Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,443
- 113,456
Mwiba, amini nakuambia wewe ndio unawazimu!.Nakumbuka msemo wa kikwetu usemao "...Ukimsifu mgema tembo hulitia maji...! Magufuli amesema yale majumba ya shirika la umeme yanayoleta mandhari ya aina yake hapa jijini yaliyojengwa kwa mabilioni ya shilingi ni lazima yavunjwe eti yamejengwa kwenye sehemu iliyohifadhiwa kwa ajili ya kupita barabara.
Huyu mtu kama hana wazimu atakuwa na kitu gani hivi anafikiria hela iliyotumika ni hela ya serikali, ? Au ya shirika la umeme ,akili za watu wengine zinakuwa za ajabu ajabu ,anachotaka ni kuwapa tanesco eneo jingine wajenge upya ,kwa maana kwa dau hilo hela ingine itapatikana na wajanja kupata chao.
Mtu huyu alikuwa wapi wakati majumba hayo yakijengwa ?Serikali ilikuwa wapi ?
Unaenda kuvunja mijumba hiyo kwenye nchi ambayo uchumi wake ni wa kubahatisha au wakuu mnataka na kutafuta njia mbadala ya kufanya ufisadi,
Unajisikiaje kuitwa 'Mwiba una wazimu!', hizi lugha nyingine, sio za kutumia!, Magufuli ni waziri halali wa JMT wewe unamuita anawazimu, sio tuu unataka kumshushia hadhi, bali pia unaidharaulisha JF.
Unataka kuithaminisha sheria na fedha?. Eneo lile inajengwa fly over, hebu kwa akili piga kila hesabu hiyo fly over ichepushiwe wapi?.
Sio jengo tuu la Tanesco pale, majengo yote kuzunguka pale yanaondoka, na kama CCM watamsimamisha Magufuli 2015, tutamshauri Dr, asipoteze muda!, maana akishinda, mtu wa kanza kumpandisha kizimbani ni JK!,