John Magufuli ni mweupe kwelikweli, sijui huo urais aliwaza nini kugombea!

G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
11,555
35,874
Naomba nieleweke kuwa ni kweli pasipo shaka kabisa John Magufuli mgombea urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia CCM ana upeo mdogo sana wa kuchanganua mambo! Hajui kitu kinachoitwa kanuni za utawala bora!

Jana nimemsikia akisema eti yule mtu mwenye ghorofa aliyezuia bomba la maji lisipite angekuwa yeye ndiye mwenye mamlaka angemvunjia kwa nguvu! Huyu ndiye mtu anayepigiwa chapuo kuwa rais wa nchi!

Bomba unataka upitishe kwenye nyumba ya mtu kimabavu tu eti kwa kuwa una mamlaka? Nini maana ya mahakama? Hujui na wala huitambui hadhi ya mahakama? Ama kweli sasa naanza kuwaelewa Kikwete na Pinda kwanini walikuwa wanamzima hadharani! Huyu
mtu anaweza kusababisha taifa lenye migogoro mikubwa nje na ndani!

Juzi nilifanya mahojiano na waziri Fenela Mkangala kaniambia kuwa Magufuli alikuwa akipewa fedha kidogo za bajeti kwenye kikao cha mawaziri kulikuwa hakukaliki! Alitaka awe yeye kwanza na anadiriki kusema wizara ya fulani haina maana hizo hela nipeni mimi! Hata hivyo bado miradi mingi haina ubora, kwa nini?

Lipo jambo lingine la 'mahakama ya mafisadi' sijui ataipa tafsiri gani kwenye mfumo wa mahakama! Au anataka kuunda mahakama ya kijeshi? Maana lazima iwe ndani ya mfumo wa kimahakama. Yote tisa kwani mahakama zilizopo zimezidiwa mpaka kuanzishwa mahakama (sijui ya kijeshi? ) Magufuli hajui kuwa kabla ya kumfunga mtu kuna kesi? Hajui kuwa kuna kushinda na kushindwa mahakamani? Ukipeleka mtuhumiwa mahakamani then akashinda utashinikiza afungwe eti kwa kuwa ni lazima umfunge?

Kesi ni lazima iamuliwe na hukumu ikitoka imetoka unashinda au umeshindwa! Labda ukate rufaa!!

Akiwa Chato juzi nikamsikia akisema "nitakutia ndani" sijui alikuwa anamwambia nani? Unamtiaje mtu ndani hujampeleka mahakamani?

Kwa kweli kuwa na kiongozi anayekurupuka hovyohovyo kama Magufuli! Hapana!

.............................
Alipokuwa Arusha alisema hadharani kuwa kiwanda cha Tanelec kimefungwa na kingeweza kuzalisha viatu bora kabisa vya ngazi. Akaomba apewe kura ili akifungue akiwa rais! Masikini kiwanda chenyewe kinazalisha vifaa vya hali ya juu kabisa vya umeme e. g Transfoma!

Leo nimefanya utafiti kuhusu lile bomba alilosema jana kumbe nalo lilishatandazwa siku nyingi ila hela ya kumalizia kazi imekosekana hali iliyowafanya wachina wasitishe kufanya kazi!

Leo akiwa Mbezi mwisho waziri Mkangara kashindwa kumuandalia mkutano kutokana na mwitikio hafifu wa watu. Cha ajabu hiyo imekuwa ajenda kwenye mikutano iliyofuata! Anamchanachana waziri wake hadharani akimuita mzembe! Sijui alitaka hao watu awatapike?
 
Kiukweli ni bora Kikwete 'dhaifu' kuliko Magufuli mkurupukaji.
Huyu jamaa akipewa nchi hata mwezi mmoja tu atasababisha vita.
Tuchukulie mfano wa mgogoro wa ziwa Nyasa kati yetu na Malawi Magufuli ndio angekuwa rais ingekuwaje?
Tuache ushabiki,Magufuli hafai kuwa rais.
 
Chief, watu wengi wanaofanya naye kazi wizara ya ujenzi wako perplexed na hii desperate move ya CCM kumsimamisha huyu jamaa kuwania urais. wanasema jamaa anaweza akawageuka hata wateuzi wake - and according to them CCM is likely kufia mikononi mwa Magufuli hata kama wakibahatika kupenya kwenye uchaguzi huu (a very unlikely situation of course).

wanadai jamaa si kiongozi kabisa, amekaa kiunyampara na u-foreman zaidi!
 
Kiukweli ni bora Kikwete 'dhaifu' kuliko Magufuli mkurupukaji.
Huyu jamaa akipewa nchi hata mwezi mmoja tu atasababisha vita.
Tuchukulie mfano wa mgogoro wa ziwa Nyasa kati yetu na Malawi Magufuli ndio angekuwa rais ingekuwaje?
Tuache ushabiki,Magufuli hafai kuwa rais.
Nchi ya wapenda dezo na kubembelezana inafikia ukomo wake soon. Hapa ni semi-dictatorship ili wote wapenda kubembelezwa mnyooke, huyu ndio nchi inamhitaji zaidi sasa hivi. Hamtaki nendeni kutafuta uraia Somalia.
 
Hata Kagame nasikia ni dikteta ndio maana Rwanda leo wapo vizuri.

Jumapili ni Magufuli tu.

Kagame si mkurupukaji na mropokaji kama Pombe. Kagame anaheshimu fani zingine kama wanasheria. Kwa ujinga magufuli akikariri kifungu cha sheria kama anayokariri kms za barabara anadhani kamaliza pasipokujua kwamba vifungu vya sheria vina tafsiri.
 
Kiukweli ni bora Kikwete 'dhaifu' kuliko Magufuli mkurupukaji.
Huyu jamaa akipewa nchi hata mwezi mmoja tu atasababisha vita.
Tuchukulie mfano wa mgogoro wa ziwa Nyasa kati yetu na Malawi Magufuli ndio angekuwa rais ingekuwaje?
Tuache ushabiki,Magufuli hafai kuwa rais.

Wewe nifah kazi unayoweza ni kupakaa mdomo hiyo rangi, vingine huviwezi. Diplomasia inataratibu zake. Kwa kuwa ni mgumu kuelewa jua tu, anayefaa yupo kwenye kazi ya kampeni mchague tr 25/10/ awe Rais wako wa Tanzania.
 
Hata Kagame nasikia ni dikteta ndio maana Rwanda leo wapo vizuri.

Jumapili ni Magufuli tu.
Dikteta haimanishi kufanya maamuzi kabla ya kufanya uchambuzi wa kutosha.

Tofauti kati ya Mgufuli na Lowasa ni kwamba Lowasa anaongea jambo baada ya kulifanyia analysis lkn Magufuli Anaongea ndipo anafanya analysis.
 
Kwa nchi ilipofika ni bora udikteta iki tunyooke na ndipo tutaelewana, demokrasia ndiyo imetufikisha hapa. Waafrika hatuwezi kuendelea kupitia mfumo huu wa kidemokrasia
 
Nilishasema hapa kuna siku tujajuta na kumtaka kikwete badala ya magufuri? Ivi huyu mkurupukaji asiejua hata kutatua migogoro ni mtu gani?

Anaendeshwa na hasira kuna siku ataruka kamba yaan tutoe unafiki makofuri ni mbovu kila sehemu hafai hata kuwa mjumbe wa nyumba kumi
 
32 Reactions
Reply
Back
Top Bottom