanikiwa kumtoa jasho Magufuli.

Katika uchaguzi ule alipata ushindi wa asilimia 66.39 dhidi ya asilimia 26.55 za mgombea wa Chadema. Na baada ya kuchaguliwa kuwa mbunge kwa mara ya nne, Rais Kikwete alimrudisha katika Wizara ya Ujenzi ambako yuko hadi hivi sasa.

Mbio za urais

Dk Magufuli ni mmoja wa wana CCM ambao wamekuwa wakitajwa sana kuwa anaweza kuwa mgombea sahihi wa CCM baada ya kipindi cha Rais Kikwete kumalizika. Lakini yeye mwenyewe amekuwa akikana na kutotaka kuhusishwa na kinyang'anyiro hicho. Hata hivyo, watu wa karibu na Dk Magufuli wanasema kuwa ameshafuatwa na vigogo wakubwa ndani ya CCM wakimwomba, wakati ukifika, achukue fomu. Yeye amekuwa na msimamo kuwa anapaswa kupima hali ya mambo kabla hajaamua kujihusisha na urais au la.

Nguvu zake

Nguvu ya kwanza ya Magufuli iko katika uwezo wake wa kielimu. Inawezekana kuwa elimu si kila kitu katika siasa, lakini ukweli unabakia kuwa mwanasiasa mwenye elimu ya kutosha akiwa na sifa nyingine za kushika wadhifa fulani, ana nafasi kubwa sana ya kufikiriwa kuliko yule ambaye hana elimu. Katika hili Magufuli amejizatiti na amebobea sana. Elimu ukiichanganya na ujana vinamfanya awe mgombea wa umri ambao ni karata muhimu ndani ya CCM.

Lakini jambo lingine linalompa nguvu, ni kukaa kwa muda mrefu katika wizara zake. Amekuwa Naibu Waziri wa Miundombinu kwa miaka mitano na pia Waziri wa Miundombinu wakati wa Mkapa; akaongoza wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa miaka mitatu kabla ya kuongoza ile ya Uvuvi na Mifugo kwa miaka miwili. Lakini pia tangu mwaka 2010 hadi hivi leo ameiongoza Wizara ya Miundombinu bila kuhamishwa. Jambo hili hulikuti kwa mawaziri wengi sana, hasa katika serikali ya Kikwete.

Jambo la tatu linalompa nguvu ni umakini na na uwezo wa kusoma na kuchambua nyaraka. Watu wanaofanya kazi na Dk Magufuli, kote alikopita wanasema kuwa, tofauti na mawaziri wengi waliowazoea ambao huhitaji kuchambuliwa taarifa hadi zirahisishwe, kwake ni tofauti. Yeye husoma kila jambo na kwamba anatumia muda mwingi sana kusoma kila taarifa na hadi anaweka mistari na michoro kwenye taarifa.

Mhandisi mmoja ambaye amewahi kufungiwa leseni na Magufuli anasema kuwa kosa moja kubwa alilofanya ni kumwandikia Magufuli taarifa ndefu lakini yenye uongo kwenye aya moja. Anasema kuwa aya hiyo ilikuwa iko ukurasa wa 20 lakini ndani ya muda mfupi "Magufuli aliibaini na kibarua chake kiliota nyasi". Utendaji huu wa kufuatilia hadi vilivyomo kwenye maandishi ndani kabisa, umewashinda wanasiasa na viongozi wengi, Magufuli anabebwa na jambo hilo.

Udhaifu wake

Moja ya udhaifu mkubwa wa Dk Magufuli ni tabia ya "kufanya maamuzi haraka". Baadhi ya watendaji wa wizara yake wanasema kuwa anafanya maamuzi haraka mno na kuna wakati inaonekana maamuzi yake hayana tija, au ni ya kung'ang'ania tu kwa sababu za kimsimamo. Kuna mambo kadhaa ambayo yamekuwa na madhara makubwa katika wizara alizoziongoza:


Kwa mfano, uamuzi alioufanya wa kukamata meli iliyotuhumiwa kufanya uvuvi haramu na kukiuka sharia, haukuwa na tija kwa taifa kwani baada ya kesi ile kwisha, serikali iliamriwa kulipa kiasi cha shilingi za Kitanzania bilioni 2.8 pamoja na kurudisha meli husika kwani mahakama ilijiridhisha kuwa ilikuwa inafanya shughuli zake kihalali.

Lakini pia amewahi kufanya mazoezi ya "bomoa bomoa" kwa haraka mno tena kuna wakati bila kuzingatia haki za binadamu za wanaovunjiwa nyumba na makazi yao. Hii, ndiyo sababu Waziri Mkuu Mizengo Pinda, tena akiwa katika ziara ya Wilaya ya Chato alimtaka kutumia nguvu hizo kutumikia wananchi. Baadaye Rais Kikwete alifafanua watu wanaostahili kubomolewa nyumba kuwa ni wale waliofuata barabara na siyo wale wa asili na ambao barabara imewafuata. Kwa hiyo, wale ambao wamefuatwa na barabara wanastahili kulipwa fidia.

Kosa jingine kubwa linalompa Magufuli udhaifu usiomithilika, ni uamuzi na ushiriki wake katika mpango haramu wa uuzaji wa nyumba za serikali ambao ulilalamikiwa sana wakati akiwa Waziri wa Nyumba. Katika nchi ambayo wafanyakazi hawana nyumba na serikali inahitaji sana viwanja katika maeneo maalum, haikutarajiwa uamuzi wa namna ile ungekuwa na tija. Uamuzi ule uliisababishia serikali hasara kubwa na uliacha manung'uniko mengi maana hata wasio wafanyakazi wa serikali, nao walinufaika na nyumba zile.

Nini kinaweza kumfanya apitishwe?

Suala la kwanza linaloweza kumvusha Dk Magufuli kwenye chekecheo la wagombea ndani ya CCM ni uchapakazi na nidhamu kazini. Magufuli ni mchapakazi na mimi binafsi namwona kama waziri mchapakazi kuliko mawaziri wote ambao wamebahatika kufanya kazi kwenye serikali ya Kikwete. Ikiwa CCM inahitaji Rais ambaye atakuwa na uwezo mkubwa wa kutenda na kusimamia kazi, basi Magufuli ndiye anaweza kabisa kuchukua nafasi.

Jambo jingine linaloweza kumvusha Magufuli ni msimamo. Yeye ni kiongozi mwenye misimamo isiyotia shaka. Hajui kuuma maneno lakini anajua nini anachokisimamia. Watendaji wa Wizara ya Miundombinu wanasema ni vigumu kumyumbisha Magufuli katika jambo ambalo anaona hilo ndiyo njia, lazima mlitekeleze kwanza. Tabia ya namna hiyo alikuwa nayo Mwalimu Julius Nyerere, kwamba akishaamua jambo fulani na kama anajua njia yake, humtoi relini.

Alipokuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi alithubutu hata kumtaja Naibu wake kwamba anahodhi viwanja. Mwaka 2013, aliwashangaza watu wakati alipopishana hadharani na Waziri Mkuu Pinda, kuhusu suala la magari ya mizigo kupita katika barabara yakiwa yamezidisha uzito.

Baada ya Pinda kuruhusu, Magufuli aliweka msimamo kuwa jambo hilo halikubaliki na halitekelezeki na akalipiga marufuku. Baadhi ya watu walichukulia msimamo wa Magufuli kama dharau kwa Waziri Mkuu wake lakini wanaomfahamu wanasema angekuwa tayari kufa na msimamo wake. Ikiwa CCM wanahitaji mgombea urais mwenye sifa ya msimamo thabiti, namwona Magufuli akiwa mbele kabisa.

Jambo la tatu ni kutokuwa na makundi. Kati ya mambo ambayo yanaiumiza CCM hivi sasa ni ikiwa itajikuta imepitisha mgombea mwenye makundi na anayeweza kuleta migawanyiko. Chama hicho kinahofia kuwa mtu wa namna hiyo atakosa uungwaji mkono wa makundi yanayosigana na hivyo anaweza kuangushwa kwenye uchaguzi kutokana na vita ya ndani ya chama.

Pamoja na Magufuli kuwa waziri muhimu sana kwenye serikali ya Kikwete, angeweza kuwa mtu wa maana kwenye makundi ya kusaka urais lakini amejiweka pembeni sana. Kwa sababu ya kusimama katikati, anaweza kabisa kuwa mmoja wa watu watakaoonekana wanastahili kupewa nafasi ili kutuliza nguvu ya makundi. Kuna wakati Samuel Sitta alidai kwamba wakati ukifika atashirikiana na marafiki zake Bernard Membe, Harrison Mwakyembe pamoja na Magufuli kumchagua anayefaa kuwania urais, lakini Magufuli alikana na kujiweka kando na kundi hilo.



Kingine kinachoweza kumpitisha ni kufahamika na kuuzika. Bila shaka CCM inahitaji mgombea anayeuzika na kufahamika ili kupunguza mishale ambayo itakuwa inapigwa na UKAWA dhidi ya taswira ‘mbaya" ya chama hicho. Ili kujitoa katika hatari hiyo nadhani Magufuli anaweza kuvushwa.


Na mwisho, Magufuli anaweza kuvuka mchujo kwa sababu ya taswira yake kwa Rais Kikwete. Kama tunavyofahamu, rais anayeondoka anakuwa na mchango mkubwa katika kusababisha uteuzi wa rais ajaye na tayari kuna viashiria vingi mno vinavyoonesha kuwa Kikwete huenda anamchukulia Magufuli kati ya wana CCM wachache anaowaamini.

Kikwete amewahi kuhutubia mkutano mmoja Kanda ya Ziwa na wananchi wakawa hawamsikilizi, bali alipopanda jukwaani Magufuli, wananchi wakanyamaza na Kikwete akarudishiwa kipaza sauti akaendelea na hotuba yake huku akisisitiza kuwa Magufuli ni kiongozi imara.

Lakini kama hiyo haitoshi, Rais Kikwete alipotoka kwenye matibabu nchini Marekani aliwahi kunukuliwa akisema "…nilitaka kutangaza mapema kuhusu ugonjwa wa kansa uliokuwa ukinisumbua, lakini Magufuli ndiye alinikataza kufanya hivyo wakati wa kikao cha Baraza la Mawaziri". Kauli hii ya Kikwete inachukuliwa kama dalili ya kuonesha ni jinsi gani anamwamini Magufuli. Na hata katika hotuba zake Dk Magufuli hakosi kumsifu Dk Kikwete.

Nini kinaweza kumwangusha?

Jambo la kwanza linaloweza kumwangusha Magufuli ni dhana ya "ugeni" ndani ya CCM. Magufuli hakuwahi kuwa kiongozi wa CCM na hakuwahi kuitumikia CCM. Yeye amefanya kazi serikalini kisha akawa mbunge, na kwa miaka 20 sasa amekuwa waziri na si kiongozi wa CCM. Wahafidhina na watu wasiokubali mabadiliko ndani ya CCM wanamchukulia kama "mtu wa kuja" kwenye chama chao na ikiwa sauti zao zitakuwa nyingi anaweza kuangushwa.

Kitu cha pili ni misimamo yake. Misimamo inaweza kumvusha Magufuli kwenye mchujo wa wagombea wa CCM, pia inaweza kabisa kumwangusha. Ikiwa upitishaji wagombea utafanywa kwa lengo la kupata mtu ambaye ikiwa atakuwa rais atakuja kuendeleza mitandao, kujuana na kubebana, nadhani Magufuli ataogopwa. Misimamo yake katika baadhi ya mambo imekuwa ikiwakwaza makada wa chama hicho ambao wangependa ulaji uendelee kuwepo, kwa hiyo, sifa hii inaweza kutumika kumpunguza.

Jambo la mwisho linaloweza kumwengua kwenye safari hii ni kukosa kundi kubwa ndani ya chama linalomuunga mkono. Ndani ya CCM, kwa wanachama wa kawaida, naambiwa hata katika vikao vya chama hicho, Magufui hana uungwaji mkono mkubwa. Hali hii inaweza kuwa kikwazo kwake, hasa itakapotokea kuwa makundi makubwa ya wasaka urais yakapenya na kufanikiwa kuteka mwelekeo wa maamuzi ya chama hicho.

Asipopitishwa (mpango B)

Magufuli anaweza kuwa na mipango miwili muhimu kwa sasa. Kwanza, kuendelea na ubunge katika jimbo la Chato. Pamoja na kuwa hali yake ya kisiasa ndani ya jimbo si salama sana kwa maana ya nguvu ya UKAWA kuzidi kuwa kubwa, bado anaweza kurejea na akafanikiwa na huenda, kama chama chake bado kitachaguliwa kuongoza dola baada ya uchaguzi, anaweza kupenya na kuchukua nafasi ya juu zaidi ya uwaziri.

Pili, aaweza kurudi chuo kikuu ili kufundisha vijana. Kama tunavyofahamu nchi yetu iko kwenye kampeni kali ya kuhamasisha vijana wasome sayansi na Magufuli ni mwanasayansi aliyebobea katika masomo ya Kemia na Hisabati. Atakuwa na fursa nzuri sana ya kulisaidia taifa kukuza uwezo wa taaluma ya vijana katika maeneo aliyobobea.

Hitimisho

Wahenga walisema, "mwenda pole ndiye hula vinono". Mipango ya kimya kimya ya Magufuli katika safari ya ikulu kupitia CCM inaweza kuwa na maana kubwa sana. Tayari tumekwishaona makada wote wa chama hicho ambao walianza safari hiyo kwa fujo na mbwembwe wakionywa na kuwekwa kwenye uangalizi maalum. Inawezekana Magufuli alisoma "mchezo" huu mapema na akawa hataki "kudandia treni kwa mbele".

Nachokiona mimi ni kuwa Magufuli ni mmoja wa wana CCM tishio sana dhidi ya makundi makubwa ya vigogo ambayo yamejipanga kuingia ikulu muongo mmoja uliopita. Namtakia ndugu John Pombe Joseph Magufuli, safari salama na ya heri katika mbio hizi.








 
Atakwamishwa na uuzaji wa nyumba za serikali, kivuko MV dar es salaam; barabara dar msata; barabara za mbweni jkt ; madaraja mangumashi bil.230 yeye na mwakyembe
 


Moja ya udhaifu mkubwa wa Dk Magufuli ni tabia ya "kufanya maamuzi haraka". Baadhi ya watendaji wa wizara yake wanasema kuwa anafanya maamuzi haraka mno na kuna wakati inaonekana maamuzi yake hayana tija, au ni ya kung'ang'ania tu kwa sababu za kimsimamo. Kuna mambo kadhaa ambayo yamekuwa na madhara makubwa katika wizara alizoziongoza:


Kwa mfano, uamuzi alioufanya wa kukamata meli iliyotuhumiwa kufanya uvuvi haramu na kukiuka sharia, haukuwa na tija kwa taifa kwani baada ya kesi ile kwisha, serikali iliamriwa kulipa kiasi cha shilingi za Kitanzania bilioni 2.8 pamoja na kurudisha meli husika kwani mahakama ilijiridhisha kuwa ilikuwa inafanya shughuli zake kihalali.

Lakini pia amewahi kufanya mazoezi ya "bomoa bomoa" kwa haraka mno tena kuna wakati bila kuzingatia haki za binadamu za wanaovunjiwa nyumba na makazi yao. Hii, ndiyo sababu Waziri Mkuu Mizengo Pinda, tena akiwa katika ziara ya Wilaya ya Chato alimtaka kutumia nguvu hizo kutumikia wananchi. Baadaye Rais Kikwete alifafanua watu wanaostahili kubomolewa nyumba kuwa ni wale waliofuata barabara na siyo wale wa asili na ambao barabara imewafuata. Kwa hiyo, wale ambao wamefuatwa na barabara wanastahili kulipwa fidia.

Kosa jingine kubwa linalompa Magufuli udhaifu usiomithilika, ni uamuzi na ushiriki wake katika mpango haramu wa uuzaji wa nyumba za serikali ambao ulilalamikiwa sana wakati akiwa Waziri wa Nyumba. Katika nchi ambayo wafanyakazi hawana nyumba na serikali inahitaji sana viwanja katika maeneo maalum, haikutarajiwa uamuzi wa namna ile ungekuwa na tija. Uamuzi ule uliisababishia serikali hasara kubwa na uliacha manung'uniko mengi maana hata wasio wafanyakazi wa serikali, nao walinufaika na nyumba zile.
Hii ni muhimu kuliko sifa zake zingine, tunapomjadili Magufuli kama mgombea wa Chama Tawala. Nina shaka uwezo wake wa kidiplomasia na uvumilivu sifuri unaweza kugharimu taifa pakubwa kama anakuwa rais.

Kwa washabiki wa 'mwana-ukome' tunaweza kumuona ni mtendaji lakini kuna loopholes kwenye sheria ambazo huwafanya waathirika wa maamuzi ya kijinga wafungue kesi na kuidai Serikali mamilioni.

Tusubiri!
 
Hii Ni Kujibu Moja ya Mambo yaliyotumwa HUMU Kumtuhumu huyu Mzee

1. Nyumba za serikali: Zilichoka sana,
hazikuwa na fungu la maintenance kutokana na udogo wa kodi inayolipwa kwa njia ya makato ya mishahara. Ameuza nyumba kwa watanzania, chini ya mpango huo, ameshajenga nyumba mara dufu zaidi ya hizo. Na wanaishi watanzania. Kwa kauli yake mwenyewe, atajenga na ntauza, ataendelea kujenga na ataendelea kuuza.
hapa mkuu, tuache roho ya kwa nini sio mimi!!!!

2. Ujenzi wa Barabara: Haya ni Majungu, na umbumbumbu wa kitaaluma. Tambua kuwa Ujenzi wa Barabara una michakato mingi, na husimamiwa kitaaluma. Magufuli sio Mhandisi, Sio Quantity Surveyor na wala sio Architect. Uthibitisho wa vipimo vya barabara ni wa kitaaluma zaidi, na hivyo, kama ni hoja, ipelekwe kwa wakaguzi wa fedha na works inspector. Sio Magufuli. Bado mzee huna hoja.

3. Sakata La Bomoa Bomoa. Mzee. Hapa umpongeze sana mzee huyu kwa kuisimamia sheria. Ameweza kuongea watu wakorofi wakajua hili. Kawaida ya miundombinu ya nchi kama barabara, umeme, gesi, maji, mkonga au mkongo?? Hupewa kitu kinaitwa corridor. Leo hii kwa maendeleo ya watanzania, tunahitaji kutumia miundombinu yote hii (barabara, maji, umeme, gesi, internet). Lakini njia zilizoainishwa kitaalamu, zimevamiwa na ujenzi usiozingatia sheria za mipango miji. Mzee, kubali watu wapelekewe huduma muhimu hizi. Kwa taarifa, angalia historia ya miji mikongwe kama New Delhi, Washington, Cairo! Jinsi ilivyofanikiwa kuendelezwa. Ni baada ya kukubali kuachia njia kuu ili miundombinu ipite. Mimi namshauri Mh Magufuli, pamoja na mambo mengine, aanze na hili kwa utaratibu atakoona unafaa.4. Shelly Ya Mwanza: Mzee uliza uambiwe. Kuna mambo hapa unayasemea bila takwimu. Hii imejibiwa na namba 3, lakini kwa nyongeza tu, kushinda kesi mahakamani kwa watu ambao tunawafahamu a, b, c zao! Hapa nakuachia point moja. Kweli kuna makosa ya kiutekelezaji yalifanyika, lakini sio kosa la nia na dhamira ya Magufuli kuhakikisha road reserves zinaachwa wazi..

5. Magufuli ni mtu mwenye kiburi, majivuno na hashauriki: Unapomtuhumu mtu kwa kiburi na majivuno, sio sawa. Ukitaka ututendee haki wasomaji, tueleze wewe ukoje? Labda wanaokufahamu watasema. Hata hivo, hakuna mtu ambaye hajipambanui kwa tabia na hulka.

6. Umiliki wa Kebby's Hotel: Haya ni majungu.

7. Kuvunja Ndoa: Haya ni majungu mengine. Ila unaweza fungua kesi sasa kama unao ushahidi. Hii ilifanyika kwa Mh mmoja huko UKAWA na kilichoendelea huko, ni kusuluhishana kimya kimya. Na inasemekana huyu MKAWA anagombea urais.

8. Magufuli Hakifahamu Chama Vizuri: Kufahamu au kutofahamu chama inatokana na opportunity tu, ya kupata fursa ya kutumikia chama. Oportunity nyingine, ni kutumikia serikali, hata NGO. Haina maana usipotumikia chama huwezigombea nafasi kubwa nchini. Hapa huna hoja kabisa.9. Sakata La Samaki: Kosa la Magufuli nilipi? Sasa wezi wa samaki wetu watambue wazi. Yule askali wa mwavuli anarudi kwa sura mpya. Wajiandae kukamatwa na hakuna mizengwe tena ya uendeshaji kesi za aina hii.

10. Sakata La Kivuko: Ulianza vizuri, lakini hapa umeishiwa kaka. Watanzania mnapenda sana ku-amplify mambo. Tumeshuhudia kauli kama ...., they can go to hell by Malechela, .... vijisenti by Chenge, .... hela ya mboga by Tibaijuka. Hizi ni sentensi nyepesi sana ambazo watu mmeziamplify tu.... Hakuna hoja hapa.

11. Magufuli ni Mtu wa Visasi vya Hatari: Haya ni mashambulizi binafsi, nafikiri hata Makufuli inabidi ayakubali. Mie nauliza, je wale wagonjwa wote waliolzwa hospitali kwa mashinikizo ya moyo, wameshindana na Magufuli? Ugonjwa husababishwa na mambo mengi sana. Ninavyofahamu mimi, hata Mh Magufuli, aliwahi kulazwa hospitali kwa ugonjwa. Sijui naye angedai kuwa ni visasi vya washindani wake kisiasa, nani atabebeshwa mzigo??
 
Hii ni muhimu kuliko sifa zake zingine, tunapomjadili Magufuli kama mgombea wa Chama Tawala. Nina shaka uwezo wake wa kidiplomasia na uvumilivu sifuri unaweza kugharimu taifa pakubwa kama anakuwa rais.

Kwa washabiki wa 'mwana-ukome' tunaweza kumuona ni mtendaji lakini kuna loopholes kwenye sheria ambazo huwafanya waathirika wa maamuzi ya kijinga wafungue kesi na kuidai Serikali mamilioni.

Tusubiri!

hapo nimekuelewa sana manake maamuzi ya haraka bila kufanya utafiti itamgharimu sana.
 
Kumbe Pinda mwenyewe alishawahi kuonja jeuri ya Magufuli.!
 
Ndoto piga mbizi . Watu bhana sh. 200 nayo hela ya kulalamika. Kivuko cha geita sh. 400 nyie 200 mnalalamika pigeni mbizi.
 
Back
Top Bottom