John Magufuli, Rais mwenye kubeba imani ya watu wa kipato cha chini, A Populist Leader

Leslie Mbena

JF-Expert Member
Nov 24, 2019
207
677
JOHN MAGUFULI,RAIS MWENYE KUBEBA IMANI YA WATU WA KIPATO CHA CHINI,A POPULIST LEADER.

Leo 20:45pm,05/12/2019.

Rais wetu John Magufuli jinsi anavyopendwa na idadi kubwa ya Watanzania wa rika zote inatoa picha kuwa ndiye mwenye kubeba imani kubwa ya Wananchi wengi wa kipato cha chini ambao kwa muda mrefu walisahaulika na badala yake tabaka la matajiri lilitamba na kuwanyanyasa.

Rais John Magufuli ndiye mbeba maono ya Watanzania kwa sasa baada ya wabeba maono watatu kushindwa kupenya ikulu na kutekeleza maono ya Watanzania,Mwaka 1995 tulimuona mbeba maono na imani ya watu wa hali ya chini kwa lugha ya beberu wanasema "a Populist leader" Augustino Lyatonga Mrema ambaye kwa hakika alibeba imani ya watu wa hali ya chini walioona wametengwa baada ya visa vya Chavda na kuuzwa kwa ardhi ya Loliondo.

Mwaka 2010 alitokea "Populist leader" mwingine Dkt Wilbroad Slaa ambaye kwa hakika nae alishinda imani ya Watanzania wengi wa kipato cha chini na kubeba maono yao hasa baada skendo ya Ufisadi wa Richmond na yeye kuanzisha operation sangara iliyozunguka Tanzania nzima kupinga mafisadi papa.

Mwaka 2015, Edward Lowassa alishinda imani ya Wananchi wengi wa hali ya chini na kubeba maono ya Watanzania baada ya skendo ya Escrow na kuahidi kuwashughulikia mafisadi wote bila kuogopa na kutishia kuwagusa hata wale ambao walikuwa hawagusiki kwa lugha ya beberu "untouchable ".

John Pombe Magufuli akionekana kuyajua matatizo mengi ya Wananchi wa hali ya chini baada ya kuyaishi matatizo na kujua suluhisho,Mungu akamleta kuja kubeba maono ya wote waliomtangulia na hasa kubeba imani kubwa ya Wananchi wengi masikini ambao walikuwa wameshasahaulika katika awamu tatu zilizopita.

Hivi sasa makundi mengi ya watanzania wameonekana kumuunga mkono na haswa kundi la Wananchi masikini ambao amekuwa akiwasemea matatizo yao na kujua kuwa ndiye waliyempigia kura mwaka 2015 kuja kuwawakilisha kama Rais wao, na hasa kuwaondoa kwenye mkwamo Wa kiuchumi uliowasulubu miaka nenda rudi kwa kuwa keki ya taifa ililiwa na watu wachache.

Rais John Magufuli amekuwa kiongozi mwenye weledi Wa kutosha sana na utumishi uliotukuka na heshima hiyo watanzania wameona wamtunuku tena miaka mitano ijayo yaani 2020 hadi 2025 ili aweze kuipeleka Tanzania katika nchi zenye uchumi wa kati.

Rais John Magufuli amekuwa kiongozi mwenye kutokomeza matabaka ya " mabwanyenye na wasakatonge" na kuleta Usawa wa kimaisha kwa kila mmoja tajiri na masikini na wanaompinga ni kuwa hawajui wanachopinga na wameishia kufanya sweeping analysis kwa fikra za utopian na Wananchi wameamua hawatarudi nyuma na mwaka 2020 Watanzania tutampa tena Rais John Magufuli miaka mingine mitano kwani ndiye kiongozi bora na mwenye maono ya uzalendo kwa lugha ya beberu "A populist and patriotic leader".

Miaka ishirini iliyopita Augustino Mrema, Dkt Wilbroad Slaa na Edward Lowassa walipata umaarufu katika kipindi ambacho wananchi wengi waliamini kuwa nchi inanuka rushwa na ufisadi ambao ulikuwa unagusa maisha ya chini kabisa ya wananchi.

Hakuna wakati ambao watawala wanaogopa kama watu wa kipato cha chini kabisa wanapoamua kupambana na utawala,Kwa awamu tatu zilizopita upinzani ukaimarika Tanzania kwa kuwa tu wananchi wa hali ya chini waliona wametengwa na wakaamua kupambana na utawala mapambano yaliyoongozwa na Upinzani.

Utawala wa sasa chini ya Rais John Magufuli umejenga imani kwa watu wa kipato cha chini na masikini ambao wanaamini matatizo yao yanafanyiwa kazi na wamehakikisha utendaji kazi ni mkubwa kuliko maneno na propaganda. Kujenga Imani kwa wananchi wengi ni nguzo na silaha mathubuti kwa wanasiasa.

Kinyume chake sasa upinzani nchini Tanzania unapata uungwaji mkono kutoka kwa baadhi ya wananchi wenye kipato cha kati na juu na manazi wa ubeberu,ufisadi na upigaji dili na hela chafu kwa sababu utawala huu umehakikisha kipato chao kisichofuata sheria na utaratibu vimedhibitiwa na keki ya Taifa inaliwa na Wananchi wote.

Nadhani kelele za ''elitist'' na wanazi wa ubepari kwa payrol ya akina Zito,Fatma,Maria,na wafuasi wao kwenye mitandao ya kijamii zinadhibitisha kuwa upinzani wa Tanzania hivi umegeuka na kuwapigania mabeberu,mabwanyenye,mafisadi na "criminals" ambapo tayari tumeshuhudia wakiiba madini yetu miaka nenda rudi na kutuachia mashimo katika ardhi yeti.

Niwatahadharishe tu wapinzani wa Tanzania kwa sasa,Ogopeni sana watawala wanaoitwa ''populist leaders'' katika wakati ambao wananchi wengi masikini wamejenga imani nao mfano sasa ambapo wananchi wengi wamejenga imani yao kwa Rais John Magufuli.

Mrema na Dkt. Slaa walikuwa ''populist leaders'' kama ilivyo kwa Rais Magufuli kwa sasa.

Katika Uchaguzi ambao present incumbent haitakuwa na shida ni katika Uchaguzi Mkuu wa 2020.

Watu wenye akili pana na maono kwa sasa hawaongelei Uchaguzi wa 2020 kwa sababu mshindi anajulikana labda litokee jambo ambalo liko nje ya uwezo wa kibinadamu. Ndio maana unasikia watu wanaongelea suala la kubadilisha katiba au la kwa sababu wanajua mwaka 2020 atashinda Uchaguzi Mkuu na suala je atayekuja ataweza kwenda na kasi ya sasa ya Rais John Magufuli au tumpe tena miaka kumi hadi 2035.

Nimalizie kwa kusema John Magufuli ndiye Rais aliyebeba imani ya Watanzania wengi wa hali ya chini,masikini,wenye kumudu mlo wa siku kwa taabu akiwa na lengo la kuwainua,kuwapa nguvu ya kufanya kazi na kupata kipato.

Rais mwenye kuwafanya watu wote wa nchi yake bila matabaka kuwa sehemu ya wanufaika wa uchumi wa Taifa. Rais John Pombe Magufuli ndiye mwenye lengo lenye hakika ya kweli ya kuwajumuisha Watanzania wote kufaidika na rasilimali na utajiri wa Taifa lao.

Ahsante Mwenyezi Mungu kwa kumbariki Rais wetu John Magufuli,Ahsante kwa kuibariki Tanzania.

Nikiishia hapa,Mimi ni,
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854
 
Kweli wewe ni original CHAKUBANGA
Huyo Chakubanga angesoma kwanza tafsiri ya populist leader halafu atuambie ni sayari gani populist leader alifanikiwa na kuwa tumaini kwa anaowatawala. Mtaji mkubwa wa populist leader ni ujinga na woga wa anaowatawala na si kuwaongoza.

Hatma ya populist leader ni udikteta uchwara kwani adui mkubwa wa populist leader ni demokrasia au uhuru wa mawazo. Populist leader anaamini ni yeye tu anayejua what's best kwa taifa na hilo ndilo tunalishuhudia hapa kwetu.

Populist leader is a politician who pejoratively panders to people’s fear and enthusiasm. Populism has never succeeded and is short-lived for eventually the same people will rise up and rebel against imminent authoritarianism.
 
well said japo wengi watakupinga
lakini ndiyo ukweli
Dhana ya 'populism' siyo nzuri kuitumia hasa kwa mtu unayeona anafanya vizuri.

Hivyo naona kama vile umejichanganya.

Maana halisi ya "populist leader" ni kiongozi anayefanya siasa za ulaghai akiwaaminisha watu kwamba matatizo yao yanasababishwa na kundi dogo la jamii lililofanikiwa ama matajiri au lolote lile ambalo huwa la kipekee.

Hivyo hufanya siasa za kutaka uungwaji mkono na kundi la watu masikini ili apambane na matajiri.

Kiuhalisia viongozi wa namna hii hupata umaarufu wa muda mfupi maana watu hugundua kuwa licha ya kundi la matajiri kupunguzwa nguvu hali ya maisha ya "wanyonge" huzidi kuwa mbaya.
 
matunge,
Ametumia neno pupulist akidhani ana mjaza misifa kumbe anamuonyesha uhalisia wake, ndo tatizo LA kuwa praise n worship
 
Haya ndio matokeo ya ushudu wa lumumba mwenyewe unaona kama umemsifia japo najua hata muhusika akiusoma uzi atakuwa hiv😂😁😁😁
 
Mag3,
umetafsiri vizuri sana.

this stupid alieleta hii mada anadhani kuwa populist ni sifa yenye tija kwa nchi.
 
umetafsiri vizuri sana.

this stupid alieleta hii mada anadhani kuwa populist ni sifa yenye tija kwa nchi.

Huwezi kuamini wanaccm wengi hawajui tofauti ya hilo neno, na huyo aliyemwaga hizo sifa ndio anategemewa kwa kujenga hoja!
 
Angesema tu, Watanzania wa hali ya chini na wenye umaskini ulitopea, pia wajinga flan hivi ambao wanashindwa kuchanganua mambo.

Hakuna Mtanzania mwenye akili zake na ameenda shule kufuta ujinga atampenda Magufuli.
 
Back
Top Bottom