Uchaguzi 2020 John Magufuli, Hussein Mwinyi ndio watashinda Urais Bara na Visiwani

Deogratias Mutungi

Senior Member
Oct 1, 2019
137
179
Na Deogratias Mutungi

Nianze kwa kusema nia na dhumuni ya makala haya ni pana kimantiki na inalenga kuonyesha mitizamo ya mbali kisiasa aidha inajikita katika uchambuzi unaoegemea fungu la upande wa uwazi na ukweli bila kupendelea upande wowote ule kisiasa, mtu, wala chama chochote au itikadi ya namna yoyote ile isipokuwa tu kutumia vigezo na ishara muhimu za kisiasa zilivyo hapa nchini kwa sasa hasa kwa kipindi hiki tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu hapo Oktoba ili kuwapata Wabunge, Rais na Madiwani. Kwa mantiki hiyo uchambuzi huu ni huru unaozingatia misingi na mizania ya hoja ili kuupata ukweli wa mambo jinsi ulivyo katika medani zetu za kisiasa kulingana na dhana hii inayojengwa.

Aidha andiko hili si utabiri au unajimu wala astronomia unaojikita katika kubashiri nyota ya nini kitatokea, wala si kamali ya kubashiri siasa “ Political betting” bali ni uchambuzi wa kisayansi wa medani za siasa unaosimama ndani ya weledi na ubobevu wa kimantiki katika kuchambua mienendo ya siasa za ndani na watu wake, Ukweli unaposemwa na kujengewa hoja kisiasa si dhambi hata kama unapingana na kile kinachoaminiwa na upande wa pili kulingana na itikadi za vyama vyao, ni sharti ukweli usemwe na huo ndio utamaduni wa demokrasia tunayoihubiri na kuijengea hoja kila siku, demokrasia ni fungu la uhuru haki na ukweli wa kujenga hoja katika mstari wa kukosoana, tunakosoana kujenga na si kwa nia ya kubomoa.

Japo andiko hili linaelewa fika kuwa mfumo wa vyama vingi unaundwa na watu wenye matabaka tofauti tofauti, wengi wao wakiwa ni wale wasiotaka kusikia siasa za ukweli zenye kusimamia nadharia za kisayansi ndani yake jambo ambalo linaonyesha kukosekana kwa wanasiasa wenye ukomavu uliotukuka kisiasa, na makundi haya kwa wingi yapo katika mataifa yanayoendelea ikiwa ni pamoja na bara letu la Afrika, Kwa nini Afrika kwa sababu wanasiasa wengi ni magenge ya maslahi binafsi badala ya maslahi ya umma. Ni dhahiri kuwa uchambuzi wowote wa kisiasa unaosimamia ukweli wakati mwingine ujengewa uadui na vyama vingine vinavyodhani vinaonewa katika uchambuzi huo, Kisiasa huu ni upofu wa demokrasia dhidi ya tasnia ya habari.

Ifahamike wazi kuwa siasa ni sayansi na tabia ya sayansi uwa ni kutoa matokeo ya ukweli yasiyo na shaka kutoka mahabara, kwa nukta hiyo nikiri wazi kisiasa kuwa mantiki ilivyo kwa sasa inaonyesha mgombea wa Chama Cha Mapinduzi CCM Dkt. Magufuli ndiye mshindi wa nafasi ya urais kwa Tanzania bara, na Dkt. Hussein Mwinyi ndiye mshindi kwa upande wa Tanzania Visiwani hii ndio picha ya kimantiki inavyo onyesha na ni vigumu kuibishia kwa sababu inajitambulisha katika dhana zinazoonekana na kujitambulisha zenyewe huku zikiwa na mashiko ndani yake, Hoja hii inajengwa kidemokrasia kwa maana ya ushindi wa sanduku la kura na si vinginevyo.

Pengine tujiulize kwanini mantiki inaonyesha ushindi kwa viongozi hawa bila kuonyesha viongozi wa vyama vingine hususani vyama vya upinzani, Jibu ni matokeo ya historia, falsafa, sera na mifumo ya chama cha viongozi hawa, aidha hulka zao kisiasa ni mtaji mwingine juu ya ushindi wao unaojengewa hoja ndani ya makala haya, Kwa lugha nyepesi huu ndio utambulisho wa kimantiki juu ya ushindi wa Dkt. Magufuli na Dkt. Mwinyi.

Hata hivyo hili Msomaji wa makala haya aweze kuelewa vizuri nadharia ya somo hili na kupata ukweli na uhalisia wa hoja hii ya kimantiki inayojengwa ndani ya makala haya ni sharti ufafanuzi wa kina utolewe ili kuweka mambo sawa sawia napengine kuondoa shaka juu ya hoja hii inayojengwa kupitia andiko hili na kutoonekana niyakishabiki na yenye mrengo wa itikadi fulani yenye kupendelea upande mmoja.

Tukianza kudurusu hoja za kimantiki juu ya ushindi wa Dkt. Magufuli na Dkt. Mwinyi, turejee historia fupi ya uchaguzi wa mwaka 2015, uchaguzi ambao ulikuwa na hamasa kubwa ndani ya jamii ya Watanzania ukiwa umebebwa na dhana ya mabadiliko, Ukweli ni kwamba umoja wa upinzani wakati huo UKAWA ulifanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwashawishi watu kuamini sera, kauli mbiu na ilani ya umoja huo chini ya kiongozi wao Mzee Lowassa ambaye kwa njia moja au nyingine alionyesha ushindani wa hali ya juu kwa Chama Cha Mapinduzi CCM, huo ndio ukweli kisiasa.

Nguvu za Mzee Lowassa wakati huo hazikuwa za bahati mbaya bali mipango na mikakati yake aliyoiweka kwa muda mrefu akiusaka urais kwa namna yoyote ile japo Malaika wa riziki hakuwa upande wake, wote tunajua kilichotokea napengine Mungu alikuwa na kusudio lake la kutenda yote yaliyotokea, Bila shaka Mzee Lowassa ni shahidi wa kwanza juu ya nini kilitokea mwaka 2015.

Aidha mgombea wa CCM ambaye kwa sasa ndiye rais anayetetea muhula wake wa pili kwa kiasi kikubwa alionekana si maarufu sana kama ilivyokuwa kwa Mzee Lowasa baadhi ya watu walibeza na kumchukulia kama mtu wa kawaida sana katika ulingo wa siasa za Kitanzania, Pengine ni kwanini ilikuwa hivyo ni kwa sababu Lowassa aliutafuta urais kwa vipande vya fedha tofauti na Magufuli, hivyo umaarufu wake kwa njia moja au nyingine ni matokeo ya fungu la vipande vya fedha zilizokwenda kila sehemu ndani ya nchi hii.

Jambo ambalo kwa muda mrefu ndio limekuwa kidonda ndugu na anguko la nchi nyingi za kiafrika kuwapata viongozi wenye uwezo na weledi wa kutosha katika kutatua matatizo ya Waafrika wenyewe katika nyanja ya maendeleo, Kasumba yetu imekuwa ni kumchagua kiongozi aidha kwa sababu ya umaarufu wake au kwa sababu ya kutoa rushwa nyingi kwa wajumbe kwa maana hiyo tunazo siasa za kupima mtu kwa kumuangalia sura bila kupima dhamira yake na uwezo wake kiutendaji ukoje na ndio sehemu kubwa ya umaskini wetu Watanzania na Waafrika kwa ujumla unapoanzia kwa kuwapata viongozi wabovu kwa sababu ya kukubali rupia inunue utu na haki zetu za kikatiba.

Makala haya yanaamini kama Dkt. Magufuli angejitambulisha kwa kusema ndani ya miaka mitano atakuwa amefanya haya tunayoyaona sasa naamini hakuna Mtanzania yoyote Yule ambaye angeweza kumuamini na kumtuma Ikulu awe rais wetu bali wangempiga vijembe na kumuona ni muongo na mwenye ahadi ambazo hatoweza kuzitekeleza kwa sababu ni vitu ambavyo kwetu Watanzania ilikuwa ni adimu kuviona vikitekelezwa kwa kiwango tunachokiona sasa hivyo kuamini kwa kuambiwa kwa namna moja au nyingine ilikuwa ni ngumu sana kushawishi umma kuamini ahadi hizo zaidi ya kufikiri ni hadithi za kusadikika.

Kwa mantiki hiyo hoja mojawapo ya ushindi wa Dkt. Magufuli katika uchaguzi wa mwaka huu hapo Oktoba imejikita kwenye uaminifu uliopo ndani mioyo ya watanzania juu yake dhidi ya utendaji uliotukuka na usio na upinzani wa aina yoyote ile. Kasi ya ufanisi wa sasa wa serikali ya awamu ya tano ni matokeo ya vitu ambavyo Dkt. Magufuli mwaka 2015 hakuaidi kuvifanya lakini kwa sababu ya ubunifu wake na weledi wa serikali yake katika ukusanyaji wa kodi na matumizi bora ya rasilimali za nchi yanampa tiketi ya moja kwa moja kuchaguliwa kama rais wa muhula wa pili ndani ya serikali ya awamu ya tano.

Bila shaka wapiga kura watajiuliza maswali lukuki ikiwa ni pamoja na hili, kama Dkt. Magufuli ameweza kutekeleza agenda za muda mrefu za wapinzani na kufikia malengo kwa kasi ya ajabu ya miradi mbalimbali kwa kila eneo la nchi yetu ndani ya kipindi kifupi itakuwaje akiongezewa kipindi kingine cha miaka mitano.

Aidha mambo mengi yaliyo nje ya ilani ya chama chake yametekelezwa kwa kasi inayokubalika iweje mtu huyu asiginwe pembeni na asipewe fursa tena ya kuwatumikia Watanzania, Yote haya yanaweza kuwa maswali kwa wapiga kura ili kuwapima wagombea wote watakaojitokeza kushindanishwa na Dkt. John Pombe Magufuli

Kwa mantiki hiyo kupitia uwezo, misimamo na mafanikio ya Dkt. Magufuli kwa Watanzania ndipo tunapoweza kujenga hoja juu ya Dkt. Mwinyi ambaye ushindi wake kwa Tanzania visiwani ni matokeo ya mfumo wa kisiasa ulivyo kwa sasa kutokana na ufanisi wa maendeleo yanayoonekana kwa macho kupitia chama chenye kusimamia sera, ilani na falsafa moja yenye mrengo wa ukombozi.

Aidha andiko hili linazijua vyema siasa za Zanzibar zilivyo ,na ushindani uliotukuka hata hivyo siasa hizo utegemea ni nani anapambana na nani, kwa jinsi ilivyo Dkt. Mwinyi atapambana na Maalim Seif wa ACT-Wazalendo, Kwa mantiki ya kawaida Dkt, Mwinyi anauzika kuliko Maalim Seif anavyouzika hasa zama hizi za kizazi kinachohitaji mawazo mapya, nguvu mpya na ubunifu uliotukuka katika kufikia maendeleo ya kweli yenye nia njema ya kukomboa Wazanzibar kiuchumi, Aidha umahiri na uchapakazi wa Dkt. Mwinyi ni turufu nyingine mujarabu inayompa nafasi ya ushindi mnono dhidi ya mpinzani mwenzake kutoka ACT-Wazalendo, Uchambuzi huu ni kwa mujibu wa mtazamo wa kimantiki kwa kuzingatia mazingira ya sasa kisiasa yalivyo na kulinganisha maoni ya Watanzania yalivyo juu ya nani anafaa kuwa rais kwa kipindi hiki tunapoelekea Oktoba 28.
 
Uchambuzi wa andiko hili kamwe ahuusiani na dosari zozote zile zilizojitokeza kwenye uchaguzi mkuu.
Siku hizi naona kila mmoja anakana alichokisema wakati wa utawala wa mkono wa mtu mmoja. Alianza Kheri James na sasa naona na wewe umeanza maungamo. Ila ni vizuri maana Pasaka amechinjwa mwanakondoo. Ila Deo jaribuni kutumia hekima. Mungu hadhihakiwi maana yeye sio mwanadamu.
 
Siku hizi naona kila mmoja anakana alichokisema wakati wa utawala wa mkono wa mtu mmoja. Alianza Kheri James na sasa naona na wewe umeanza maungamo. Ila ni vizuri maana Pasaka amechinjwa mwanakondoo. Ila Deo jaribuni kutumia hekima. Mungu hadhihakiwi maana yeye sio mwanadamu.
Ndugu Mromboo mie ni mwanademokrasia Aidha natumia hekima katika Kujenga hoja, sina chuki na visasi katika ulingo wa siasa, Nikutakie Pasaka njema.
 
Ndugu Mromboo mie ni mwanademokrasia Aidha natumia hekima katika Kujenga hoja, sina chuki na visasi katika ulingo wa siasa, Nikutakie Pasaka njema.
Asante sana Deo. Hata ukimuuliza Kheri James leo atasema yeye ni muumini mzuri sana wa umoja wa kitaifa. Nakutakia pasaka njema sana kaka wewe na familia yako.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom