John Magufuli ni mweupe kwelikweli, sijui huo urais aliwaza nini kugombea!

kwa namna alivyojibu maswali jana BBC. Luwasa sitampa kura yangu. Ni mtupu kichwani haijapata tokea.
 
Hata Kagame nasikia ni dikteta ndio maana Rwanda leo wapo vizuri.

Jumapili ni Magufuli tu.
Kagame ni thinker mwenye akili na vision ya muda mrefu kwa nchi yake. Siyo mkurupukaji. Sijasikia vision ya Magufuli zaidi ya kuongelea miradi kwenye kampeni zake.
 
Tunamtaka huyo huyo comedian, mkurupukaji na dictator Mara mia zaidi ya lowasa
 
Naomba nieleweke kuwa ni kweli pasipo shaka kabisa John Magufuli mgombea urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia CCM ana upeo mdogo sana wa kuchanganua mambo! Hajui kitu kinachoitwa kanuni za utawala bora!

Jana nimemsikia akisema eti yule mtu mwenye ghorofa aliyezuia bomba la maji lisipite angekuwa yeye ndiye mwenye mamlaka angemvunjia kwa nguvu! Huyu ndiye mtu anayepigiwa chapuo kuwa rais wa nchi!

Bomba unataka upitishe kwenye nyumba ya mtu kimabavu tu eti kwa kuwa una mamlaka? Nini maana ya mahakama? Hujui na wala huitambui hadhi ya mahakama? Ama kweli sasa naanza kuwaelewa Kikwete na Pinda kwanini walikuwa wanamzima hadharani! Huyu
mtu anaweza kusababisha taifa lenye migogoro mikubwa nje na ndani!

Juzi nilifanya mahojiano na waziri Fenela Mkangala kaniambia kuwa Magufuli alikuwa akipewa fedha kidogo za bajeti kwenye kikao cha mawaziri kulikuwa hakukaliki! Alitaka awe yeye kwanza na anadiriki kusema wizara ya fulani haina maana hizo hela nipeni mimi! Hata hivyo bado miradi mingi haina ubora, kwa nini?

Lipo jambo lingine la 'mahakama ya mafisadi' sijui ataipa tafsiri gani kwenye mfumo wa mahakama! Au anataka kuunda mahakama ya kijeshi? Maana lazima iwe ndani ya mfumo wa kimahakama. Yote tisa kwani mahakama zilizopo zimezidiwa mpaka kuanzishwa mahakama (sijui ya kijeshi? ) Magufuli hajui kuwa kabla ya kumfunga mtu kuna kesi? Hajui kuwa kuna kushinda na kushindwa mahakamani? Ukipeleka mtuhumiwa mahakamani then akashinda utashinikiza afungwe eti kwa kuwa ni lazima umfunge?

Kesi ni lazima iamuliwe na hukumu ikitoka imetoka unashinda au umeshindwa! Labda ukate rufaa!!

Akiwa Chato juzi nikamsikia akisema "nitakutia ndani" sijui alikuwa anamwambia nani? Unamtiaje mtu ndani hujampeleka mahakamani?

Kwa kweli kuwa na kiongozi anayekurupuka hovyohovyo kama Magufuli! Hapana!

.............................
Alipokuwa Arusha alisema hadharani kuwa kiwanda cha Tanelec kimefungwa na kingeweza kuzalisha viatu bora kabisa vya ngazi. Akaomba apewe kura ili akifungue akiwa rais! Masikini kiwanda chenyewe kinazalisha vifaa vya hali ya juu kabisa vya umeme e. g Transfoma!

Leo nimefanya utafiti kuhusu lile bomba alilosema jana kumbe nalo lilishatandazwa siku nyingi ila hela ya kumalizia kazi imekosekana hali iliyowafanya wachina wasitishe kufanya kazi!

Leo akiwa Mbezi mwisho waziri Mkangara kashindwa kumuandalia mkutano kutokana na mwitikio hafifu wa watu. Cha ajabu hiyo imekuwa ajenda kwenye mikutano iliyofuata! Anamchanachana waziri wake hadharani akimuita mzembe! Sijui alitaka hao watu awatapike?

Magufuli ni zuzu tu.
 
Ulitaka aongee dakika 3 kama mgombea wako?

Lowasa kila uchao ni kulalamika Ameonewa. Magufuli Nyapara Mkuu anakuja hatutaki Uzembe tumechoka.

Mimi nitampigia kura yangu ya thamani "EDWARD NGOYAI LOWASSA" pamoja na "Diwani na "Mbunge" wa UKAWA!!..Kwa maisha bora ya kwako na ya Kizazi chako Ondoa CCM,kwani imeishiwa pumzi na imeshindwa kutatua matatizo ya Ujinga,maradhi,Umaskini na Ufisadi.(CCM ni jumba la MAFISADI) !!!! "ALUTA Continua, Victoria Ascerta".... "The Struggle Continues, Victory is Certain"; ...Mapambano yanaendelea, Ushindi unakuja!!
 
Hasara za KUKURUPUKA.....

Alivunja nyumba za wakazi wa kimara akisema barabara ilipimwa mwaka 1973, wakati barabara ya Dar es salaam - Morogoro miaka hiyo ilikuwa ni Pugu Road....fidia serikali inatakiwa kulipa bilioni 12
Alivunja kituo cha mafuta cha Mansoor pale makongoro mwanza...mahakama ikaamuru serikali ilipe fidia bilioni 4.

Alikamata samaki kwenye bahari huru....serikali imeshindwa kesi na sasa wanatakiwa kwanza kulipa ,eli bilioni 12, samaki walitulisha hasara ya kuwahifadhi na sasa tunatakiwa kulipa.

Alivunja mkataba wa Konoike wa ujenzi wa barabara kati ya Dodoma na Manyoni ...Tanroad wakawalipa Konoike bilioni 120
The list goes on..

Cha msingi Mh. Magufuli anahitaji Kiiongozi juu yake MKURUPUKAJI
 
Tutaelewana tu kuhusu huyu mtu! Ni bomu kwelikweli na kuona vya wenzake siyo kitu! Alikuwa akiwadharau sana wenzake ndani ya serikali!! Na kujikweza kwa misifa!!
 
Haamini katika uongozi wa pamoja.,na kwa misingi hiyo anaamini ni yeye pekee awezae kufanya kazi yenye tija.hawaamini wenzake,haiamini serikali yake,hawaamini wenzake afanyao kazi nao serikalini.anaamini katika kuyabeba majukumu yeye mwenyewe. Hafai kuwa raisi.
 
magufuli hajawahi toa maamuzi hayo ya kidikteta yenye maslahi ya nchi mengi yamelitia taifa hasara mfano meli ya wachina kituo cha mafuta kule mwanza Nyumba ya tanroad ubungo kuchomea wananchi nyavu zao kuvunja nyumba za watu bila fidia kisa tu eti ni lazima barabara ipite.
 
Hasara za KUKURUPUKA.....

Alivunja nyumba za wakazi wa kimara akisema barabara ilipimwa mwaka 1973, wakati barabara ya Dar es salaam - Morogoro miaka hiyo ilikuwa ni Pugu Road....fidia serikali inatakiwa kulipa bilioni 12
Alivunja kituo cha mafuta cha Mansoor pale makongoro mwanza...mahakama ikaamuru serikali ilipe fidia bilioni 4.

Alikamata samaki kwenye bahari huru....serikali imeshindwa kesi na sasa wanatakiwa kwanza kulipa ,eli bilioni 12, samaki walitulisha hasara ya kuwahifadhi na sasa tunatakiwa kulipa.

Alivunja mkataba wa Konoike wa ujenzi wa barabara kati ya Dodoma na Manyoni ...Tanroad wakawalipa Konoike bilioni 120
The list goes on..

Cha msingi Mh. Magufuli anahitaji Kiiongozi juu yake MKURUPUKAJI

Kwa huyu jamaa kungekua na uwezekano wa kubadili mgombea kikwete angembadilisha ni kilaza mno, na ndiyo maana kikwete anamchukia lowasa make ndiye kasababisha huyu achaguliwe hakua chaguo la ccm.
 
Mimi nitampigia kura yangu ya thamani “EDWARD NGOYAI LOWASSA” pamoja na “Diwani na “Mbunge” wa UKAWA!!..Kwa maisha bora ya kwako na ya Kizazi chako Ondoa CCM,kwani imeishiwa pumzi na imeshindwa kutatua matatizo ya Ujinga,maradhi,Umaskini na Ufisadi.(CCM ni jumba la MAFISADI) !!!! “ALUTA Continua, Victoria Ascerta”.... “The Struggle Continues, Victory is Certain”; ...Mapambano yanaendelea, Ushindi unakuja!!

Nchi ilipofika inataka Kiongozi muadilifu anayepiga vita Rushwa na kila aina ya Ufisadi kama Magufuli amejipambanua.

Lowasa kwa kauli yake amesema Swala la kupiga vita Rushwa na Ufisadi ni Gumu hawezi mpaka ufanyike mchakato, tunatakaTingatinga, Mzalendo NYAPARA nchi inyooke.

Piga Kura kwa Magufuli kwa mabadiliko ya kweli
 
Mkuu unapoongea uwe na reference. Wizara ya ujenzi iliyo chini ya maguguli inaongeza kwa rushwa huko kujipambanua kwa magufuli kupambana na rushwa ni kupi huko?

Manunuzi ya ile meli ya bagamoyo yamezingirwa na rushwa tupu-zero value for money. Ugawaji wa nyumba zetu ulizingirwa na aina zote za rushwa zikiwemo za ngono, kujipambanua kwa magufuli kuko wapi? Ningemwelewa kama angesafisha wizara alizoongoza lakini zote zinanuka rushwa!
 
CCM usanii umewaponza
Mnasema mawaziri wakuu hawakuleta maendeleo lakini hamsemi waziri wenu mkuu ataletaje maendeleo, mnasema kitu kimefanyika kwenye awamu ya mkapa na awamu ya kikwete lakini hapo hapo mnasema mawaziri wakuu na mshauri wa raisi kwa awamu zote hizo ni mafisadi na waliwarudisha nyuma
Kwa nini tu msiseme ukweli kuwa sera zenu zina matatizo? Hakuna atayeweza kutukwamua kiuchumi ndani ya sera zenu ameshindwa sumaye na mkapa, ameshindwa mwinyi , ameshindwa kikwete na pinda ...hakuna atayeweza full stop!!

Sasa mmkalia uongo tu, na unafiki wa kushangaa elimu bure hadi chuo kikuu wakati mkishangilia elimu bure hadi form four!!!! Hivi kati ya wanafunzi wanaomaliza form four wanafunzi wanaokwenda form five nchi nzima ni wangapi na wangapi wanaenda vyuoni, kama mtu anaweza kufanya elimu bure hadi form four anashindwa nini kuifanya bure hadi chuo kikuu??

Ati mtakamata mafisadi, kwani kinachowafanya msiwakamate sasa hivi nini? Mahakama hizihizi mbona zilimfunga Yona na Mramba? Mbona Hao mafisadi mmnaokula nao sahani moja mnawanadi kwenye ubunge??

Lowasa sio fisadi, kama angekuwa fisadi mngekuwa mmeshamsweka jela alipo hamia ukawa kwa jinsi mbavyomchukia

Tunataka mabadiliko ya sera na katiba, hayo ndiyo mabadiliko ya kweli na yeyote anayetusapoti kwa hilo tunamsapoti hatutaki mabadiliko ya sura kumtoa kikwete na kumuweka magufuli wakati kila kitu kipo palepale!

Sera za kuiweka nchi kwenye umaskini, ufisadi, mikopo na kuomba omba mwisho keshokutwa!!!!
 
Mkuu unapoongea uwe na reference. Wizara ya ujenzi iliyo chini ya maguguli inaongeza kwa rushwa huko kujipambanua kwa magufuli kupambana na rushwa ni kupi huko?

Manunuzi ya ile meli ya bagamoyo yamezingirwa na rushwa tupu-zero value for money. Ugawaji wa nyumba zetu ulizingirwa na aina zote za rushwa zikiwemo za ngono, kujipambanua kwa magufuli kuko wapi? Ningemwelewa kama angesafisha wizara alizoongoza lakini zote zinanuka rushwa!

Ondoa Mahaba yako ili uweze kuuona utendaji wa Magufuli
 
Hata Kagame nasikia ni dikteta ndio maana Rwanda leo wapo vizuri.

Jumapili ni Magufuli tu.
Bwana mdogo, ni bora kuwa na dikteta mwenye maarifa na mbunifu anayejua taratibu za utawala kuliko Rais mtakatifu lakini mjinga, asiye na maono na kujua taratibu za utawala yaani mbumbumbu.
 
32 Reactions
Reply
Back
Top Bottom