Alimfukuza kazi Mrema Wa TANROADS kwa kuwa alikuwa ni FUNDI nzuri.
Kagame ni thinker mwenye akili na vision ya muda mrefu kwa nchi yake. Siyo mkurupukaji. Sijasikia vision ya Magufuli zaidi ya kuongelea miradi kwenye kampeni zake.Hata Kagame nasikia ni dikteta ndio maana Rwanda leo wapo vizuri.
Jumapili ni Magufuli tu.
Naomba nieleweke kuwa ni kweli pasipo shaka kabisa John Magufuli mgombea urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia CCM ana upeo mdogo sana wa kuchanganua mambo! Hajui kitu kinachoitwa kanuni za utawala bora!
Jana nimemsikia akisema eti yule mtu mwenye ghorofa aliyezuia bomba la maji lisipite angekuwa yeye ndiye mwenye mamlaka angemvunjia kwa nguvu! Huyu ndiye mtu anayepigiwa chapuo kuwa rais wa nchi!
Bomba unataka upitishe kwenye nyumba ya mtu kimabavu tu eti kwa kuwa una mamlaka? Nini maana ya mahakama? Hujui na wala huitambui hadhi ya mahakama? Ama kweli sasa naanza kuwaelewa Kikwete na Pinda kwanini walikuwa wanamzima hadharani! Huyu
mtu anaweza kusababisha taifa lenye migogoro mikubwa nje na ndani!
Juzi nilifanya mahojiano na waziri Fenela Mkangala kaniambia kuwa Magufuli alikuwa akipewa fedha kidogo za bajeti kwenye kikao cha mawaziri kulikuwa hakukaliki! Alitaka awe yeye kwanza na anadiriki kusema wizara ya fulani haina maana hizo hela nipeni mimi! Hata hivyo bado miradi mingi haina ubora, kwa nini?
Lipo jambo lingine la 'mahakama ya mafisadi' sijui ataipa tafsiri gani kwenye mfumo wa mahakama! Au anataka kuunda mahakama ya kijeshi? Maana lazima iwe ndani ya mfumo wa kimahakama. Yote tisa kwani mahakama zilizopo zimezidiwa mpaka kuanzishwa mahakama (sijui ya kijeshi? ) Magufuli hajui kuwa kabla ya kumfunga mtu kuna kesi? Hajui kuwa kuna kushinda na kushindwa mahakamani? Ukipeleka mtuhumiwa mahakamani then akashinda utashinikiza afungwe eti kwa kuwa ni lazima umfunge?
Kesi ni lazima iamuliwe na hukumu ikitoka imetoka unashinda au umeshindwa! Labda ukate rufaa!!
Akiwa Chato juzi nikamsikia akisema "nitakutia ndani" sijui alikuwa anamwambia nani? Unamtiaje mtu ndani hujampeleka mahakamani?
Kwa kweli kuwa na kiongozi anayekurupuka hovyohovyo kama Magufuli! Hapana!
.............................
Alipokuwa Arusha alisema hadharani kuwa kiwanda cha Tanelec kimefungwa na kingeweza kuzalisha viatu bora kabisa vya ngazi. Akaomba apewe kura ili akifungue akiwa rais! Masikini kiwanda chenyewe kinazalisha vifaa vya hali ya juu kabisa vya umeme e. g Transfoma!
Leo nimefanya utafiti kuhusu lile bomba alilosema jana kumbe nalo lilishatandazwa siku nyingi ila hela ya kumalizia kazi imekosekana hali iliyowafanya wachina wasitishe kufanya kazi!
Leo akiwa Mbezi mwisho waziri Mkangara kashindwa kumuandalia mkutano kutokana na mwitikio hafifu wa watu. Cha ajabu hiyo imekuwa ajenda kwenye mikutano iliyofuata! Anamchanachana waziri wake hadharani akimuita mzembe! Sijui alitaka hao watu awatapike?
Ulitaka aongee dakika 3 kama mgombea wako?
Lowasa kila uchao ni kulalamika Ameonewa. Magufuli Nyapara Mkuu anakuja hatutaki Uzembe tumechoka.
Hasara za KUKURUPUKA.....
Alivunja nyumba za wakazi wa kimara akisema barabara ilipimwa mwaka 1973, wakati barabara ya Dar es salaam - Morogoro miaka hiyo ilikuwa ni Pugu Road....fidia serikali inatakiwa kulipa bilioni 12
Alivunja kituo cha mafuta cha Mansoor pale makongoro mwanza...mahakama ikaamuru serikali ilipe fidia bilioni 4.
Alikamata samaki kwenye bahari huru....serikali imeshindwa kesi na sasa wanatakiwa kwanza kulipa ,eli bilioni 12, samaki walitulisha hasara ya kuwahifadhi na sasa tunatakiwa kulipa.
Alivunja mkataba wa Konoike wa ujenzi wa barabara kati ya Dodoma na Manyoni ...Tanroad wakawalipa Konoike bilioni 120
The list goes on..
Cha msingi Mh. Magufuli anahitaji Kiiongozi juu yake MKURUPUKAJI
Mimi nitampigia kura yangu ya thamani EDWARD NGOYAI LOWASSA pamoja na Diwani na Mbunge wa UKAWA!!..Kwa maisha bora ya kwako na ya Kizazi chako Ondoa CCM,kwani imeishiwa pumzi na imeshindwa kutatua matatizo ya Ujinga,maradhi,Umaskini na Ufisadi.(CCM ni jumba la MAFISADI) !!!! ALUTA Continua, Victoria Ascerta.... The Struggle Continues, Victory is Certain; ...Mapambano yanaendelea, Ushindi unakuja!!
Nchi ilipofika inataka Kiongozi muadilifu anayepiga vita Rushwa na kila aina ya Ufisadi kama Magufuli amejipambanua.
Lowasa kwa kauli yake amesema Swala la kupiga vita Rushwa na Ufisadi ni Gumu hawezi mpaka ufanyike mchakato, tunatakaTingatinga, Mzalendo NYAPARA nchi inyooke.
Piga Kura kwa Magufuli kwa mabadiliko ya kweli
Mkuu unapoongea uwe na reference. Wizara ya ujenzi iliyo chini ya maguguli inaongeza kwa rushwa huko kujipambanua kwa magufuli kupambana na rushwa ni kupi huko?
Manunuzi ya ile meli ya bagamoyo yamezingirwa na rushwa tupu-zero value for money. Ugawaji wa nyumba zetu ulizingirwa na aina zote za rushwa zikiwemo za ngono, kujipambanua kwa magufuli kuko wapi? Ningemwelewa kama angesafisha wizara alizoongoza lakini zote zinanuka rushwa!
Bwana mdogo, ni bora kuwa na dikteta mwenye maarifa na mbunifu anayejua taratibu za utawala kuliko Rais mtakatifu lakini mjinga, asiye na maono na kujua taratibu za utawala yaani mbumbumbu.Hata Kagame nasikia ni dikteta ndio maana Rwanda leo wapo vizuri.
Jumapili ni Magufuli tu.